Kwanini makombora ya 'hypersonic' ni hatari?

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwezi uliopita, kitu kama roketi kilionekana kikiruka kwa kasi ya juu sana katika anga ya China.

Baada ya kuzunguka karibu dunia nzima, inasemekana ilianguka takriban kilomita 40 kabla ya shabaha yake.

Kwa mujibu wa wataalamu, ilikuwa aina mpya ya kombora la hypersonic, ingawa China imekanusha.

Lakini pia ni kweli kwamba makombora yanayoenda kwa kasi mara nyingi kuliko sauti zake yamekuwa sababu ya ushindani wa silaha kati ya Marekani, China na Urusi.

Kwa hivyo wiki hii ulimwenguni, acha tuchunguze makombora ya hypersonic yakoje na kwa nini yanaweza kuwa jambo la muhimu kuzingatia kwetu?

Sayansi ya roketi

Wanasema kuwa historia ya vita ni ya zamani kama vile kushambulia kwa kurusha vitu hewani.

Katika zama za awali, kulikuwa na silaha kama kombora kubwa na mizinga ya kurusha mawe au mipira ya chuma.

Utambuzi wa kuweza kurusha vitu mbali kwa nguvu zaidi kwa kufunga injini ulizaa teknolojia ya makombora.

Mbinu hii iliboreshwa zaidi na Ujerumani katika miaka ya 1930. Ujerumani walitaka kutengeneza silaha mpya.

HULTON ARCHIVE

Chanzo cha picha, HULTON ARCHIVE

Kwa hili walikusanya maelfu ya wanasayansi na vikwazo vingi vya uhandisi vinavyohusishwa na teknolojia hii viliondolewa."

Mwishoni mwa Vita ya kwanza ya dunia, Mkataba wa Warsay ulianzisha Jeshi la Anga nchini Ujerumani na teknolojia ya kijeshi ilipigwa marufuku.

Lakini hakuna kilichosemwa kuhusu teknolojia ya roketi kwa sababu teknolojia hii haikutengenezwa wakati huo.

Ujerumani ilianza kazi juu yake na kutengeneza silaha mpya hadi mwisho wa Vita ya pili ya dunia .

"Ujerumani ilifanya programu mbili tofauti za utafiti, V-1 na V-2, ambapo makombora ya masafa mafupi na masafa marefu yalitengenezwa.

m

Zote zilikuwa silaha aina tofauti kabisa ," anasema GresselHizi ziliitwa Silaha za Kisasi.

Kulikuwa na mabomu au, sema, mabomu ya kuruka ambayo yanaweza kutupwa mbali kwa msaada wa injini za ndege za V-1.

Wanaweza kuitwa waasisi wa makombora ya cruise. Kasi ile ile ya sauti ilikuwa kombora la masafa marefu la V-2.Walakini, zote mbili zilikuwa na dosari pia. V-1 ingeshika moto haraka na kupoteza njia yake, na Hitler hakuweza kuitumia dhidi ya Marekani kwa sababu ya dosari katika V-2.Gressel anasema, "Ilikuwa na dosari katika teknolojia yake ya kuongoza, ikiwa safu hiyo ingeongezeka, teknolojia isingeweza kuunga mkono na kungekuwa na hatari ya kukosa shabaha. Kwa shambulio la New York, kombora lilipaswa kuongezwa ukubwa.

Jambo ambalo halikutimiza matarajio ya jeshi la Ujerumani kuhusu utengenezaji huo.Wakati wa vita, Ujerumani ilizindua mashambulio ya makombora huko London, Antwerp na Paris, lakini hii haikubadilisha mkondo wa vita.

Baadaye, wanasayansi wanaofanya kazi katika miradi hii walikwenda Marekani na Umoja wa Kisovieti kufanya kazi ya utafiti wa silaha na misheni ya anga.

Nchi zote mbili zilifanya kazi kuboresha teknolojia ya makombora ili kuongeza nguvu ya jeshi lao.

