Je kombora la Hypersonic lililofanyiwa majaribio na China ni kombora la aina gani?

Gettyimages

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, China ilifanya jaribio la kombora la hali ya juu la hypersonic miezi miwili iliyopita (mwezi Agosti). Hatua hii iliishangaza idara ya ujasusi nchini Marekani.

China ilidaiwa kufanya jaribio la kombora la hali ya juu la hypersonic hivi majuzi, hatua iliowashangaza idara ya ujasusi nchini Marekani.

Gazeti la Financial Times liliripoti kuhusu jaribio hili la kombora la hypersonic kwenye ripoti yake ya hivi punde. Gazeti hili lilisema liliandika kufuatia habari lililopata kutoka vyanzo vitano ambavyo halikuvitaja.

Hata hivyo China imekana rasmi madai hayo. Kisha wakasema kuwa walichofanyia majaribio halikuwa kombora la hypersonic bali chombo cha angani.

Licha ya China kukataa hilo, habari hizo zinaendelea kuzua mjadala kote duniani.

Marekani , Urusi na China wote wamejaribu kuunda makombora ya hypersonic.

Hii inahusu kuunda chombo kinachoelekezwa. Chambo hiki kinarushwa angani kwa kutumia roketi. Kisha kinaizunguka dunia na baadaye kufululiza kwenda kwa lengo lake.

Prof Taylor Favel, mtaalamu wa sera za nyuklia za China aliliambia gazeti la Financial Times kuwa chombo hiki cha hypersonic ambacho kinaweza kubeba silaha za nyuklia kitaisadia China kuzuia kujikuta imefungwa kwenye mifumo ya makombora ya ulinzi ya Marekani.

BBC imezungumza na baadhi ya wataalamu katika nyanja ya zana za nyuklia na ulinzi kuhusu teknolojia hii.

Rais wa China Xi Jinping

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais wa China Xi Jinping

Maana ya Kombora la hypesonic ni nini?

Kombora la hypersonic ni kombora ambalo husafiri kwenda eneo linalolenga kushambulia kwa kasi kubwa ya mara tano kuliko kasi ya sauti.

Kombora la hypersonic, limekuwa ni teknolojia ya kiwango cha juu zaidi ya makombora kwa kipindi cha miaka 30 hadi 35. Kwanza linarusha chombo kwenda angani. Baada ya hapo linashika kasi ambayo inakuwa vigumu kulifuatilia na kuliharibu.

Baada ya kombora hili kurushwa njia yake inaweza kubadilishwa. Kombora hili huzunguka kwa kasi ya juu angani.

Kwa njia nyingine wakati nchi inarusha kombora la hypersonic inakuwa vigumu kulizuia kwa kutumia mifumo ya ulinzi ya makombora.

Changamoto kwa Marekani

Magazeti yaliandika kuwa habari kuhusu kombora la hypersonic ziliipata ghafla idara ya ujasusi nchini Marekani.

Lakini China yenyewe imekana habari kama hizo. Lakini ripoti kutoka kwa watu ni kwamba hilo ndilo lilinafanyika.

Marekani haukutarajia kuwa China inaweza kuboresha teknolojia yake hadi kufikia kiwango kama hicho kwa kuwa China ambayo imekuwa ikinakili teknolojia kwa kati ya miaka 25 hadi 30 huunda kila kila kitu kuanzia mifumo yake ya makombora hadi vifaa vinavyotumiwa na jeshi.

Kwa hivyo itakuwa ni jambo la kusangaza kwa Marekani, alisema Rahul Badi.

Kombora la Hypersonic

Chanzo cha picha, 3DSCULPTOR

Gazeti la Financial Times linasema kuwa jaribio hilo lilikuwa lenye mafanikio kulingana na taarifa lililopata.

Hata hivyo lilisema kuwa kombora hilo la China liligonga kombora la kwanza kwa umbali wa karibu kilomita 32.

Uwezo wa China uliongezeka kwa jaribio hilo. Nafasi ya Marekani kama nchi namba moja umepingwa.

Hata hivyo PR Shankar, mkurugenzi wa zamani katika jeshi la India, alisema habari hizi hazikuhitaji kupewa umuhimu sasa.

"Nchi yoyote iliyo na pragramu ya anga za mbali itakuwa na teknolojia ya hypesonic, lakini kuigeuza kuwa silaha inahitaji mifumo ya ardhini na pia mifumo ya setilaiti na makombora. China bado inasafari ndeefu," alisema.

Kombora la Hypersonic

Chanzo cha picha, NOEL CELIS

Je dunia ipo hatarini?

Hali kama hii ilishuhudiwa miaka 60 iliyopita. Wakati huo nao serikali ya Marekani ilipingwa.

Inafahamika kama Cuban Missile Crisis. Wakati huo vita vya nyuklia vilikuwa vinatokota kati ya Marekani na Muungano wa Usovieti.

Baadaye juhudu zilifanywa kumaliza misukosuko kati ya nchi hizo. Makubaliano kadha yakaafikiwa kusitisha vita vya nyuklia.

Baada ya Cuban Missile Crisis, dunia iliewa kuwa ikiwa nchi moja itarusha kombora la nyuklia, nchi nyingine itafanya hivyo na nchi zote zitaharibiwa. Ndio maana makubaliano mengi yameafikiwa kuzuia vita vya nyuklia.

Hata hivyo Marekani ilianza kuunda mifumo ya makombora ya ulinzi hatua iliyoenda kinyume na mkataba wa ABM wa mwaka 2001. Ilitetea hatua hiyo yake ikisema kuwaa inajenga mfumo wa ulinzi kujilinda dhidi ya nchi ndogo kama Korea Kaskazini.

Lakini China na Urusi wanahofu kuwa iwapo Marekani inajenga mifumo ya ulinzi, makombora yetu hayatafanya hivyo. Kwa hilo nchi zote zikaanza kuunda makombora ya hypersonic.

Kombora la Hypersonic lenye kichwa cha Kinyuklia

Chanzo cha picha, TASS / GETTYIMAGES

Maelezo ya picha, Kombora la Hypersonic lenye kichwa cha Kinyuklia

Zinadai kuwa Marekani inaweza kujilinda kwa kutumia mifumo yake ya makombora ya ulinzi kwa hivyo zinajenga makambora yanayoweza kushambulia bila kuzuiwa.