Uchina imekanusha kufanya jaribio la kombora hatari la nyuklia la haypersonic

Image shows DF-17 medium-range ballistic missiles equipped with a DF-ZF hypersonic glide vehicle, involved in a military parade to mark the 70th anniversary of the Chinese People's Republic

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, China ilionyesha makombora ya hypersonic katika gwaride lake la kijeshi hivi karibuni

China imekanusha ripoti kwamba ilifanya jaribio la silaha ya nyuklia ya lombora la masafa la hypersonic mapema mwaka huu, ikisisitiza kuwa ulikuwa ni ukaguzi wa kawaida wa chombo cha anga.

Ripoti ya awali katika gazeti la Financial Times iliibua wasi wasi mjini Washington, ambako Idara ya ujasusi ya Marekani iliripotiwa kutofahamu taarifa hiyo.

Makombora ya Hypersonic yana kasi zaidi na yanasafiri kwa urahisi zaidi kuliko ya kawaida, ikimaanisha kuwa ni magumu sana kuweza kuyazuwia yanapofyatuliwa.

Hii inakuja huku hali ya wasi wasi ikiendela kuongezeka kuhusu uwezo wa nyuklia wa Uchina.

Jumatatu, msemaji wa wizara ya mambo ya nje Zhao Lijian aliwaambia waandishi wa habari kwamba majaribio yalifanyika Julai kuthibitisha aina ya teknolojia mbali mbali ya chombo cha anga.

"Hili halikuwa kombora, hiki kilikuwa ni chombo cha anga za mbali ," alisema. "Hili lilikuwa ni la umuhimu mkubwa kwa ajili ya kupunguza gharama ya matumizi ya chombo cha anga za mbali ."

Bw Zhao aliongeza kuwa nchi nyingi zilifanya majaribio sawa na hayo katika nyakati zilizopita. Wakati alipoulizwa iwapo taarifa ya Financial Times haikuwa sahihi, alijibu "ndio".

Taarifa hiyo ya Jumamosi ilinukuu vyanzo vya habari ambavyo havikutajwa majina vilivyosema makombora hayo yalifyatuliwa katika majira ya kiangazi. Lilipaa kwenye eneo la anga la obiti kabla ya kushuka chini na lilikosea kidogo eneo lililolengwa, ilisema taarifa hiyo.

"Jaribio hilo lilionyesha kwamba Uchina ilikuwa imepiga hatua kubwa katika utengenezaji wa silaha za hypersonic na iko mbele zaidi kuliko maafisa wa Marekani walivyoelewa ," ilieleza ripoti hiyo.

Unaweza pia kusoma:

Mjumbe wa ngazi ya juu wa Baraza la Congress baadaye alisema kuwa jaribio hilo linapaswa kuchukuliwa kama sababu ya kuchukuliwa hatua kwa Marekani.

Mike Gallagher, mbunge wa Republican katika kamati ya huduma za silaha ya bunge, alisema iwapo Washington imekwama kwenye msimamo wake wa sasa itashindwa katika vita vipya baridi na Uchina katika kipindi cha muongo.

Mahusiano baina ya Marekani na Uchina yamekuwa ya wasi wasi, huku Beijing ikiushutumu utawala wa Rais Joe Biden kwa kuwa adui.

Nchi kadhaa za Magharibi pia zimeelezea hofu yao kuhusiana na hatua ya hivi karibuni ya Uchina ya kunadi uwezo wake wa kijeshi.

Wanajeshi

Chanzo cha picha, Rheuters

Michael Shoebridge, Mkurugenzi wa usalama, mkakati na usalama wa taifa katika taasisi ya Australia ya mkakati wa sera, alisema kama kombora la hypersonic lilifanyiwa majaribio litakuwa limetimiza kigezo cha kuwekwa katika "sehemu ya kuongezeka katika nyuklia na silaha nyingine za mashambulio ya hali ya juu ".

China ilionyesha kile kilichoonekana kama jukwaa la kombora la masafa ya kasi kubwa (panasonic missile) katika maonyesho ya hivi karibuni ya kijeshi.

Sambamba na Uchina, Marekani, Urusi na takriban nchi nyingine tano zinashugulikia teknolojia ya makombora hayo ya Hypersonic.

Yanaweza kupaa kwa uwezo wa zaidi ya mara tano wa kasi ya sauti , sawa na makombora ya ballistc, yanaweza kufikisha kwenye eneo lililolengwa vilipuzi vya nyuklia.

Mwezi uliopita, Korea Kaskazini, ilisema kuwa ilifanikiwa kufanya jaribio la kombora jipya la hypersonic. Na Julai, Urusi ilitoa tangazo kama hilo na ikasema kombora lake lilifyatuliwa kutoka eneo la bahari nyeup.