Ufisadi Afrika Kusini:' Sijihisi kuwa salama na maisha yangu'

Mauaji ya hivi karibuni ya mtumishi wa umma wa Afrika Kusini bwana Babita Deokaran, ambaye alitoa taarifa juu ya ufisadi wa seriakali, yameweza kuonesha hatari ya ambayo inaweza kuwakuta kwa wale ambao wanaweza kuongea kuhusu kuongezeka kwa hilo tatizo, Mwandishi wa BBC, Pumza Fihlani ameandika.
"Inakuaje kama bosi wako akiwa mla rushwa na ... rais pia anahusishwa?"
Swali la Mosilo Mothepu linabakia kuwa kutaka majibu kuhusu maadili, uraia mwema na usalama wa mtu.
Miaka sita iliyopita, alikabiliwa na changamoto ya nini cha kufanya na kuamua kusema kuhusu rushwa.
Kila kitu kilibadilika.
"Sijihisi kuwa na amani ,sifuati utaratibu, mara zote ninahisi kama kuna mtu ananifuata hivyo sina amani. Ni ngumi sana, imeniwia vigumu sana sana," alisema.
Hana ajira kwa miaka miwili
Maamuzi yake kuhusu hilo ana imani kwamba alifanya jambo sahihi, lakini imekuja kwa gharama.
"Kwa ueleo wangu mdogo kuhusu ripoti itakayokuja na watu ambao walikamatwa na kufungwa gerezani ndani ya miezi kadhaa , nikipata kazi maisha yataendelea kama kawaida.
"Ingawa,nilikuwa sina ajira kwa kipindi cha miaka miwili," anasema anapambana na machozi.
Mwaka 2015, bi Mothepu alikuwa mkurugenzi mkuu wa uwekezaji katika kiwanda cha Trillian. Kilikuwa kinahusisha na familia ya Gupta ambayo imekuwa ikishutumiwa kuhusu kashfa kubwa ya rushwa inayofahamika kama kuliibia taifa. Walikanusha madai dhidi yao.
Bi Mothepu ameanza kuona namna kiwanda ambacho kinashutumiwa fedha zilizoibiwa kutoka makampuni ya serikali, kwa kutumia bili za uongo.
Aliwauliza maswali mabosi wake na kuambiwa kama atakuwa mwaminifu basi ataangaliwa vizuri.
Lakini imani yake ya kikristo pamoja na utu wake ulimfanya aweke wazi jambo hili.
Aliacha kazi na kutoa ushahidi kwa walinzi wa umma, idara inayohusika na kupambana dhidi ya rushwa.
Ni kwa sababu ya yeye kutoboa siri kashfa nyingi za rushwa nchini humo ziliweza kuibuliwa.
Licha ya kupewa ulinzi , bi Mothepu bado anahofia usalama wake.
Rushwa ya Corona
Mwezi uliopita, Babita Deokaran, afisa wa ngazi ya juu katika kitengo cha fedha, idara ya afya ya jimbo la Gauteng , amekutwa amekufa nje ya nyumba yake baada ya kupigwa risasi mara kadhaa.
Watu sita wanashtakiwa dhidi ya mauaji yake.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuna tuhuma kuwa ameuawa kwasababu alikuwa awe shahidi wa uchunguzi unaoendelea kuhusu mikataba ya ulaghai yenye thamani ya dola milioni 23, iliyotolewa na idara yake ili kununua vifaa kinga vitakavyosaidia kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona.
Wakati akieleza juu ya kile ambacho kingeweza kuchochea kuuawa kwake licha ya kuwa sababu ya kuuliwa haijulikani bado, Rais Cyril Ramaphosa alimuelezea marehemu kuwa shujaa na mzalendo na kusema kuuliwa kwake kuna kutukumbusha kuwa kuna matukio mengi zaidi ya rushwa ambayo jamii inapaswa kukabiliana nayo na kuyatokomeza.
Familia yake iliongea na BBC kuwa sasa wanahofia maisha yao na hawajui wamuamini nani.
Kifo cha Deokaran kimeibua maswali mengi kuhusu ulinzi mbaya unaotolewa kwa wale ambao wanakuwa tayari kueleza ukweli.
Na kuna mengi zaidi.
Zaidi ya dola billioni 106 zilipotea katika ufisadi uliobainika kati ya mwaka 2014 na 2019, kwa mujibu wa utafiti wa chuo kikuu cha Stellenbosch.
Ufadhili wa zaidi ya miezi 18 iliyopita uliolenga kupambana na maambukizi ya virusi vya corona zimeporwa, wezi ambao bi Deokaran aliwazungumzia.
