Nyota wa filamu Genevieve Nnaji ang'ara Netflix

Nyota wa filamu nchini Nigeria Genevieve Nnaji tayari ameonyesha wazi kuwalazimisha watu kumfikiria mara baada ya kutolewa katika filamu yake inayooneshwa Netflix katika tuzo za Oscars na kuna uwezekano mkubwa kuwa hatua hiyo haijamkatisha tamaa.

Kutolewa kwa filamu ya Lionheart mwanzoni mwa mwezi katika kipengele cha filamu bora ya kimataifa kunaweza kumpa mafanikio makubwa zaidi kwa siku zijazo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 40 ameweza kutengeneza filamu zaidi ya 80 kwa miongo miwili iliyopita na ilimfanya apate umaarufu mkubwa katika tasnia ya filamu nchini Nigeria na barani Afrika kwa ujumla.

Ni mafanikio licha ya kupata changamoto kadhaa kama ile ya kufunguwa na studio kubwa ya filamu nchini Nigeria mwaka 2004, yeye pamoja na waigizaji wengine.

Alifungiwa na Nollywood

Studio zinazotengeneza filamu nchini Nigeria zilizopo mji wa kibiashara wa Lagos na Onitsha zilianzishwa mwaka 1990 mpaka mwanzoni mwa mwaka 2000.

Walitoa udhamini kwa waandaaji wa filamu na kuwaambia nani wawakodishe, alisema ripota wa BBC Igbo Vining Ogu, ambaye alikuwa muandaaji wa fikamu.

"Kuna wakati ambao hizo studio zilihisi kuwa wasanii wa daraja 'A' walikuwa wanachukua pesa nyingi sana na walikuwa wanahisi kunyimwa uhuru wao," alisema.

Muigizaji mmoja alikuwa anapokea dola 28,000 taslimu mwanzoni mwa mwaka 2000 , kiwango cha fedha ambacho kilikuwa kikubwa.

Wakati ambao hakukuwa na waandaaji ambao walikuwa werevu kwenda tofauti na matakwa ya studio, Nnaji alijikuta amepoteza ajira yake na hivyo kuamua kuingia katika muziki na kutoa albamu yake aliyoiita 'One Logologo Line'.

Albamu yake moja tu aliyowahi kuitoa , inakumbukwa kuwa na wimbo unaotwa 'No More', wimbo wa kimapenzi ukionyesha tasnia yake: "Hakuna kulia tena, hakuna kugombana tena , hakuna machozi tena, nimepata uhuru wangu , nguvu zangu na mengine mengi."

Mwandishi na muongozaji filamu Ishaya Bako alifuatilia kukua kwa muigizaji huyu na uhuru wa waandaji filamu wa Nigeria mpaka alipofutiwa.

"Wakati studio hiyo ilipokuepo kulikuwa kuna mapungufu lakini kuna mafanikio makubwa yalipatikana ," alisema Bako, yeye alifanya kazi na Nnaji ijulikanayo kama 'Road to Yesterday' mwaka 2015 - wakati ambapo alijitambulisha kuwa muandaaji filamu.

"Nilimfanya kutambua kuwa kuna maisha nyuma ya kamera," alisema.

Kuanzia hapo alionyesha kuwa ana weledi mkubwa zaidi ya hata filamu alizokuwa anaonekana.

Genevieve alianza kujulikana katika filamu kwa jina la Sharon Stone

Alianza kuigiza akiwa na umri wa miaka minane katika kituo maarufu cha televisheni ambacho kinaonyesha filamu.

Aling'ara zaidi akiwa na umri wa miaka 19 katika filamu za Nollywood .

Muongozaji wa filamu Adim Williams, anasema anajivunia kuwa sehemu ya kuibua kipaji cha muigizaji huyo. Anasema kuwa aliandika filamu mwaka 2002 na Genevieve alitambulika kwa jina la Sharon Stone.

Muongozaji huyo wa filamu anasema kuwa anaweza kumuelezea Nnaji kama muigizaji mwerevu sana na alionekana kuwa mkorofi mara ya kwanza alipokutana naye.

Unaweza kuvutiwa kusoma hizi pia:

Tabia yake hiyo ilimsaidia kukua katika tasnia yake katika siku za mwanzoni wakati akiigiza kama msichana mrembo , anayevutia na anayependwa..

Genevieve amekulia katika jiji la Lagos - baba yake akiwa muhandisi na mama yake akiwa mwalimu.

"Yeye bado ni malkia wetu na huwa anakuja kwenye sherehe akiwa na morali ya ushindi," aliiambia BBC.

Mwaka 2011 Genevive alitunukiwa tuzo na serikali ya Nigeria.

Je Netflix itaweza kusaidia kuboresha viwango vya filamu?

Mwaka 2018 wakati Netflix ilipotangazwa kuwa na haki miliki ya filamu ya Lionheart, muongozaji filamu wake alijivunia kuwa inakuza sekta ya filamu nchini Nigeria.

Nollywood inasifika kwa kuwa na utajiri katika tasnia ya filamu ingawa imekuwa haitoi kipaumbele kwa kuwalipa vizuri waandishi wa simulizi na waandaaji wa maudhui.

Kwa bajeti ya kuandaa filamu kwa bajeti ya kiasi cha $15,000 na $70,000, filamu nyingi zinatengenezwa ndani ya mwezi huku zikitarajiwa kuwa na faida.

Kenneth Gyang, ambaye ni muandaaji wa filamu wa kujitegemea anasema kuwa Nnaji kufanya kazi na Netflix kumewafumbua watu macho na kuona kuwa kuna fursa za kupata pesa katika sehemu tofautitofauti.

"Netflix inazingatia ubora wa juu wa filamu.Kwa sasa sisi waandaaji wa filamu tunajua kama filamu ni nzuri ,tunaweza kuiuza na kupata pesa nyingi zaidi", aliiambia BBC.

Mkosoaji wa filamu Oris Aigbokhaevbolo anakubali kuwa Netflix imeweza kuwaonesha watengeneza filamu kuwa filamu nzuri zinalipa.

Wakati filamu ya Lionheart ilipochaguliwa katika tuzo za Oscars, Nnaji alielezewa kuweka historia katika tasnia ya filamu nchini Nigeria.

Hata kama filamu hiyo iliondolewa katika kipengele cha filamu bora za mataifa kwa kuwa na mazungumzo yote ya kiingereza.

Bado filamu hiyo ya Lionheart, ambayo Nnaji ni nyota inatumia lugha ya kiingereza zaidi na huku kukiwa na dakika 11 tu ambapo lugha ya Igbo ilitumika- hiyo ndio ilikuwa sababu ya kutolewa.

Nnaji aliandika kwenye kurasa za twitter " Hatukuchagua nani angetutawala."

"Nollywood imedhihirisha kuwa ngumu kuleta mabadiliko labda sasa Genevieve na wengine wataleta mabadiliko," alisema bwana Aigbo khaevbolo.