Madonna: 'Mwanangu atakuwa rais wa Malawi'

Nyota wa muziki wa Pop nchini Markani na mwanawe david wameitembelea Malawi kila mara taifa alilomuasili mwanawe

Chanzo cha picha, AFP/Getty images

Maelezo ya picha, Nyota wa muziki wa Pop nchini Markani na mwanawe david wameitembelea Malawi kila mara taifa alilomuasili mwanawe
Muda wa kusoma: Dakika 1

Nyota wa muziki wa pop nchini Marekani Madonna amesema kuwa mwanawe David Banda atakuwa rais wa Malawi siku zijazo katika ujumbe aliouchapisha katika mtandao wa Twitter akimsifu mvulana huyo mwenye umri wa miaka 12.

Mwanamuziki huyo wa Marekani ana watoto sita ,wanne akiwa aliwahasili kutoka Malawi. Madonna amekuwa na uhusiano mbaya na mamlaka ya taifa hilo la kusini mashariki mwa Afrika.

Mwaka 2013 Malawi ilimshutumu Madonna kwa kutumia ushawishi wake kuwatishia maafisa wa serikali akisisitiza mchango wake kwa taifa hilo mbali na kutaka kupewa heshima.

Meneja wa Madonna aliishutumu serikali ya Malawi kwa kiuwa na chuki dhidi ya shirika la hisani la nyota huyo la Raising Malawi ambalo alilianzisha 2006 mwaka huohuo aliomuasili David.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

David Banda ndio mkubwa kati ya watoto hao wanne. Uasili wake ulizua hisia kali miongoni mwa raia kwa kuwa sheria ya Malawi inawataka wazazi waliomchukua mtoto kuishi ndani ya taifa hilo mwaka mmoja kabla ya kuasili mtoto.

Kikwazo hicho kiliondolewa kwa nyota huyo wa muziki ambaye alimwambia Oprah Winfrey wakati huo kwamba hakuna sheria za kuasili ambazo zilikuwa zinadhibiti uasili wa kigeni.

Baada ya kukata rufaa mahakama ya juu ilimpatia haki za kuasili mwanawe wa pili kutoka Malawi Mercy James.

Chanzo cha picha, Twitter/@Madonna

Maelezo ya picha, Baada ya kukata rufaa mahakama ya juu ilimpatia haki za kuasili mwanawe wa pili kutoka Malawi Mercy James.

Mwaka 2009, mahakama ya taifa hilo ilikataa ombi la Madonna la kuasili msichana chini ya sheria kwamba hajaishi katika taifa hilo la Afrika kwa miezi 18 ili kuweza kuasili.

Baada ya kukata rufaa mahakama ya juu ilimpatia haki za kuasili mwanawe wa pili kutoka Malawi Mercy James.

Mwaka uliopita ,Malawi ilimpatia nyota huyo ruhusa nyengine ya kuasili tena na akawa mama wa pacha wa kike Esther na Stella Mwale.