Jaribio la China la kombora la hypersonic linaashiria mashindano ya utengenezaji silaha?

Chanzo cha picha, Getty Images
Habari kuwa China ilifanyia majaribio kombora jipya la uwezo wa juu la hypersonic zilitajwa na baadhi kuwa hatua kubwa iliyowashangaza maafisa nchini Marekani. Kwa hivyo suala hili ni kubwa kiwango gani, anauliza Jonathan Marcus kutoka taasisi ya masuala ya ulinzi chuo cha Exeter.
Mara mbili wakati wa msimu wa joto jeshi la china lilirusha roketi kwenda anga za mbali iliyozunguka dunia na kisha kufululiza kwenda kwa lengo lake.
Mara ya kwanza ilikosa lengo lake kwa karibu kilomita 40 kwa mujibu wa wale waliojulishwa waliozungumza na gazeti la Financial Times, gazeti lililokuwa la kwanza kuandika habari hizo.
Wakati baadhi ya wanasiasa nchini Marekani wazifahamu hatua hizo za China, China ilikanusha kwa haraka ripoti hiyo ikisisitiza kuwa hilo lilikuwa jaribo la chombo cha anga za mbali.
Kukana kwa Uchina sio jambo zuri, anasema Jeffrey Lewsi mkurugenzi wa East Asia Non-Proliferation Program taasisi ya Middlebury Institute of International Studies huko Monterey, California, kwa sababu habari hiyo imethibitishwa na maafisa nchini Marekani.

Zana za ICBM na FOB ni gani?
• ICBM ni kombora la masafa marefu linalovuka anga ya dunia kabla ya kurudi na kufululiza kwenda kwa lengo
• FOB au Fractional Orbital Bombardment ni mfumo unaotuma kombora kuzunguka mzingo wa dunia, ambalo hushambulia lengo lake kutoka upande usiotarajiwa.
Mifumo ya FOB sio mipya
Ulitumiwa na muungano wa usovieti wakati wa vita baridi na sasa hivi unafufuliwa na China. Suala hapa ni silaha ambayo inaizunguka dunia na kushambulia sehemu inazolenga kutoka pande zisizotarajiwa,
Kile china imeonekana kufanya ni kujumuisha teknolojia ya FBO na ile ya Hypesonic glider - ambapo kombora linaingia anga za mbali ili kukwepa kutambuliwa na mitambo ya rada na mifumo ya ulinzi wa makombora. Lakini ni kwa nini?
"China ina hofu kuwa Marekani itatumia mifumo iliyoboreshwa ya nyuklia na mifumo ya ulinzi wa makombora kuzima uwezo wake wa nyuklia," anasema Bw Lewis.
Iwapo Marekani itaishambulia China kwanza, mifumo ya ulinzi wa makombora huko Alaska inaweza kukabiliana na idadi ndogo ya zana za nyuklia za China ambazo zitakuwa zimebaki.

Chanzo cha picha, TASS
Nchi zote zenye nguvu ya nyuklia zinaunda mifumo ya hypersonic lakini zinaitazama kwa njia tofauti, anasema Aaron Stein. Na mitazamo hii tofauti anasema, inaweza kuchochochea mashindano ya silaha.
China na Urusi zinaiona teknolojia ya hypersonic kama njia ya kuhakikisha kuwa mifumo ya ulinzi wa makombora imeshindwa.
Kwingineko Marekani inapanga kuzitumia kushambulia maeneo yanayotajwa kuwa magumu kama yale yanayotumiwa kuongoza mifumo ya zana za nyuklia kwa kutumia zana zisizo za nyuklia.
Lakini baadhi ya wataalamu hawamini kuwa jaribio hili la China linazua tisho jipya. James Acton wa shrika la Carnegie Endowment for International Peace anasema Marekani imekuwa kwenye hatari ya shambulizi la nyuklia kutoka China tangu miaka ya 1980.
Lakini anaamini kuwa pragramu za China, Urusi na Korea Kaskazini kushinda mifumo ya ulinzi wa makombora ya Marekani zinaweza kusababisha Marekani kutathmini iwapo mikataba ya kuweka viwango kwa mifumo ya ulinzi ina manufaa kwake.
Bw Lewis sasa anesema kuwa suala kuu sasa ni Marekani kufanya maamuzi bora.
Mahasimu wa Marekani wote wanaboresha zana zao za nyuklia.
Zana za China sio nyingi ikilinganishwa na nchi kama Marekani. Lakini kuna wasi wasi kuwa mifumo ya ulinzi wa makombora na ya zana zingine za masafa marefu inashinikiza kuundwa zana zilizoboreshwa za nyuklia.
Korea Kaskazini nayo inaboresha uwezo wake wa nyuklia kwa lengo la kuwa na usemi wa kidiplomasia siku zinazokuja, kwa mujibu wa Ankit Panda kutoka Carnegie Endowment.
Anasema kwa miaka michache, wametaka kutendewa na Marekani kama walio sawa na wanaona kuwa kuunda zana bora za nyuklia na makombora kama njia ya kupata heshima.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni masuala ambayo yanazua changamotoa za nyuklia kwa uongozi wa Biden.
Kuvunjika kwa mikataba ya kuzuia zana kutoka kipindi cha vita baridi haisaidii. Wala misukosuko inayozidi kukua kati ya Urusi na pia China.
Kulingana na Ankit Panda kile ambacho Marekani inaweza kafanya kupunguza kasi ya mshindano ya silaha ni kujadili viwango vya mifumo ya ulinzi jinsi ilifanya wakati wa vita baridi.
Kuweka suala la mifumo ya ulinzi wa makombora mezani, yaweza kuruhusu Marekani kufikia muafaka na Urusi na pia China.
Pia inazuia kila mmoja wao kutafuta njia ghali na hatari za kusafirisha zana za nyuklia.