Hili haliwezi kupotea miongoni mwa wapiga kura na kwa miaka mingi kumekuwa na maandamano ,kwa namna moja yalkuwa yakilengwa dhidi ya Jacob Zuma wakati alipokuwa rais.

Chanzo cha picha, AFP
Alishutumiwa kwa kushindwa kukabiliana na ufisadi wa familia ya Gupta wakati wa utawala wake kati ya mwaka 2009 na 2018.
Walimshutumu kwa kuhusika katika kufanya maamuzi ya kutolewa fedha kwa ajili ya maslahi yao binafsi .
Bwana Zuma amekanusha pia kuhusika na uchunguzi unaenelea.
Bwana Ramaphosa alichukua madaraka Februari 2018, lakini tuhuma zinazowahusisha wanasiasa na maofisa kupora fedha za umma bado zinaendelea.
Hii ni kwasababu kuna misingi ambayo iliwekwa ,kwa mujibu wa Lawson Naaidoo kutoka taasisi ya Casac, ambayo inafanya kazi ya kupambana na rushwa.
"Hili limekuwa janga sasa," aliiambia BBC.
Na wale wanaojaribu kufanya lolote kuhusiana na hilo wanakuwa wanaweka maisha yao hatarini.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Watoa taarifa za siri hawajawa na maisha mazuri katika taifa hili … Ninajilaumu kuwa katika matukio mengi hatujaweza kuwalinda wao kwanza," alisisitiza rais Ramaphosa wakati akitoa ushahidi juu ya madai ya ufisadi nchini humo.
Bi Mothepu anafahamu kuwa kwa uelewa wake binafsi rais anaongea ukweli.
"Inawezekana nimekuwa shujaa kwa baadhi ,lakini si kwa wafanyakazi.
"Hali yangu ya afya ilidhoofika, nililazwa hospitalini baada ya kupata matatizo ya akili .
Nilikuwa sijajiandaa kwa ajili ya kulipa bili za hospitali ," alisema.
"Vilevile sikujua ni nani wa kumwendea , nani wa kumwamini , hawa walikuwa watu wenye nguvu sana. Sheria haiwezi kukulinda hivyo unabaki unapambana mwenyewe."
Kulikuwa na sheria ya kuwalinda watu kama bi Mothepu kutopoteza ajira zao , ilifahamika kama 'Personal Disclosure Act'. Lakini shida ni kuwa imejikita katika mambo mengi.
Kati ya mwaka 2015 na 2020, zaidi ya watu 850 wanasiasa au wakuu wa ofisi waliuawa , kwa mujibu wa utafiti.
Wengi wao walitoa taarifa kwa siri au walikuwa mashahidi katika madai ya uhalifu yaliyokuwa yanachunguzwa, watafiti walisema.
Kulikuwa na mpango ambao unasaidia kulinda mashahidi mashaidi lakini baada ya miaka kadhaa ya taifa kukithiri katika rushwa, ni watu wachache ndio walikubali kuamini mfumo huo ili kulinda maisha yao.
Hakuna majuto
Mamlaka ya taifa ya mashtaka (NPA) yamekanusha kuwa serikali inashindwa kuwalinda watoa taarifa kwa siri.
"Mpango wa kuwalinda mashahidi umefanikiwa kwa kiasi kikubwa na hakuna haja ya kueleza namna ambavyo wameboresha utendaji woa kwa namna yeyote," aliandika katika barua kwa ajili ya BBC.
Lakini kujiunga na mpango huo ni sawa na kuachana na kila kitu , jambo ambalo linakuwa gumu kwa baadhi kulitelekeza.
Sasa serikali itafanya nini kuhusu watu hao ?
"Hatuwezi kuwalinda… tunawashauri hatua ambazo wanapaswa kuzifanya ili wajilinde wenyewe. NPA inaweza kutoa msaada wa ulinzi katika ukomo fulani tu ," taarifa ilisema.
Ni zaidi ya miaka minne tangu bi. Mothepu alivyoongea kwa mara ya kwanza kuhusu Guptas, ambaye bado hajahojiwa na mamlaka , amehamia Dubai.
Anataka kutengeneza maisha yake upya na ameandika kitabu, Uncaptured, ambacho ana matumaini ya kuwavutia watu wengi kuzungumza dhidi uovu unaotendeka".
"Piga picha taifa hili litakuwa wapi kama kila mtu atafanya lolote , kama kila mtu ataamua kuangalia upande mwingine ? Hatuwezi kuliacha taifa linaharibika.
"Maisha yangu yatakuwa mazuri kwa kuwa nimefanya sehemu yangu na sijutii , hii ni nchi yangu hivyo lina thamani kubwa".













