China: Kwanini baadhi ya Wachina hawavutiwi na 'macho madogo'

"Je sistahili kuwa Mchina kwa sababu tu nina macho madogo?"

Hivi ndivyo mwanamitindo wa China Cai Niangniang aliandika katika chapisho la hivi karibuni la mtandao wa kijamii, baada ya picha zake za zamani kusambaa kwa sababu zisizo sahihi.

Kwa siku kadhaa alikuwa ameshambuliwa mtandaoni kwa kuwakera watu kwa "kutoonesha uzalendo", kutokana na mfululizo wa matangazo ambayo alikuwa amefanya ya bidhaa za vitafunio vya Kichina ya Three Squirrels.

Kosa lake kubwa likiwa ni kuwa macho membamba.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walikasirishwa sana na kufanya kampuni hiyo kuondoa matangazo hayo mtandaoni, na kuomba radhi kwa kuwafanya watu "kukereka".

Lakini Bi Cai alisema kuwa hakujua amefanya nini mpaka kushambuliwa mtandaoni, akisema kuwa "nafanya kazi yangu tu" kama mwanamitindo.

"Mwonekano wangu nilipewa na wazazi wangu," kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 aliandika kwenye jukwaa kama Twitter la Weibo.

"Nimeitukana China siku niliyozaliwa kwa sababu tu ya muonekano wangu?"

'Mataifa ya magharibi hayana maamuzi dhidi ya uwasilishi wao'

Matangazo hayo, ambayo yalitolewa mwaka 2019, yalichimbuliwa na watumiaji wa mtandao wanaopenda uzalendo wakati wa kipindi cha usikivu mkubwa mtandaoni nchini China kuhusu matangazo yanayoonesha watu wa China.

Mnamo Novemba, mpiga picha maarufu wa mitindo wa China aliomba msamaha kwa "ujinga" wake baada ya picha aliyopiga kwa chapa ya kifahari ya Ufaransa ya Dior kuzua chuki. Ilikuwa imeonyesha Mwanamitindo wa China mwenye macho madogo.

Katika siku za hivi karibuni , kumekuwa na visa vingine vya hasira kwenye mitandao ya kijamii kutokana na matangazo ya Mercedes-Benz na Gucci ambayo yaliwahusisha wanawake wa China wenye macho madogo.

Huku kukiwa na ongezeko la hisia za utaifa mtandaoni na chuki dhidi ya mataifa ya Magharibi nchini China, baadhi wamechukua matangazo haya kama mifano ya ubaguzi dhidi ya Wachina.

Kwa kuangazia wanamitindo wenye macho madogo, wakosoaji wanasema makampuni haya yanaendeleza mila potofu za Magharibi kuhusu sura za Wachina.

Wengi waliuliza kwa nini matangazo haya hayakuwa na aina ya wanamitindo wanaoonekana zaidi katika matangazo ya Kichina ambao wana ngozi nyeupe na macho makubwa ya mviringo, ambayo kwa kawaida huchukuliwa kuwa sifa bora za urembo nchini China.

Taarifa za hivi karibuni kutoka chombo cha habari cha serikali China Daily iliangazia jinsi "kwa muda mrefu sana, vigezo vya urembo vya Magharibi, na ladha za Magharibi na zinazopendwa na zisizopendwa zilivyotawala urembo". Hiyo ni pamoja na kuwaonesha wanawake wa bara la Asia kwenye matangazo kuwa na macho membamba, ilisema.

"Magharibi hayana tena usemi kamili juu ya kila kitu," maoni yalisomwa.

"Wachina hawana haja ya kufuata viwango vyao kuhusu urembo na ni aina gani ya wanawake wanaochukuliwa kuwa warembo."

Kama chapa ya Kichina, Squirrels watatu "walipaswa kujua juu ya usikivu wa watumiaji wa Kichina jinsi wanavyoonyeshwa kwenye matangazo," iliongeza.

