Tetesi za soka Ulaya Jumatano tarehe 13.11.2019: Mbappe, Ronaldo, Haaland, Napoli, Xhaka, Pellegrini, Matic

Real Madrid wanaangalia uwezekano wa kutoa malipo makubwa kuwahi kushuhudiwa kumchukua Kylian Mbappe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Real Madrid wanaangalia uwezekano wa kutoa malipo makubwa kuwahi kushuhudiwa kumchukua Kylian Mbappe

Real Madrid wanaangalia uwezekano wa kutoa malipo makubwa kuwahi kushuhudiwa ya pauni milioni £340 kwa ajili ya mchezahi wa safu ya mashambulio wa Paris St Germain mwenye umri wa miaka 20 Kylian Mbappe. (Le Parisien via Calciomercato)

Unaweza pia kusoma;

Cristiano Ronaldo hatalipishwa faini na Juventus kutokana na mienendo aliyoonyesha baada ya kutolewa uwanjani na badala yake kuwekwa mchezaji wa ziada katika mchezo wa pili.

Ingawa mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 34, atatarajiwa kuomba msamaha kwa wachezaji wenzake. (Gazzetta dello Sport, in Italian)

Cristiano Ronaldo anatarajiwa kuomba msamaha
Maelezo ya picha, Cristiano Ronaldo anatarajiwa kuomba msamaha

Barcelona wanamtaka mshambuliaji wa timu ya Salzburg mwenye umri wa miaka 19 Erling Braut Haaland kama mtu atakayechukua nafasi ya Luis Suarez mwenye umri wa miaka 32, lakini wanasitasita kuafiki kiwango cha thamani ya mchezaji huyo wa klabu ya Austria cha pauni milioni 85. (ESPN)

Rais wa klabu ya Napoli Aurelio de Laurentiis amepokea Euro milioni 560 kwa ajili ya Ligi ya klabu ya Serie A kutoka Qatar huku mashabiki wakipinga na wachezaji wakigoma . (Mail)

Nemanja Matic anataka kuondoka Manchester United ikiwezekana mwezi Januari

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nemanja Matic anataka kuondoka Manchester United ikiwezekana mwezi Januari

Tottenham wanatarajia kumchukua mshambuliaji wa kati wa timu ya Roma ya Italia Lorenzo Pellegrini, mwenye umri wa miaka 23, kama mtu anayeweza kuchukua nafasi ya Christian Eriksen. (Football Italia)

Nemanja Matic anataka kuondoka Manchester United, ikiwezekana mwezi Januari, huku kiungo huyo wa kati Mserbia mwenye umri wa miaka 31 akitarajiwa kwenda Italia. (telegraph)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino huenda akafutwa kazi baada ya Spurs kushindwa na West Ham baada ya kipindi cha mapumziko cha kimataifa. (Telegraph)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino huenda akafutwa kazi
Maelezo ya picha, Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino huenda akafutwa kazi

Pep Guardiola, ambaye alikuwa kocha wa Bayern Munich kwa misimu mitatu kabla ya kuwasili Manchester City, anaweza kurejea katika Bavaria wakati Niko Kovac anasemekana kuondoka katika timu hiyo. (The Athletic, subscription required)

Fiorentina wamefanya mazungumzo na meneja wa zamani wa Inter Milan Luciano Spalletti huku wakionyesha kuwa wamemchoka Vincenzo Montella. (Football Italia)

Lyon wanasaka mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lyon wanasaka mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema

Arsenal wanamfanyia majaribio mchezaji wa safu ya kati wa klabu ya Colorado Rapids Cole Bassett na kijana huyo Mmarekani mwenye umri wa miaka 18 anaweza kujiunga na Gunners mwezi Januari. (Sun)

Wolves wameafiki mkataba wa kumleta kikosini Mholanzi Nigel Lonwijk mwenye umri wa miaka 17 kutoka klabu ya PSV Eindhoven anayecheza katika safu ya kati ifikapo mwezi Januari kwa pauni £170,000. (ED via Birmingham Live)

Lyon wanasaka mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema, mwenye umri wa miaka 31, kumalizia mchezo kule alikouanzia katika klabu hiyo ya Ufaransa. (Mundo Deportivo, in Spanish)