'Nimetuhumiwa kuwateka watoto wangu wa kizungu'

Peter, Anthony, Johnny and their dog

Chanzo cha picha, Fosterdadflipper

1px transparent line

Suala la kuasili watoto mara nyingi linahusisha wazungu kuasili watoto wa kiafrika ama wa kihindi.

Lakini wazazi wa Kiafrika au wa Kihindi wakiasili watoto wa Kizungu maafisa wa usalama au jamii huenda ikatilia shaka hatua hiyo kwasababu ni nadra sana kuona jambo kama hilo.

Hali hiyo ilimkumba mwanaume mmoja raia wa Uganda ambaye alimuasili kuasili mtoto wa kizungu nchini Marekani

Siku moja Peter akiandamana na mwanae Johnny mwenye umri wa miaka saba kuelekea kwenye gari lao walilokuwa wameegesha nje ya duka, walikutana na mwanamke aliyeonekana kuwa na wasiwasi ambaye amuuliza Peter…

"Yuko wapi mama yake huyu kijana mdogo?" aliuliza.

"Mimi ndiye baba yake," Peter alimjibu.

Mwanamke huyo alipiga hatua nyuma kidogo na kusimama mbele ya gari la Peter. Aliangalia nambari ya usajili ya gari kisha akatoa simu mfukoni na kwanza kupiga.

"Haloo, hapo ni kituo cha polisi,"alisema kwa upole kwenye simu. "Sasa, kuna mtu mweusi hapa ambaye nadhani amemteka kijana mdogo wa kizungu."

Johnny aliingia na uwoga ghafla akimwangalia usoni Peter ambaye ni baba yake mlezi ambaye alimwekea mkono mabegani kama ishara ya kumtuliza na kumwambia: "Ni sawa," alimwambia mwanae.

Peter and Johnny

Chanzo cha picha, Fosterdadflipper

Short presentational grey line

Peter alilelewa katika mazingira ya umasikini nchini Uganda, karibu na mpaka wa Rwanda na DR Congo, eneo ambalo ni njia ya kuingia na kutoka katika mbuga kadhaa za kitaifa.

Maisha yake ya utotoni yanamkumbusha hali ngumu aliyopitia.

Yeye na familia yake walikuwa wakilala chini kwenye sakafu ya nyumba yao iliyokuwa na vyumba viwili.

Peter's mother stands outside the house where he grew up

Chanzo cha picha, Fosterdadflipper

Maelezo ya picha, Mama yake Peter akiwa nje ya nyumba ambayo alikulia

Akiwa na umri wa miaka 10, Peter aliamua kutoroka nyumbani kwao na kwenda kutafuta ''maisha mazuri'' mjini Kampala kama mtoto wa kurandaranda.

Alipofika Kampala Peter baada ya safari ya karibu siku nzima, alishuka kwa gari na kwenda katika sokoni karibu na kituo cha mabasi ambako alikutana na wauzaji bidhaa na kuomba kazi yoyote bora apate chakula.

Peter and Jacques.

Chanzo cha picha, Fosterdadflipper

Maelezo ya picha, Jacques Masiko, alimchukua Peter kutoka mtaani na kumpeleka shule

Peter aliishi mitaani kwa miaka kadhaa ambako alipata marafiki wengi ambao pia walikuwa wkiishi mitaani kama yeye. Peter anasema alijifunza mbini tofauti za maisha ambazo zilimwezesha kuwatambua watu wakarimu.

Mmoja kati ya watu hao ni Jacques Masiko, ambaye alikuwa akimnunulia Peter chakula kila akitoka sokoni kufanya manunuzi ya nyumbani.

Baada ya karibu mwaka mmoja, Bw. Masiko alimuuliza Peter ikiwa angelipendelea kusoma shule. Peter aliitikia ombi lake na hatimaye akajiunga na shule mjini Kampala.

Baada ya mieze sita familia ya Bw. Masiko iliamua kumchukua Peter na kuishi naye. Katika nyumba ya Jacques Masiko, Peter alipata mtu aliyemtunza kama baba yake mzazi.

Naye aliamua kulipa wema wake kwa kufanya vyema masomoni na hatimaye akapata udhamini wa elimu ya juu katika chuo kikuu nchini Marekani.

