Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kamera ya mwilini yanasa mauaji ya mtu mweusi mikononi mwa polisi tangu George Floyd
Polisi huko Minneapolis wametoa video inayoonesha mauaji ya mtu mweusi yaliyotekelezwa na polisi, kifo cha kwanza cha aina hiyo tangu kile cha George Floyd, kilichotokea mnamo mwezi Mei.
Mwathirika kijana mweusi, Dolal Idd, 23, alikuwa mshukiwa wa uhalifu na alisimamishwa na maafisa wa polisi Jumatano.
Walioshuhudia mauaji hayo wanasema, bwana Idd ndiye aliyeanza kufyatua risasi kabla ya polisi kujibu.
Mji wa Minneapolis ulishuhudia maandamano yaliyodumu kwa miezi kadhaa baada ya kifo cha Bwana Floyd aliyeuawa mikononi mwa polisi.
Maandamano hayo yalisambaa kote Marekani huku kukiwa na madai ya ukatili unaotekelezwa na polisi.
Bwana Floyd alifariki dunia baada ya afisa wa polisi kupiga goti juu ya shingo yake kwa takriban dakika 9.
Video ya mauaji ya hivi sasa ya ufyatuaji wa risasi unaomhusisha afisa wa polisi ilitolewa Alhamisi.
Video hiyo inaonesha gari la polisi likizuia gari jeupe katia kituo cha kuuza petroli kusini mwa mji huo, ikiwa sio mbali sana na eneo ambapo George Floyd aliuawa.
Maafisa wa polisi wanasikika wakipaza sauti na kusema "Simamisha gari lako, inua mikono yako juu, Inua mikono juu!" kabla ya kuanza kwa ufyatulianaji wa risasi na maafisa wa polisi.
Abiria wa kike aliyekuwa kwenye gari na Bwana Idd amepata majeraha na pia hakuna polisi aliyejeruhiwa.
Mkuu wa polisi wa Minneapolis Medaria Arradondo amesema bunduki ilipatikana kwenye eneo la tukio.
"Nilipotazama video ambayo kila mmoja anaitazama - na uhalisia wa mambo - inaonekana aliyekuwa kwenye gari ndiye aliyeanza kufyatulia polisi risasi," amesema.
Watu ikiwemo baba yake Idd, Bayle Gelle walikusanyika kwenye eneo la tukio siku iliyofuata, na kusababisha hofu ya kuanza tena kwa maandamano.
"Alikuwa tu ameketi ndani ya gari, na akaanza kufyatuliwa risasi bila sababu yoyote, alisema kama alivyonukuliwa na shirika la habari la CBS News.
"Kwanini tumefika hapa?... Kwasababu ya ubaguzi wa rangi. Ni mwanaume mweusi. Tunataka kujua kwanini kijana wangu alipigwa risasi na kuuawa."
Meya wa mji huo Jacob Frey alisema amejitolea kuhakikisha anafahahamu kwa undani kilichotokea na kuwa haki itatende
"Tunajua maisha ya mtu yamekatizwa usiku huu na ule uaminifu kati ya jamii za watu weusi na maafisa wa polisi umezorota," amesema hivyo katika taarifa yake aliyotoa.
"Kujenga tena uaminifu uliokuwepo kutategemea na uwazi tu."
Kifo cha Bwana Floyd mamo mwezi Mei likisababisha kutolewa kwa wito wa mabadiliko au hata kuondolewa kabisa kwa idara ya polisi mjini humo lakini juhudi hizo zimegongwa mwamba.