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Makombora ya hypersonic

Silaha hizi mbili za Ujerumani ni makombora ya madafa marefu ya leo.

Makombora ya cruise yanaruka karibu na uso wa dunia na hupiga umbali mfupi, wakati makombora ya balistiki huenda nje ya anga na yanaweza kulenga shabaha umbali wa maelfu ya kilomita.

Dk. Laura Grego ni Mtafiti katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts.

Anasema kwamba ni muhimu kwa kombora kudhibiti harakati zake angani ili kugonga shabaha kwa usahihi na kujificha kutoka kwa adui.

Makombora ya kisasa ya hypersonic yana uwezo wa kufanya hivi.

"Linaweza kubadilisha mkondo wake ,Umbo lake limeundwa maalum ili liweze kugeuka juu na chini au kulia na kushoto huku likisafiri kwa kasi sana katika anga," anasema.

Uwezo huu humsaidia kushambulia kwa kujificha kutoka kwa macho ya adui. Ingawa Laura anasema kuwa kufuatilia kombora sio ngumu.

m

Chanzo cha picha, Reuters

Ufaransa, India, Japan, China na Australia zinafanyia kazi teknolojia ya hypersonic.

Lakini Marekani, Urusi na China wana teknolojia ya kisasa zaidi katika suala hili.

Dk. Marina Favaro ni Mtafiti katika Taasisi ya Utafiti wa Amani na Sera ya Usalama, Chuo Kikuu cha Hamburg.

Anasema kuwa mataifa makubwa duniani yanashindana kukaa mbele ya kila mmoja katika masuala ya teknolojia ya kijeshi.

Anasema, "Kwa ujumla inaaminika kwamba kadiri kombora linavyoenda kasi ndivyo inavyokuwa bora zaidi.

Silaha pia inakuwa suala la heshima ya nchi. Sio kwamba nchi hizi zinatengeneza silaha bora kwa sababu zinataka kuzitumia."

Badala yake, wanataka kusema kwamba wanaweza kutengeneza silaha za kisasa.

Hii inamaanisha kuwa uzinduzi wa hivi majuzi wa china ni jaribio la kuonesha kuwa iko sawa na Marekani katika suala la teknolojia.

Dk Marina anasema, " Marekani imekuwa ikisema kwamba inafanya kazi kwa teknolojia ya hypersonic ili kupunguza vitisho vinavyoweza kutokea katika siku zijazo na kukabiliana na mashambulizi ikiwa inahitajika. Viongozi wengi wana hakika kwamba Urusi na China zinatengeneza silaha hizo, kwa hiyo Marekani inahitaji kufanya vivyo hivyo."

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Ikiwa inaonekana, mbio za silaha ni kwamba, teknolojia iliyoundwa na moja, nyingine inajaribu kufanya sawa au bora zaidi.

Diplomasia, Mvutano na Silaha

Wakati wa Vita Baridi, mikataba kadhaa ilitiwa saini kati ya Marekani na Umoja wa Kisovieti ili kupunguza hatari ya mashambulizi ya nyuklia.

Mikataba hii mingi imeisha muda wake na makubaliano ya mwisho yanastahili kuisha mnamo 2026.

Lakini Marekani haina makubaliano hayo na China.

Dk. Cameron Tracy ni msomi wa utafiti katika Kituo cha Usalama wa Kimataifa na Ushirikiano cha Chuo Kikuu cha Stanford, anasema kwamba makombora ya hypersonic huongeza mvutano kati ya nchi.

Anasema, "Tuna ukweli wa wazi unaoashiria kuwa nchi zinahusika katika mbio za silaha na mvutano kati yao unaweza kuongezeka katika siku zijazo."

Kwa sasa, badala ya kuzisukuma Marekani na China kwenye vita, teknolojia mpya ya makombora inazidisha mvutano kati yao. Lakini hali hii inaweza kubadilika.