UN: Asilimia 90 ya ardhi ya kilimo inaweza kuharibiwa ifikapo 2050

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakulima walikuwa wakizika barafu yao ardhini ili kupima ubora wa udongo na kuangalia jinsi unavyooza haraka.
Kadiri bakteria na vijidudu vyenye afya zaidi kama vile fangasi zilivyokuwepo kwa kasi kitambaa kingeharibiwa.
Hata hivyo, wakati njia hii inajaribiwa siku hizi, kipande cha kitambaa kilichozikwa chini kinaweza kuondolewa kwa njia ile ile, hata baada ya mwaka, bila uharibifu wowote.
Wataalamu wanaripoti kuwa zaidi ya nusu ya ardhi inayotumika katika kilimo duniani imezorota.
Nchini India, ambayo imekuwa ikikabiliwa na matatizo makubwa katika kilimo hivi karibuni na inasemekana kuwa karibu watu 30 wanajiua kila siku, wakulima wanashirikisha kwamba uharibifu wa udongo ni moja ya sababu kubwa zaidi ya madeni.
Gwigi maarufu aitwaye Sadhguru, ambaye alitaka kupata tiba ya hali hii nchini India, alizindua kampeni ya kimataifa iitwayo SaveSoil.
Sadhguru, ndani ya wigo wa kampeni hiyo yenye lengo la kuboresha afya ya udongo, anadai wakulima wapewe motisha mbalimbali kuhifadhi viumbe hai kwenye udongo wao na kuweka angalau asilimia 3.
Sadhguru anasema, ‘’Tukiharibu hilo pia, udongo utageuka kuwa mchanga na hapo ndipo unapoishia. Ikiwa hatuwezi kukabiliana na tatizo la ardhi, itatulazimu kuishi jangwani.’’
Watu mara nyingi wametatizika katika historia na udongo duni.
David Montgomery, Profesa wa Geomorphology katika Chuo Kikuu cha Washington.
‘’Usipoupa udongo fursa ya kupona na ukiuharibu mara kwa mara, uzalishaji wa kilimo hautawezekana katika udongo huo. Sehemu yenye rutuba zaidi ya udongo ni tabaka la juu. Uzalishaji huu unaharibiwa na miaka na karne za shughuli za kilimo. Hivyo, inazidi kuwa vigumu kulima chakula.’’
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) linaripoti kwamba asilimia 33 ya ardhi ya dunia imeharibiwa, na hii inaweza kuongezeka hadi asilimia 90 ifikapo 2050.
Kulingana na FAO, inaweza kuchukua miaka 1,000 kujenga sentimita 2-3 tu za udongo wenye afya.
Kwa nini udongo unaharibika katika kilimo?
Kuna sababu nyingi za uharibifu wa udongo.
Kulisha mifugo kupita kiasi, upandaji wa aina moja ya mazao mfululizo, na matumizi ya dawa za kuua wadudu ni baadhi tu ya hayo.
Sababu nyingine inayoathiri vibaya udongo ni teknolojia ya kulima kwa kutumia jembe, ambayo imeleta mapinduzi makubwa katika kilimo na hutumika kuingiza hewa kabla ya kupanda shambani.
Matumizi ya teknolojia ya zamani ya kilimo cha trekta, imekuwa sehemu ya lazima ya kilimo.
Katika kilimo cha kisasa, udongo hugeuka ili kuondokana na magugu, lakini kwa kufanya hivyo, vijidudu ambavyo ni muhimu kwa afya vinaonekana chini ya udongo.
Vikiwa wazi juani, vijidudu hivi hufa na udongo hupoteza rutuba yake.
Lakini ukulima wa kutumia jembe, pamoja na zana nyingine za kilimo, bado inapendekezwa kwa sababu inapanua kiwango, kasi na tija ya kilimo, na kuwezesha ardhi zaidi kulimwa kwa ufanisi zaidi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ben Raskin, Mkuu wa Kilimo cha misitu na Kilimo cha mboga mboga katika Chama cha Ukulima nchini Uingereza, anasema dhima ya teknolojia katika kilimo inahitaji kutathiminiwa upya.
‘’Afya ya udongo na mimea inapaswa kuwa kipaumbele katika teknolojia,’’ anasema Raskin.
Katika mwelekeo huu, makampuni mengine yanaendeleza teknolojia mpya ambazo zitasababisha uharibifu mdogo kwa udongo.
Kwa mfano, badala ya zana zinazochimba ndani kabisa ya udongo, vipanzi vya mbegu vinavyotoboa mashimo madogo na kuacha mbegu ndani, na roboti zinazopanda mbegu na kusafisha magugu kwa njia nzuri na kama mbadala wake zinaundwa leo
Kwa upande mwingine, inasemekana kwamba mimea inayotumika kuzuia udongo kuwa wazi pia ni muhimu.
Raskin anashirikisha kwamba teknolojia zilizotumiwa hadi sasa zimechunguza tu uso wa udongo, na sasa ni muhimu kwenda ndani zaidi na kuzingatia biolojia ya udongo.
Wanasayansi wanafikiriwa kuwa wamegundua asilimia 10 tu ya maisha katika udongo.
Montgomery amesema kwa muda mrefu ‘’ulimwengu wa chini ya ardhi hauonekani kwa sayansi, udongo huo ndio mwisho katika ulimwengu wa sayansi.’’
Inapendekezwa kuwa kuelewa muundo wa udongo kunaweza pia kusababisha kuundwa kwa viwanda vipya kabisa.
Mfano ni teknolojia ya jeni ambayo hupanga vijidudu kwenye udongo ili kuwapa wakulima rutuba bora kwa udongo wao.
Kwa upande mwingine, inasemekana kwamba njia rahisi zaidi na za zamani zinaweza pia kuchangia mawazo ya kuvutia na makubwa.
Katika jaribio lililofanywa kama sehemu ya mpango wa Chama cha Ubunifu kwa Wakulima, matandazo ya machujo ya mitishamba yalimwagwa kuzunguka miti ili kukandamiza magugu na magonjwa.
Asidi katika matandazo ilipatikana ili kuchochea mmenyuko wa kinga katika miti.

