Kombe la Dunia 2022: Sababu 3 zinazoifanya Ufaransa kuogopwa kabla ya fainali na Argentina

Safu hatari ya mashambulizi , kocha anayevunja rekodi na wachezaji ambao watashiriki katika kombe lao la pili la Dunia.

Barua ya Ufaransa ya kutambulishwa katika fainali dhidi ya Argentina Jumapili ijayo inaamrisha heshima.

The blues waliilaza Morocco 2-0 siku ya Jumatano, ufunuo mkubwa wa michuano hiyo, kupitia mabao ya Theo Hernández na Randal Kolo Muani.

Kulikuwa na mataifa makubwa matatu yaliovutia kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia: Ufaransa, Argentina na Brazil.

Mawili kati yao yatakutakana katika fainali siku ya Jumapili

Fainali hii itakuwa marudio ya hatua ya 16 bora ya Urusi 2018, wakati Gauls waliwashinda albiceleste kwa 4-3 ya kusisimua.

Tunachanganua sababu tatu zinazoifanya Ufaransa kuwa timu ya kutisha na na sehemu mbili za udhaifu wao ambazo Argentina inaweza kuzitumia.

Wana wafungaji 3 kati ya waliofunga mabao mengi zaidi katika Kombe la Dunia

Washambuliaji wa Ufaransa wamefunga magoli mengi na takwimu za magoli yao zinawatetea.

Kylian Mbappé ana mabao matano na ndiye mfungaji bora wa michuano hiyo pamoja na Lionel Messi. Olivier Giroud ana manne Pamoja na Antoine Griezmann mwenye magoli matatu.

Ni wachezaji hawa watatu pekee waliofunga mabao (12) ikilinganishwa na kikosi chote cha Argentina

Kuwa na nguvu hii ya kukera itakuwa changamoto kwa Argentina na mojawapo ya funguo za kulitetea kombe la Dunia

Didier Deschamps, Kocha anayevunja rekodi

Kocha huyo wa Ufaransa aliiongoza Ufaransa kutwaa Kombe la Dunia 2018 na sasa ameirudisha timu yake katika fainali ya 2022.

Kati ya michezo 18 ambayo Deschamps ameongoza Ufaransa kwenye Kombe la Dunia tangu Brazil 2014, ameshinda 14, amepoteza 2 na kufungwa 2.

Ushindi dhidi ya Morocco unamfanya kuwa sawa kwa idadi ya ushindi na Mbrazil Luiz Felipe Scolari na kumfanya ashinde mara mbili nyuma ya rekodi ya mechi 16 alizoshinda Mjerumani Helmut Schön.

Ingawa Jumapili ijayo Deschamps atakuwa na mpinzani mgumu.

Lionel Scaloni , mwenye uzoefu mdogo, ameweza kuwaongoza albiceleste kushinda Copa America na kufika fainali ya Kombe la Dunia katika kipindi cha miaka minne pekee.

Kizazi cha wachezaji walioshinda kombe la Dunia 2018

Ufaransa imehifadhi idadi kubwa ya wachezaji walioshiriki kombe la Dunia la 2018 nchini Urusi huko Qatar.

Wachezaji kadhaa kama vile kipa Hugo Lloris , mlinzi Raphael Varane na washambuliaji Kylian Mbappé, Olivier Giroud na Antoine Griezmann walishiriki katika fainali huko Moscow walipoichapa Croatia 4-2.

Ni kizazi ambacho tayari kina uzoefu katika fainali za Kombe la Dunia na ambacho ni muhimu kila wakati.

Katika timu ya Argentina, ni Messi na Ángel Di María pekee waliosalia kati ya wale waliopoteza fainali hiyo dhidi ya Ujerumani huko Brazil 2014.

Ufaransa ni timu ya kwanza kufuzu fainali za Kombe la Dunia mfululizo tangu Brazil mwaka 1994 na 1998.

Canarinha ilirudi fainali huko Korea na Japan mnamo 2002.

Mpungufu ya Ufaransa

1. Tatizo la kumaliza mechi bila kufungwa

Ni vigumu kupata udhaifu katika timu hii ya Ufaransa, lakini ukiangalia takwimu ni wazi kuwa wana matatizo ya kuzuia magoli

Kati ya michezo sita katika Kombe hili la Dunia wameruhusu mabao yote isipokuwa nusu fainali na Morocco, ambayo ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga.

Australia, Denmark, Tunisia, Poland, Uingereza. Wote waliweza kumfunga kipa Hugo Lloris.

Kwa kulinganisha, Argentina haikuruhusu mabao mara tatu: dhidi ya Mexico (2-0), Poland (2-0) na Croatia (3-0).

Hiyo inaweza kuwa moja ya udhoofu wao.

2.Safu ya kati isio na uzoefu

Ushindi mwingi wa Ufaransa mnamo 2018 ulitokana na safu dhabiti na ngumu ya kati ilioshirikisha wachezaji wanaotambulika kimataifa kama vile Paul Pogba, N'golo Kanté na Blaise Matuide.

Safu ya kiungo ya mwaka huu haiwezi kusemwa kuwa haina kipaji kidogo.

Aurélien Tchouaméni na Eduardo Camavinga ni wachezaji muhimu katika timu ya Real Madrid; Youssouf Fofana hana ubishi katika klabu ya Monaco kwenye ligi ya Ufaransa na Griezmann amelazimika kuwacha nafasi yake na kucheza kama kiungo wa kati na hivyobasi kufanya vizuri zaidi ya matarajio.

Lakini sio safu ya kati iliyojumuishwa na ustadi ambayo Ufaransa ilikuwa nayo mnamo 2018.

Hiyo inaweza kuwa pointi nyingine dhaifu ambayo Argentina inaweza kutumia dhidi ya timu hii imara.