Katika Picha:Jinsi mifuko ya plastiki inavyotumika katika mitindo

Mpiga picha wa NigeriaObinna Obioma anatumia namna ya kipekee kuwasilisha jinsi mifuko ya plastiki inavyotumika Afrika Magharibi.

Mifuko ambayo ni maarufu katika masoko ya Afrika Magharibi , ya rangi ya bluu na nyekundu ambayo nchini Tanzania ni maarufu kwa jina la 'shanngazi kaja'.

Lakini miaka ya 1980, mamia ya maelfu ambao walikuwa wanatumia mifuko hiyo nchini Nigeria ni wahamiaji wengi waliotokea Ghana.

Kipindi ambacho tangazo la kuondoka nchini humo lilipotoka walikuwa wakibeba mizigo yao kwa haraka kwa kuweka mizigo yao katika mifuko hiyo hivyo mifuko hiyo ikapewa jina 'Waghana lazima waondoke'.

Mifuko hiyo ni gharama nafuu na mikubwa kuhifadhi vitu vingi kwa pamoja.

All images subject to copyright