Miongo kadhaa baadaye Peter mwenye umri wa miaka 40 na ambaye anaishi nchini Marekani na kufanyia kazi na shirika moja lisilokuwa la kiserikali wakati mwingine amekuwa akiwashawishi wadhamini na kusafiri nao hadi Uganda ili kuwasaidia watoto kutoka jamii masikini.

Katika moja ya safari zake hizo nchini Uganda alikutana na familia moja ya Kizungu ikisafiri na binti yao mwafrika waliye msaili.

Peter, Anthony and Johnny on the stairs with their dog

Chanzo cha picha, Fosterdadflipper

Na hapo ndipo wazo la kuwasaili watoto wa kizungu lilimjia Peter ambaye alifahamu kuwa huenda kuna watoto wa Marekani ambao pia wanaishi katika mazingira magumu sawa na wenzao wa Uganda.

Aliporejea nyumbani kwake North Carolina, Peter aliamua kwenda katika makazi ya watoto na kuomba kufanya kazi ya kujitolea.

"Ushawahi kuwa na wazo la kuwa mzazi mlezi?" Mwanadada mmoja katika ofisi ya shirika linaloendesha makazi ya watoto alimuuliza huku akichukua maelezo yake.

"Ndio japo niko mwenyewe sina mke,"Peter alimjibu.

"Kwa hivyo?" alimuuliza na kusema "kuna wavulana wengi hapa ambao wangelipendelea kuwa na wanaume ambao wanaweza kuwatazama maishani kama mzazi mlezi."

Kulikuwa na mwanamue mmoja ambaye hakuwa na mke aliyeamua kuwa mzazi mlezi katika Jimbo la North Carolina wakati huo.

Alipowasilisha ombi lake, Peter alidhani moja kwa moja atapewa mtoto mwafrika mwenye asili ya Marekani. Lakini alipatwa na mshangao mtoto wa kwanza aliyepewa kumlea alikuwa mzungu wa miaka mitano.

"Na hapo ndipo niligundua watoto wote wanahitaji kuwa na makazi, na haijalishi rangi ya ngozi yake," anasema Peter.

"Sawa na jinsi Bw. Masiko alivyonipatia fursa maishani, ndivyo nilivyotaka kuwafanyia watoto wengine."

Short presentational grey line

Baada ya muda wa kama miaka mitatu Peter aliwalea watoto tisa kwa kutumia nyumba yake kama sehemu ya kuwatunza watoto kwa miezi kadhaa kabla ya wao kuungana tena na wazazi wao.

Walikuwa Waafrika, Wahispania na Wazungu.

"Kitu kimoja ambacho kilinipatia changamoto ni kwamba sikuwa nimejitayarisha kimawazo mtoto anapoondoka," alisema.

Anthony and Peter

Chanzo cha picha, Fosterdadflipper

Peter alikuwa na mazoea ya kukaa kwa muda kabla ya kuchukua mtoto mwingine baada ya aliyekuwa naye kuondoka.

Siku moja alipigiwa simu kutoka makazi ya watoto na kufahamishwa kuhusu Anthony, kijana wa miaka 11 ambaye alisemakana kuhitaji mahali pa kula kwa dharura, Peter alijaribu kupinga ombi hilo.

Lakini hatimaye, Peter alikubali kumchukua Anthony - mwenye asili ya kizungu- ambaye aliletwa kwake usiku saa saa tisa. Asubuhi iliyofuata Anthony na Peter walijumuika pamoja kwa kifungua kinywa

"Unaweza kuniita Peter," alimwambia kijana huyo.

"Je naweza kukuita baba?" Anthony aliuliza.

Peter alishangaa sana. Kwa sababu ndio mwanzo wameanza kujuliana hali, japo hawakuwa pamoja kwa muda mrefu Peter anasema alitokea kumpenda sana akilinaganisha na watoto wengine aliowalea kwa muda.

Wawili hao walikaa pamoja wikendi nzima wakipika na kuzungumza pamoja na walifurahia sana kufanya hivyo.

"Tunajaribu kuzoena kadri ya uwezo wetu."

Peter and Anthony playing video games

Chanzo cha picha, Fosterdadflipper