Vita Ukraine : Marekani inataka kuidhoofisha Urusi

Ukrainian President Zelensky with Secretaries Austin and Blinken

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Bwana Austin (Kushoto) na bwana Blinken (kulia) ni miongoni mwa maofisa wa ngazi ya juu wa Marekani kutembelea Ukraine tangu Urusi iivamie Ukraine

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema ana matumaini kuwa Urusi itashindwa nchini Ukraine na kuwapa fundisho viongozi wake kutorudia vitendo vya namna hiyo mahali pengine.

Aliongeza kuwa Ukraine bado inaweza kushinda vita hivi ikiwa itapata ushirikiano unaofaa, na kupongeza juhudi za jeshi lake.

Jenerali huyo mstaafu wa nyota nne alisema Marekani itatenga dola milioni 713 (£559m) kwa ajili ya msaada wa kijeshi kwa Ukraine na mataifa mengine 15 ya kati na mashariki mwa Ulaya.

Bw Austin alizungumza hayo baada ya kukutana na Rais Volodymyr Zelensky mjini Kyiv.

Akiwa amesindikizwa na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken, ziara hiyo imekuwa ya kwanza kwa viongozi wa ngazi za juu zaidi nchini Marekani kufika Ukraine tangu uvamizi huo uanze zaidi ya miezi miwili iliyopita.

Mkutano kati ya Marekani na Ukraine, ambao ulifanyika kwa zaidi ya saa tatu, unajiri wakati Urusi ikizidisha kampeni yake ya kijeshi kusini na mashariki mwa nchi hiyo.

Katika mkutano na wanahabari nchini Poland baada ya ziara hiyo, Bw Austin aliwaambia wanahabari kwamba Marekani inataka kuona "Urusi ikidhoofika kiasi kwamba haiwezi kurudia kufanya mambo ambayo yanayafanya katika kuivamia Ukraine".

Mkuu huyo wa Pentagon aliongeza kuwa maafisa wa Marekani bado wanaamini kwamba Ukraine inaweza kushinda mzozo huo "ikiwa watakuwa na vifaa vinavyofaa" na "haki".

Mkuu huyo wa Pentagon aliongeza kuwa maafisa wa Marekani bado wanaamini kwamba Ukraine inaweza kushinda mzozo huo "ikiwa watakuwa na vifaa vinavyofaa" na "msaada sahihi".

Bw Putin alionekana kukubaliana na maoni ya Bw Austin wakati wa hotuba yake siku ya Jumatatu na kuzishutumu nchi za Magharibi kwa kujaribu "kuigawa Urusi na kuleta uhasama wa ndani".

Mwandishi wa BBC wa masuala ya kidiplomasia James Landale aliona kwamba maoni ya Bw Austin ya kutaka Urusi iliyodhoofika yalikuwa na nguvu isiyo ya kawaida kwa waziri wa ulinzi wa Marekani.

Ni jambo moja kusaidia Ukraine kupinga uvamizi wa Urusi, ni jambo lingine kabisa kuzungumzia kudhoofisha uwezo wa Urusi, alisema.

Ukrainian and US delegations meeting in Kyiv

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Bwana Zelensky alitoa wito wa msaada zaidi wa silaha kutoka mataifa ya magharibi

Wakati huo huo, maafisa wa ulinzi wa Marekani walisema kati ya mamilioni yaliyotangazwa katika ufadhili mpya wa kijeshi, ni dola milioni 332(£260m) zitatengewa Ukraine.

Hivyo jumla ya usaidizi wa ulinzi kutoka Marekani kwenda Ukraine tangu uvamizi huo uanze ni zaidi ya dola bilioni 332 (£2.9bn).

Bw Zelensky amekuwa akiwasihi viongozi wa nchi za Magharibi kuongeza msaada wa silaha za kijeshi kwa wiki kadhaa, akiahidi kwamba vikosi vyake vinaweza kulishinda jeshi la Urusi iwapo vitapewa ndege za kivita na magari mengine.

Wiki iliyopita Marekani ilithibitisha kuwa imewapa wanajeshi wa Ukraine mizinga ya hoitzer na rada za kukinga mizinga kwa mara ya kwanza.

Balozi wa Urusi mjini Washington alisema Moscow ilituma barua ya kidiplomasia kutaka kusitishwa kwa usambazaji wa silaha za Marekani kwa Ukraine.

Wakati huo huo, Bw Blinken alitangaza kwamba baadhi ya wafanyakazi wa kidiplomasia wa Marekani wataanza kurejea Ukraine kuanzia wiki ijayo.

