UAE yaweka sheria kali dhidi ya 'Mauaji ya heshima' dhidi ya wanawake

With Dubai's trademark skyscrapers in the background, Muslim women walk past a minaret

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Serikali ya UAE ilibadilisha mtazamo wake, katika dhamira ya kulinda haki za wanawake

Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imeongeza adhabu kwa wanafamilia wanaofanya mauaji ya wanawake kama sehemu ya kufuata sheria za nchi za kiislamu.

Serikali ya Falme za Kiarabu imesema itazuia majaji kutoa adhabu ndogo kwa watu wanaofanya mauaji ya namna hiyo.

Mara nyingi wanahusisha mauaji ya wanawake baada ya kuona kuwa wanawake hao wanaleta aibu katika familia.

Uhalifu kama huo utachukuliwa kama mauaji kuanzia sasa, serikali ya UAE imesema.

Makundi ya haki za binadamu yamesema kila mwaka maelfu ya wanawake duniani kote wanauawa kutokana na madai ya familia zao kuwa walileta aibu katika familia zao.

Masuala kama ya kufanya ngono nje ya ndoa, hata kama ni madai tu ilikuwa ni miongoni mwa sababu ya mauaji hayo.

Mauaji ya aina hiyo mara nyingine huwa yanaitwa "mauaji ya heshima", lakini maelezo hayo yamekosolewa na wale wanaosema kuwa ni njia isiyofaa kuelezea vifo.

Taifa hilo limeamua kuweka hukumu kali kwa mauaji kama hayo kwenye "dhamira thabiti ya UAE ya kulinda haki za wanawake",

A spectator on a camel watches participants competing during the Aqua Challenge sports event in Gulf emirate of Dubai, United Arab Emirates

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, UAE inataka kuvutia uwekezaji wa utalii

Mabadiliko ya sheria za nchi za ghuba, ilipitishwa na rais sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan siku ya Jumamosi , Wakala wa habari WAM ilisema

Miongoni mwa mageuzi hayo yatawapa wakazi wageni katika nchi hiyo haki ya kuchagua sheria zao wenyewe katika sheria za urithi na wosia.

Wakala wa habari walisema , mpango huu una nia ya kuimarisha wawekezaji wa nje na kuimarisha uchumi.

UAE ilisema uamuzi huo hautawadhuru wegine, WAM ilisema bila kutoa maelezo zaidi.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya UAE kusaini mkataba wa kidiplomasia na Israel.

Mkataba huo ulilenga kukuza utalii UAE, ambao ulikuwa unajenga nguvu za kijeshi pamoja na sehemu za biashara na mapumziko.

2px presentational grey line