Chanzo cha mzozo huo ni dhana kwamba taswira kama hizo huibua itikadi kali ya "macho yaliyowatambulisha watu wa Asia ambayo yaliibuka katika utamaduni wa Magharibi katika karne ya 19, na ambayo inachukuliwa kuwa ya kuudhi sana na raia wengi wa bara la Asia kwa leo hii.

Huko Hollywood, mwanaharakati wa Kiasia Fu Manchu alipigwa picha akiwa na macho membamba. Mhusika huyo alijumuishwa na kuendeleza wazo la ubaguzi ambalo tamaduni za Asia zilitishia jamii ya Magharibi.

"Kwa hakika kuna historia ndefu katika matumizi ya 'macho yaliyoinama' kuwabagua Waasia," Dk Liu Wen kutoka Academia Sinica ya Taiwan aliiambia BBC China.

Kukataliwa kwa uzuri huo kwa wingi

Lakini msisitizo miongoni mwa baadhi ya Wachina kuhusu urembo fulani pia unasimama kinyume kabisa na mjadala wa sasa wa kimataifa kuhusu utofauti na msukumo wa uwakilishi mpana wa nyuso za Waasia kwenye vyombo vya habari.

Waangalizi wa mambo wanasema kwamba ingawa inaeleweka kwamba baadhi ya watumiaji wangechukizwa na matangazo, kilio hicho pia ni rahisi sana kwani kinakataa wazo kwamba kunaweza kuwa na njia nyingi tofauti za kuwasilisha muonekano wa Wachina.

"Kukataa 'macho yaliyoinama' ni jambo la hatari sana, kwa sababu ni kukataliwa kwa wingi wa uzuri," Dk Luwei Rose Luqiu kutoka Chuo Kikuu cha Baptist cha Hong Kong alisema.

"Inakandamiza urembo ambao haufikii kiwango fulani."

Wataalam pia wameelezea kuwa viwango vya jadi vya urembo nchini China vilipendelea macho membamba.

Kwa mfano, picha za kuchora kutoka kwa kile kinachozingatiwa sana kuwa zama za dhahabu za China kwa sanaa na utamaduni, kipindi cha nasaba ya Tang kutoka 618 hadi 907 BK, zilionesha wazi wanawake wenye macho marefu na membamba.

"Licha ya tofauti kadhaa katika nasaba tofauti, macho membamba zaidi yalipendelewa katika miaka ya zamani nchini China," Dk Jaehee Jung, mtaalam wa tabia ya watumiaji katika Chuo Kikuu cha Delaware alisema.

Upendeleo wa sasa wa macho makubwa, ni jambo la kushangaza, inaweza kuwa jambo la hivi karibuni limetokea katika tamaduni za Magharibi.

Wataalamu wengine wanaamini mabadiliko ya hivi punde zaidi katika viwango vya urembo yalianza mwishoni mwa miaka ya 1970, kutokana na kufichuliwa kwa matangazo ya kigeni na burudani wakati China ilipofungua milango yake kwa ulimwengu.

"Wanawake katika China ya sasa wanaonekana kuunga mkono viwango vingi vya Magharibi vya maadili ya urembo wa kike yaliyoenea katika picha za vyombo vya habari," Dk Jung alisema.

Siku hizi, macho makubwa ya duara yanathaminiwa sana hivi kwamba ni kawaida kwa wanawake wachanga wa China kujipodoa au hata kufanyiwa upasuaji wa urembo ili kufanya macho yao yaonekane makubwa zaidi, kama vile kutengeneza kope.

Lakini kwa Bi Cai, mwanamitindo katikati mwa mabishano ya hivi punde, anatumai kuwa watu wanaweza kuwa "wakarimu" kwa wale wanaoonekana tofauti. Alisema katika chapisho lake la Weibo kwamba hakuna haja ya kumshambulia hata kama hawakuthamini sura yake.

Kusimama mbele ya simu mahiri na kuuza imekuwa chaguo kubwa la kazi kwa vijana wa China.