Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 14.12.2019: Saul, Haaland, Sousa, Minamino, Emery, Alonso, Foyth

Atletico Madrid wanajiandaa kupunguza bei yao wanayoitaka kwa kiungo wa kati Muhispania Saul Niguez,

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Atletico Madrid wanajiandaa kupunguza bei yao wanayoitaka kwa kiungo wa kati Muhispania Saul Niguez,

Atletico Madrid wanajiandaa kupunguza bei yao wanayoitaka kwa kiungo wa kati Muhispania Saul Niguez, mwenye umri wa miaka 25, hadi kiwango cha pauni 85 , na kuituma ujumbe kwa Manchester United. (Telegraph)

Meneja wa RB Leipzig Julian Nagelsmann amaefanya mazungumzo ya uhamisho na kiungo wa mashambulizi wa , Red Bull Salzburg mchezaji wa kimataifa wa Norway Erling Haaland, mwenye umri wa miaka 19, aliyehusishwa na taarifa za kuhamia Manchester United mwezi Januari. (Mail)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer alisafiri kwa ndege hadi Salzburg kukutana Haaland Ijumaa huku klabu hiyo ikiwalenga wachezaji wa kiwngo cha juu cha timu hiyo. (Mail)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer alisafiri kwa ndege hadi Salzburg kukutana Haaland
Maelezo ya picha, Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer alisafiri kwa ndege hadi Salzburg kukutana Haaland

Wakati huo huo, mkurugenzi wa soka wa Red Bull Salzburg Christoph Freund anaamini kuwa ni "mapema saba " kwa Haaland kuondoka klabu hiyo ya Austria . (Mirror)

Kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira, mwenye umri wa miaka 23, anaweza kuondoka Arsenal kwa jili ya kuhamia Napoli kwa uhamisho wa pauni milioni £21m , lakini klabu hiyo ya ligi ya Serie A inataka kufanya mazungumzo ya mkataba wa mkopo kwanza.(Mirror)

Kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira, mwenye umri wa miaka 23, anaweza kuondoka Arsenal
Maelezo ya picha, Kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira, mwenye umri wa miaka 23, anaweza kuondoka Arsenal

Arsenal na Manchester United wamejipanga kupambana kwa ajili ya kumchukua kiungo wa kati wa Sweden Dejan Kulusevski, mwenye umri wa miaka 19, ambaye anacheza kwa mkopo katika klabu ya Parma kutoka Atalanta na amethamanishwa kwa bei ya pauni milioni £42m. (Mirror)

Meneja wa Bordeaux Paulo Sousa, anasema kuwa anajaribu kutofikiria sana juu ya hali yake ya siku zijazo baada ya kuhusishwa ghafla na kazi ya umeneja wa Arsenal. (Goal.com)

Jurgen Klopp amedokeza kuwa Liverpool inaweza kurejea sokoni kuwasaka wachezaji zaidi wa Red Bull Salzburg
Maelezo ya picha, Jurgen Klopp amedokeza kuwa Liverpool inaweza kurejea sokoni kuwasaka wachezaji zaidi wa Red Bull Salzburg

Jurgen Klopp amedokeza kuwa Liverpool inaweza kurejea sokoni kuwasaka wachezaji zaidi wa Red Bull Salzburg baada ya kumpata winga wa Japan Takumi Minamino, mwenye umri wa miaka 24, kabla ya kipindi cha uhamisho wa wachezaj cha mwezi Januari. (Mirror)

Meneja wa zamani wa Arsenal manager Unai Emery tayari amekataa ofa ya kazi kutoka kwa klabu ya Everton na timu nyingine mbili za ligi ya Uchina. (Marca)

Atletico Madrid wanaangalia uwezekano wa kumchukua mchezaji wa safu ya nyuma-kushoto wa Chelsea, mchezaji wa kimataiga wa Uhispania Marcos Alonso, mwenye umri wa miaka 28. (Star)

Atletico Madrid wanaangalia uwezekano wa kumchukua mchezaji wa safu ya nyuma -kushoto wa Chelsea , mchezaji wa kimataiga wa Uhispania Marcos Alonso
Maelezo ya picha, Atletico Madrid wanaangalia uwezekano wa kumchukua mchezaji wa safu ya nyuma -kushoto wa Chelsea , mchezaji wa kimataiga wa Uhispania Marcos Alonso

Meneja wa Chelsea Frank Lampard hatafanya mazungumzo na Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 33, kiungo wa kati wa Brazil Willian, 31, au winga Muhispania Pedro, 32 - ambao mikatapa yao inakamilika mwishoni mwa msimu - juu ya mustakabal wao kimchezo hadi mwezi ujao. (Independent)

Lampard anasisitiza kuwa Chelsea wako sokoni tu kuwasaka wachezaji wenye "haiba ya juu" katika kipindi cha dirisha la uhamisho mwezi Januari. (Express)

Crystal Palace wanaweza kumuhamisha mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya Ufaransa anayeichezea Chelsea Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 33. (Mirror)

Lampard anasisitiza kuwa Chelsea wako sokoni tu kuwasaka wachezaji wenye "haiba ya juu" katika kipindi cha dirisha la uhamisho mwezi Januari. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lampard anasisitiza kuwa Chelsea wako sokoni tu kuwasaka wachezaji wenye "haiba ya juu" katika kipindi cha dirisha la uhamisho mwezi Januari. (Express)

Sheffield United wanapanga kuanza mazungumzo mapya na with mlinzi wa Jamuhuri ya Ireland Kaskazini Enda Stevens, mwenye umri wa miaka 29. (Football Insider)

Meneja wa Tottenham Jose Mourinho angependa kupata muda zaidi wa kuwafunza wachezaji kuliko kuwananunua wachezaji wapya. (Football.London)

Mourinho ameachana na mpango wa kumnunua difenda Juan Foyth wa Argentina mwenye umri wa miaka 21-anayetaka kuondoka kwa mkopo mwezi Januari . (Sky Sports)

Jose Mourinho angependa kupata muda zaidi wa kuwafunza wachezaji kuliko kuwananunua wachezaji wapya.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jose Mourinho angependa kupata muda zaidi wa kuwafunza wachezaji kuliko kuwananunua wachezaji wapya.

Kiungo wa kati wa Manchester United Muingereza Jess Lingard,mwenye umri wa miaka 26, alifumfungukia meneja Ole Gunnar Solskjaer baada ya tatizo la kuwa nje ya uwanja na namna ilivyoathiri hali yake kimchezo mwanzoni mwa msimu. (Mail)

Rangers wanamfuatilia mshambuliaji wa Charlton Lyle Taylor, mwenye umri wa miaka 29, ambaye pia anatafutwa na mahasimu wa Championi Ligi mkiwemo Swansea, West Brom na Sheffield Wednesday. (Sky Sport

Kiungo wa kati wa Manchester United Muingereza Jess Lingard,mwenye umri wa miaka 26, alifumfungukia meneja Ole Gunnar Solskjaer
Maelezo ya picha, Kiungo wa kati wa Manchester United Muingereza Jess Lingard, alifumfungukia meneja Ole Gunnar Solskjaer juu ya masaibu ya kukaa nje ya uwanja.