Familia ya Ali Khamenei: Nani aliuawa na nani angali hai?

Chanzo cha picha, Getty Images
Ripoti za kuuawa kwa baadhi ya ndugu wa kiongozi wa zamani wa Iran, Ali Khamenei, zimeibua maswali kuhusu ni nani bado wamesalia katika familia hiyo.
Pia kuna maswali kuhusu ni wake wangapi ambao Ali Khamenei alikuwa nao, na ni nani miongoni mwa wanafamilia wake wa alikuwa karibu nao zaidi.
Wakati wa uongozi wake, Ali Khamenei aliwapa nafasi za uongozi na kazi wengi wa wanafamilia wake.
Hata hivyo, baadhi ya ndugu zake baadaye waligeuka kuwa wapinzani wake, wengine walifungwa jela, na wengine walikimbilia katika nchi za kigeni.
Ripoti hii imekusanya taarifa zilizopo kuhusu familia ya kiongozi huyo wa zamani wa Iran.

Nani alifariki pamoja na Ali Khamenei?
Mbali na kiongozi huyo wa kidini kuuawa katika shambulio lililotekelezwa na Marekani na Israel, naibu wake, Mansoureh Khojasteh Bagherzadeh, pia alifariki dunia siku tatu baada ya shambulio hilo.
Vyombo vya habari vya Iran vilithibitisha habari hiyo, vikisema kuwa alipata majeraha mabaya katika shambulio hilo yaliyomwacha katika hali mahututi.
Tangu Khamenei alipokuwa kiongozi mkuu wa Iran, picha za mwanamke huyo zimekuwa zikitolewa hadharani mara chache sana.
Kulingana na ripoti mbalimbali, kulikuwa na baadhi ya wanafamilia wake waliouawa katika shambulio hilo, wakiwemo; Zahra Haddad Adel, mke wa Mojtaba Khamenei, Kiongozi Mkuu mpya wa Iran,Misbah-ul-Hada Bagheri Kani, mkwe wake, pamoja na Hoda Khamenei.
Pia aliyeuawa alikuwa Zahra Mohammadi Golpayegani, binti wa miaka 14 wa Bashar Khamenei.
Baba, mama na babu wa Khamenei
Hossein Tafreshi Khamenei, mwalimu wa dini kutoka mkoa wa Tabriz, ni babu wa Ali Khamenei.
Hossein Mojtahid Khamenei, baba wa Ali Khamenei, alimuoa mwanamke wa Kituruki aliyeitwa Mah Khanun.
Walizaa mtoto aliyeitwa Javad Hosseini Khamenei.
Javad alizaliwa katika mji wa Najaf, kabla ya kuhamia Tabriz, na baadaye Mashhad ambako aliishi huko.
Javad Hosseini Khamenei alikuwa imamu wa msikiti wa Waturuki mjini Mashhad.
Ndugu zake khamenei
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mohammad Khamenei ni mtoto wa kiume mkubwa katika familia, na anamzidi Ali Khamenei na miaka minne. Alizaliwa mwaka wa 1935 na alisomea sheria katika chuo kikuu cha Tehran. Wakati wa utawala wa Khomeini, Mohammad Khamenei alikuwa mmoja wa wanachama wa baraza la wawakilishi wa kiongozi mkuu.
Rubabeh au Badr Sadat Khamenei, aliyezaliwa mwaka wa 1942, ni binti wa tatu katika familia, na alikuwa binti mdogo zaidi katika familia na binti wa kwanza katika familia aliyepata shahada ya chuo kikuu.Mume wake ni Ali Moradkhani Aranga.
Hadi Khamenei, aliyezaliwa mwaka wa 1947, ni mtoto wa nne wa kiume katika familia na ndugu wa Ali Khamenei, na alikuwa miongoni mwa washirika waliokuwa na uhusiano wa karibu na Ayatollah Ruhollah Khomeini.
Hassan Khamenei, aliyezaliwa mwaka 1950, ni mtoto wa kiume mdogo zaidi katika familia, na ndiye ndugu pekee ambaye si mwalimu.
Ali Khamenei alikuwa na dada watatu, ikiwa ni pamoja na Mahaifi, Fatemeh Soltan na Hamidreza Shamsollahi, pamoja na binti mwingine ambaye jina lake halijatangazwa.
Familia ya mama
Khadija Mirdamadi, mama wa Ali Khamenei, alikuwa mama wa vijana wanne na mabinti watano waliozaliwa na mke wa pili wa baba yake Mohammad, Hamid, Ali, na Safiyeh.
Familia ya baba
Baba wa Mir Hossein Mousavi, waziri mkuu wa nchi hiyo ni ndugu wa baba wa Ali Khamenei.
Baba wa Khamenei pia alikuwa na binti mmoja aliyeitwa Zahra Mousavi.
Mke wake
Mansoureh Khojasteh Bagherzadeh, mkazi wa Mashhad kutoka familia mashuhuri ya wafanyabiashara, aliolewa na Ali Khamenei akiwa na umri wa miaka 17, wakati Khamenei alikuwa na miaka 25.
Mansoureh Khojasteh alikuwa na ndugu sita, Hassan, Mohammad, Javad, Hossein, Marzieh, na Mehdi.
Mansoureh Khojasteh, ambaye alikuwa pamoja na mumewe wakati wa shambulio, alifariki dunia siku tatu baada ya shambulio lililo muua mumewe.
Mkwe wake
Vyombo vya habari vya Iran vilithibitisha kwamba Ayatollah Khamenei aliwazuia watoto wake kushiriki au kushikilia nafasi za juu serikalini. Badala yake, wanafanya kazi katika taasisi na idara kuu za nchi hiyo.
Mostafa, alizaliwa mwaka wa 1965, ndiye mtoto mkubwa wa kiume wa Ali Khamenei.
Alioa Saeideh Khoshvak, binti ya Azizollah Khoshvak, shabiki mkubwa wa Khamenei.
Mojtaba Khamenei, alizaliwa mwaka wa 1960, ni mwana wa pili wa kiume wa Ali Khamenei, na alikuwa na ushawishi mkubwa wakati wa utawala wa baba yake.
Zahra Haddad Adel, ambaye aliuawa katika shambulio la Marekani, ni mke wa Mojtaba.
Zahra alikuwa binti wa Gholam Ali Haddad Adel, aliyekuwa spika wa zamani wa bunge la Iran
Binti za Khamenei na waume zao
Bashar al-Khamenei, mmoja wa binti wawili wa Ali Khamenei, alizaliwa mwaka wa 1980.
Mumewe ni Mohammad Javad, mwana wa Mohammad Mohammadi Golpaygani, aliyekuwa mkuu wa idara katika ofisi ya kiongozi wa dini.
Mohammad Javad Mohammadi Golpaygani ni profesa wa dini katika chuo kikuu kilicho mjini Qom.
Inasemekana kwamba watoto wawili wa Bashar waliuawa siku ya shambulio lililolenga nyumba ya kiongozi huyo mkuu na wakafariki wakati mmoja.
Hoda Khamenei, binti wa Ali Khamenei, ndiye binti mdogo zaidi alizaliwa mwaka wa 1988.
Ameolewa na Misbah-ul-Hada Bagheri Kani, mwana wa Mohammad Bagheri Bagheri Kani.
Misbah-ul-Hada Bagheri ni profesa katika Chuo Kikuu cha Imam Sadeq nchini Iran.















