Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
BBC 100 Women 2020: Nani yuko kwenye orodha hiyo mwaka huu?
Orodha hiyo inajumuisha Bi . Sanna Marin, ambaye anaongoza serikali yenye uongozi wa wanawake pekee nchini Findland ikiwa ni serikali ya muungano.
Michelle Yeoh, ambaye ni nyota wa filamu za New Avatar na ile ya Marvel na sarah Gilbert, ambaye anaongoza utafiti katika chuo kikuu cha Oxford katika maswala yanahusu ugonjwa wa corona, naye bi Jane fonda ni mwanaharakati wa maswala ya hali ya anga na pia ni muigizaji.
Na katika matukio ambayo sio ya kawaida mwaka huu , huku idadi ya wanawake ambayo haiwezi kuhesabika duniani ikijizatiti kuhakikisha kuwa maisha ya jamii zao inasonga mbele licha ya changamoto ambazo zimekuwa mwaka huu jina la mwanamke mmoja halijaandikwa kama nafasi ya kuwakumbuka wanawake wote duniani kwa mengi ambayo wameyaafikia.
Na je wanawake hawa mabingwa waliteuliwa kivipi
Kikosi kilichoongoza mpango huu wa kuwatambua wanawake 100 kwanza iliandaa orodha fupi kulingana na majina yaliyokusanywa nao na kupendekezwa na idara nyengine za BBC kutoka idhaa mbali mbali zinazopeperusha matangazo
Kikosi cha wanawake 100 kilikuwa kinatafuta wagombea ambao walikuwa wameingia kwenye vichwa vya habari au kuwa na ushawishi katika utendakzi wao katika jamii , pia walikuwa wanawake ambao wamefanikiwa ufanya mambo muhimu ambayo yaliathiri jamii kwa manufaa
majina yalitathminiwa kwa kufuata kaulimbiu ya mwaka huu - wanawake ambao waliongoza mabadiliko -