Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2020: Dkt.Hussein Mwinyi ala kiapo cha urais Zanzibar

ccm

Chanzo cha picha, Getty Images

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imemuidhinisha rasmi Dkt.Hussein Mwinyi kuwa rais wa Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi.

Dkt. Mwinyi alitangazwa mshindi wa nafasi ya Urais Zanzibar kwa asilimia 76. 27% huku mpinzani wake Maalim Seif akiwa mshindi wa pili kwa asilimia 19.87%.

Sherehe za kumuapisha rais Husein Mwinyi zimeenda kwa amani na utaratibu bila ghasia zozote na huku watu wengi wakiwa wamekusanyika kushuhudia tukio hilo.

Awali jeshi la Polisi mkoa wa mjini magharibi ambako sherehe za kuapishwa kwa kiongozi huyo zinafanyika likionya kuwachukulia hatua kali wale wote wenye nia ovu ya kuvunja sheria.

Kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharibi ameta onyo kali pia kwa viongozi wa vyama vya upinzani vya ACT Wazalendio na CHADEMA kutoandamana na yeyote atakayejitokeza hawata sita kumchukulia hatua kali za kisheria.

Maelezo ya video, Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Kauli ya vyama vya upinzani

Onyo hilo limekuja baada ya vyama vya upinzani kutangaza kuwa na maandano hii leo, Tanzania bara na visiwani.

ACT

Chanzo cha picha, Getty Images

Vyama vikuu vya upinzani nchini Tanzania Chadema na ACT-Wazalendo vinataka kurejewa kwa Uchaguzi Mkuu nchini humo.

Vyama hivyo viwili vinapinga matokeo ya uchaguzi wa Jumatano ambapo rais aliye madarakani John Magufuli amekwishatangazwa mshindi.

Katika mkutano wa wanahabari wa pamoja baina ya viongozi wa Chadema na ACT Wazalendo vyama hivyo pia vimeitisha maandamano ya nchi nzima ili kudai kurejewa kwa uchaguzi huo.

Mwenyekitiwa Chadema Taifa Freeman Mbowe ameeleza kuwa: ''kilochofanyika si uchaguzi ni unyang'anyi wa demokrasia uliofanywa na ZEC (Tume ya Uchaguzi Zanzibar) na NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) .''