Zimbabwe yakabiliwa na uhaba wa wauguzi baada ya wengi kwenda Uingereza

Nurse taking blood pressure

Hospitali za Zimbabwe zinakabiliwa na uhaba wa wauguzi baada ya idadi ya wauguzi wanaondoka nchini humo kwenda ughaibuni kutafuta unafuu wa maisha, ikiongezeka, Shingai Nyoka anaoandika.

Mwanamke yule mdogo aliyevaa gauni la kijani alikuwa na uchungu, uso wake ukiwa umejikunja kwa maumivu.

Bado kwa dakika moja na kisha akiugulia na kujikunyata huku na kule.

Nilisimama kwenye mlango uliokuwa nusu wazi nikichungulia ndani, nilikuwa na ruhusa ya kuwa pale lakini nilihisi nimeingilia masuala binafsi ya watu.

Wiki mbili kabla, kaimu afisa muuguzi mkuu wa mamlaka katika mji mkuu, Harare, Perpetua Kaseke, alikuwa amenionesha zahanati hii, Warren Park Polyclinic.

Anawajibika kuhudumia watumishi katika vituo vyote vya afya vya halmashauri.

Aliniambia kulikuwa na wauguzi wanne tu wa zamu kwa kliniki nzima, ambayo inahudumia mamia ya watu kila siku.

Mbili katika chumba cha wazazi, mmoja kwa wagonjwa wa nje na mwingine kwa huduma za familia. Kawaida wanahitajika walau angalau nane.

Tulipokuwa tukizungumza, muuguzi wa nyuma yangu - alikuwa akiongezewa majukumu yake maradufu, kushughulikia sehemu ya kujifungua na wodi za baada ya kujifungua, na kusaidia wajawazito.

Kumuona mwanamke mjamzito - akiwa katika uchungu peke yake katika wakati wake wa hatari zaidi - kwa hakika kulionyesha ukubwa wa tatizo.

Matron Kaseke aliniambia kuwa kliniki yake ina uwezo wa kuhudumia 50%. Nilihisi kuchanganyikiwa kwake - wauguzi wana kazi nyingi na aliniambia, na wanaendelea kujiuzulu.

Wauguzi kumi na wawili waliondoka mwezi uliopita peke yake.

Wengi wao wanaenda Uingereza au Ireland, wengine katika nchi jirani za Zimbabwe au kwa sekta ya kibinafsi.

Alisema inaweza kuwa ngumu kupanga wafanyakazi kutoka dakika moja hadi nyingine - wengine wanatoa notisi ya masaa 24 kabla ya kuondoka.

Hakuna hata muuguzi aliyetaka kuzungumza nami, ninashuku baadhi wanatayarisha karatasi zao na kujiandaa kuondoka.

Two nurses working at a desk
Maelezo ya picha, Wahudumu wakiangaika kutoa huduma wakiwa katika idadi ndogo

Uingereza imekuwa kwenye harakati ya kuajiri wataalamu wa matibabu ili kuziba uhaba wa wafanyakazi wake kwa sababu ya athari za janga na Brexit.

Zimbabwe kwa muda mrefu imekuwa ikiwalipa mishahara duni wafanyakazi wake wa sekta ya umma. Wauguzi walioajiriwa na halmashauri ya jiji wanapata zaidi kidogo kuliko wale wanaofanya kazi katika hospitali za serikali.

Lakini katika visa vyote viwili, muuguzi anayepokea mshahara wa chini kabisa anapokea nyumbani chini ya $200 (£150) kwa mwezi, inayotosha tu kulipia kodi ya nyumba ya vyumba viwili katika ujirani wa watu wenye kipato cha chini, lakini si vingine vingi. Na wamechoka na hali hiyo.

Bodi ya Huduma ya Afya ya serikali inasema kuwa zaidi ya wafanyakazi 2,200 wa matibabu waliacha kazi mwaka jana pekee: 900 kati yao walikuwa wauguzi.

Hii ilikuwa mara mbili ya idadi ya wafanyakazi walioondoka mnamo 2020 na mara tatu ya ile ya 2019.

Matron Kaseke aliniambia kuwa wakati mmoja kliniki tisa kati ya 43 za halmashauri ya Harare zilipunguza shughuli zao au kufungwa kabisa kwa kukosa wafanyakazi.

Shingai Nyoka
BBC
It wasn't always like this - public health facilities in Zimbabwe were once envied by other sub-Saharan African countries"
Shingai Nyoka
BBC reporter, Harare
1px transparent line

Nilitembelea Zahanati ya Matapi katika wilaya ya Mbare. Milango yake ilikuwa imefungwa.

Mbare ndicho kitongoji chenye watu wengi zaidi katika mji mkuu, na kinahitaji huduma hizi za afya.

Kundi la wanaume lilikuwa na shauku ya kutaka kujua ni taarifa gani nilikuwa nikifuatilia.

Walikuwa wakipokea matibabu katika kliniki hii, lakini sasa lazima wasafiri umbali mrefu na kusubiri kwa muda mrefu.

Katika zahanati ya karibu ambayo ingali inafanya kazi, wafanyakazi walikuwa wakijitahidi kusisitiza utulivu.

Katika sehemu ya nje ya kusubiria, muuguzi msaidizi ambaye ni mwanafunzi alikuwa akipima mapigo ya moyo. Kliniki na hospitali sasa zinachukua wanafunzi zaidi kuziba pengo hilo.

Haikuwa hivi kila wakati - vituo vya afya vya umma nchini Zimbabwe viliwahi kuonewa wivu na nchi nyingine za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Lakini zilisambaratika kwa sababu ya miongo kadhaa ya uwekezaji mdogo.

Mnamo 1992, mke wa rais wa zamani Sally Mugabe alichagua kutibiwa kwa kushindwa kwa figo katika hospitali ya umma hadi kifo chake.

Zaidi ya miaka 25 baadaye, ilikuwa hadithi tofauti kwa mumewe: Rais wa zamani Robert Mugabe aliamua kutibiwa katika hospitali ya kibinafsi huko Singapore, ambapo alikufa baadaye, mbali na mfumo wa afya wa umma ulioporomoka wa nchi yake.

line

Hali ikoje kwa wauguzi wanaokaa Uingereza?

Nilizungumza na nesi mmoja ambaye amekuwa huko tangu Julai mwaka jana.

Ananiambia kwa hisia ya kufanikiwa kwamba sasa anapata takriban mara 10 ya aliyokuwa akipata Harare, ingawa wauguzi wa Uingereza wana malipo ya chini ikilinganishwa na taaluma nyingine nchini Uingereza.

Pesa anazotuma nyumbani huenda zikawa nyingi. Anaweza kumudu kupeleka watoto wake katika shule za bweni nchini Zimbabwe na kusaidia jamaa waliokwama.

Hana mpango wa kurudi hivi karibuni.