Polio: 'Sikuiamini chanjo mpaka mtoto wangu alipopata polio'

Chanzo cha picha, Getty Images
Adamu Misa alikuwa anafukuza wahudumu wa afya nyumbani kwake huko kaskazini magharibi ya Nigeria lakini sasa anafanya kampeni ya chanjo ya polio mara baada ya mtoto wake kufariki kutokana na ugonjwa wa polio.
Mtoto wake wa kiumeBuhari, mwenye miaka minane, usiku mmoja alienda kulala akiwa ana afya njema kabisa lakini alipoamka asubuhi alikuwa hana uwezo wa kutembea.
Cha kusikitisha ,baba yake alimpeleka kwa waganga wa kienyeji, mganga ambaye aliwajibu kuwa kuna pepo mbaya amempitia mtoto wake na hivyo kumpaka dawa za kienyeji.
Unaweza pia kusoma:
Hawakuweza kugundua mpaka jirani yake alipomshuku Buhari kuwa ana ugonjwa wa polio na hivyo kumpeleka hospitali haraka kwa ajili ya matibabu.
"Alikuwa hawezi kufungua vidole vyote kama mimi," Bwana Misa alisimulia miaka mitano baadae akiwa amekaa chini ya mti wa nyumbani kwake.

Kwa sasa Bwana Adamu anafanya kampeni ya chanjo, anatumia sauti yake kuwashauri watu wanaopinga chanjo katika jamii yake.
"Nimeshuhudia mtoto wangu mwenyewe akiathirika, hivyo yeyote atakayepinga chanjo hiyo nitamuonyesha mfano wa mtoto wangu, Bwana Adamu aliiambia BBC.
Wazazi wengi kaskazini mwa Nigeria eneo ambalo Waislamu wengi wanaishi humo huwa wanakataa kuwapeleka watoto wao kupata chanjo kutoka na kufungwa na imani zao.
Tatizo hili la watu kugomea chanjo halipo Nigeria peke yake.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), watu kupinga chanjo ni tatizo la ulimwengu mzima.
Kuna baadhi ya maeneo bado watu ni wagumu kukubali chanjo kama vile baadhi ya sehemu katika bara la Ulaya na Marekani , Japan na India na baadhi ya maeneo ya Pakistan.
'Tetesi zilizopo vijijini'
Waziri wa afya nchini Nigeria anasema kuwa watoto wanapaswa kupewa chanjo mara sita katika mwaka wao wa kwanza dhidi ya magonjwa yanayoua, polio ukiwa ugonjwa mmoja wapo.
Mtoto anayekosa chanjo hizo yuko hatarini.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hospitali moja ya kijiji ambayo Bwana Misa anaishi kuna huduma za mara kwa mara za chanjo, lakini maafisa wa afya wanahangaika kuwashawishi wazazi kupeleka watoto wao kupata chanjo.
Kuna ripoti ya kuongezeka kwa watu wanaopinga chanjo nchini Nigeria haswa maeneo ya kaskazini.
Watu hao wanaamini kuwa chanjo imetengenezwa ili kukabiliana na idadi ya watu.
Watu wapatao milioni 200, wengi wakiwa wametoka barani Afrika ambapo inakadiriwa kuwa na watu wengi zaidi duniani ifikapo mwaka 2050.
"Baba yangu alikuwa ana watoto 13 na hakukua na chanjo na tuliishi bila chanjo hivyo watoto wangu pia wataishi," alisema Bwana Misa.
Kwa sasa Bwana Misa ana watoto 10 na ana mpango wa kuwa na watoto 16 na wakati watoto wake wawili walivyopatiwa chanjo alikuwa kwenye ziara ya kikazi.
Buhari ni mtoto wake wa tatu.
"Niliporejea nilisikia tetesi kuwa wanawapa chanjo watoto wetu, kuna shirika la kimataifa ambalo linatoa kitu fulani katika mishipa yao.
"Niliposikia hivyo , nilisema kuwa sitaruhusu mtoto wangu kupewa chanjo."

Unaweza kusoma pia kuhusu

'Maamuzi yangu '
Adamu Bawuro anajulikana na maafisa wa afya kama mtu anayepinga chanjo.
Alisema kuwa watoto wake hawatapewa chanjo kwa sababu yeye mwenyewe hakupewa chanjo hivyo haoni umuhimu wake.
"Shirika la Afya Duniani WHO, wamekuwa wakihamasisha watu, wao walikuwa wanafanya utafiti na nyinyi je?
"Niliangalia mtandaoni na hakuna sababu iliyopo duniani ambayo inaweza kunifanya nikubali. Huu ni uamuzi wangu binafsi," alisema.
Maoni kama hayo ya Bwana Bawuro kuhusu chanjo hayana msingi wowote, alisema Magnus Ogaraku, daktari magharibi mwa jimbo la Kogi.
"Tafiti za kisayansi zimethibitisha usalama wa chanjo hizo, madhara na faida ambazo inazo kwa jamii", aliiambia BBC.
Anakubali kuwa kuwa kuna wakati ambapo kinga ya mwili inashindwa kufanya kazi bila kujua chanzo chake.
Polio ni bakteria wanaopatikana katika maji machafu na mazingira ambayo sio masafi.
Katika maeneo kadhaa nchini Nigeria kuna upungufu wa vyanzo vya maji ya kunywa , na kutokana na hali hiyo, mtoto ambaye hana chanjo ni rahisi kupata maambukizi
Ndio maana chanjo inahamasishwa sana kutolewa.

Polio ni nini?
- Ugonjwa wa Polio huwaathiri watoto wadogo wenye umri wa chini ya miaka mitano
- Huwa unaenea kwa virusi na kumsababisha mtu kathirika katika mfumo wa mishipa na kusababisha mtu kupooza.
- Dalili zake ni pamoja na homa, kichwa kuuma, uchovu, kutapika, maumivu ya shingo na miguu
- Kati ya watu 200, mmoja huwa anapooza .Na miongoni mwa 5% mpaka 10% hufariki
- Mpaka sasa ni nchi mbili tu duniani Afghanistan na Pakistan -ambazo bado ziko na ugonjwa huu kwa kiwango cha juu. Watu zaidi ya 125 walikufa na polio mwaka 1988
Chanzo: World Health Organization

Nigeria bado haijaripoti kesi mpya ya ugonjwa wa polio kwa miaka mitatu iliyopita na inatarajiwa kutangazwa kuwa taifa lisilokabiliwa na polio ifikapo katikati ya mwaka -2020
Lakini baadhi ya watu wana hofu bado kuwa ugonjwa huo bado upo katika maeneo ya pembezoni maeneo ambayo visa vyake huwa havitangazwi au kurekodiwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Laureta Anaza ambaye anatoa mafunzo kwa watu wanaojitolea kwa huduma za afya na anaamini kuwa ushawishi unahitajika kutoka kwa viongozi wa dini na kuzingatia tamaduni za watu.
Yeye anasema kuwa kundi lake lilikuwa linatoa uhamasishaji na elimu wakishirikiana na viongozi wa dini na viongozi wa jadi ili kuwaelimisha wazazi kuhusu faida za chanjo kwa watoto.
Pamoja na kwamba bado kuna watu ambao wanapinga vikali huduma hiyo lakini wana sauti za watu waliopitia changamoto hiyo kama ya bwana Misa ambaye sasa anawaunga mkono.
"Sasa nimeelewa kuwa simulizi ya maisha yangu sio kama ya baba yangu," alisema.
"Ninafahamu vizuri kuhusu chanjo na ninaweza kuwaelimisha wale ambao hawaamini."