Wanatarajiwa kuishi Lviv magharibi mwa Ukraine kwa muda mfupi na wana mpango wa muda mrefu wa kufungua tena ubalozi wa Marekani katika mji mkuu, Kyiv.

Taarifa hiyo imekuja wakati Ikulu ya White House ilipotangaza kuwa Rais Joe Biden ana nia ya kumteua Bridget Brink, mwanadiplomasia, kuwa balozi wa Marekani nchini Ukraine - wadhifa ambao umebaki wazi kwa zaidi ya miaka miwili.

Bw Blinken pia alitetea mtazamo wa kidiplomasia wa Marekani, akiwaambia waandishi wa habari kwamba muungano wa Magharibi ambao utawala wa Biden umeukusanya una shinikizo kwa utawala wa Rais Vladimir Putin.

"Mkakati ambao tumeweka, uungwaji mkono mkubwa kwa Ukraine, shinikizo kubwa dhidi ya Urusi, mshikamano na zaidi ya nchi 30 zinazoshiriki katika juhudi hizi, unaleta matokeo ya kweli," Bw Blinken alisema.

"Na tunaona kwamba linapokuja suala la malengo ya vita ya Urusi, Urusi inashindwa, Ukraine inafanikiwa."

"Ukraine huru itakuepo kwa muda mrefu zaidi kuliko ile ya Vladimir Putin kwenye eneo la tukio," Bw Blinken aliongeza.

Akizungumza kufuatia mkutano huo, Bw Zelensky alisema serikali yake inathamini "msaada ambao haujawahi kushuhudiwa" kutoka Washington na kuongeza kuwa "angependa kumshukuru Rais Biden binafsi na kwa niaba ya watu wote wa Ukraine kwa uongozi wake katika kuunga mkono Ukraine".

Unaweza pia kusoma

2px presentational grey line

Rais Biden aliweka wazi kuwa Marekani haitaingilia moja kwa moja vita vya Ukraine. Hatatuma wanajeshi wa Marekani kujiunga na vita.

Lakini ukweli ni kwamba Marekani inajihusisha zaidi - na hilo limesisitizwa na maneno ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani.

Marekani imeongeza kwa kiasi kikubwa usambazaji wa silaha kwa Ukraine katika wiki za hivi karibuni. Licha ya Urusi kutoa onyo, Marekani imesema itatuma zaidi.

Maneno ya Bw Austin yanasisitiza kwamba Marekani sio mtazamaji katika vita hivi. Marekani inataka kuona Urusi ikishindwa.

Zaidi ya hayo, inataka kuona silaha za kijeshi za Urusi zikipungua kiasi kwamba haitaweza kutishia mshirika mwingine yeyote wa Ulaya katika siku zijazo. Hofu inayowakilishwa na washirika wa Nato ni kwamba kushindwa kwa aina yoyote kwa Ukraine kutaimarisha tu matarajio ya Rais Putin.

Bw Austin sasa ameweka wazi kwamba Marekani ina malengo yake ya kimkakati kwa vita hivi - hata kama kinadharia haishiriki. Lengo ni kumzuia Rais Putin na kulidhoofisha jeshi la Urusi kiasi kwamba halitaweza tena kutishia mataifa mengine.

Kwa kiasi fulani hatua hiyo tayari imetokea. Wataalamu wa masuala ya kijeshi tayari wanaamini kwamba itachukua miaka kwa Urusi kupata nafuu kutokana na hasara zake za kijeshi. Hiyo inaweza pia kutuma ishara kwa taifa lingine ambalo Marekani inazidi kuwa na wasiwasi nalo - yaani China.

Kwa Rais Putin ni ushahidi zaidi kwamba hayuko tu katika vita na Ukraine.

Bila shaka simulizi yake mwenyewe kwa madhumuni ya usaidizi wa nyumbani. Kwa muda mrefu ameonesha Nato kama tishio kwa Urusi.

Lloyd Austin

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lloyd Austin

Katika siku za hivi karibuni Urusi imeelekeza nguvu zake katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine na vyanzo vya Marekani vinaamini kuwa Moscow imejitolea zaidi ya vikundi 76 vya kijeshi ndani ya Ukraine.

Siku ya Jumatatu, wizara ya ulinzi ya Uingereza ilisema kwamba Moscow imefanya maendeleo madogo katika eneo hilo lakini "bado haijapata mafanikio" kutokana na changamoto za vifaa.

Taarifa hiyo lilidai kuwa "utetezi wa Ukraine wa Mariupol pia umechosha vitengo vingi vya Urusi na kupunguza ufanisi wao wa mapigano".