Chanzo cha picha, AGROINTELLI
Kupima ubora wa udongo inakuwa rahisi.
Inafikiriwa kuwa udongo pia utawezesha ubunifu mkubwa katika nyanja ya dawa.
Kulingana na makala katika jarida la kisayansi la Chemistry World, vifaa vya asili katika vijidudu vya ndani ya udongo vinaweza kuwa muhimu sana kwa maudhui ya madawa ya kulevya.
Sumu iitwayo teixobactin, ambayo inaweza kutumika katika darasa jipya la kwanza la dawa za kuua vijasumu zilizotengenezwa baada ya mapumziko ya miaka 3, iligunduliwa kwa kuangalia sampuli za udongo.
Hata hivyo, kuchambua udongo inaweza kuwa ghali sana na kuchukua muda mrefu.
Wataalamu sasa wanachunguza njia za kufanya hivyo kwa kutumia simu zetu.
Jack Ingle, mkurugenzi wa Harvest Agri nchini Uingereza, anauza kifaa kiitwacho ‘microbiometer’ cha kupima udongo.
Wafanyakazi wa kilimo huchukua sampuli ya udongo wao, huimimina ndani ya bomba la majaribio lenye mchanganyiko maalum, na kisha kuihamisha kwenye karatasi.
Kisha, sampuli ya udongo inachanganuliwa na programu ya bure inayopatikana kwenye Android na iPhones na vijidudu ndani yake huchunguzwa.

Chanzo cha picha, HARVEST AGRI
Kwa upande mwingine, kundi la wanasayansi limeunda hifadhidata ya vipimo vya afya ya udongo kutoka duniani kote, inayoitwa SoilHealthDB.
Mwaka jana, Umoja wa Ulaya (EU) pia ulianzisha Shirika la Uangalizi wa Udongo la Umoja wa Ulaya ili kukusanya na kufuatilia data ya udongo na kusaidia utafiti wa udongo na maendeleo ya sera.
Montgomery anasema kwamba katika siku zijazo za teknolojia ya kilimo, lazima tuangalie siku za zamani.
“Tunaweza kuchukua maarifa ya zamani kama mzunguko wa mazao na kuyachanganya na teknolojia ya kisasa,” Montgomery anasema.















