Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
William Okumu aliyehukumiwa kifo ahitimu Chuo Kikuu
Mfungwa wa zamani aliyekuwa katika orodha ya watu waliyohukumiwa kifo nchini Kenya ameielezea BBC furaha yake alipokuwa akihitimu shahada ya sheria katika chuo Kikuu cha London.
William Okumu, mmoja ya mfungwa wa zamani ambaye amehitimu katika mahafari ya Alhamisi iliyopita katika gereza kuu la Kamiti lililopo katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, ameiambia BBC :
''Ninafikiri dunia nzima sasa inaelewa kuwa kitu kizuri kinaweza kupatikana katika uchafu'' na kuongeza kuwa:'' Hakuna neno la Kiingereza linaloweza kuelezea jinsi ninavyohisi''
Unaweza pia kusoma:
Bwana Okumu ambaye ana umri kati ya miaka 30 na 40, na ambaye aliachiliwa kutoka gerezani mwezi Mei , amesema Shahada ya sheria imebadilisha maisha yake.
Anasema aliweza kutumia ujuzi wake wa sheria alioupata alipokuwa akisoma kama mfungwa kujitetea binafsi na kuwatetea wengine.
Amesema kuwa motisha ya kusomea sheria ilitokana na kutambua kuwa hukumu yake ilitokana na ukosefu wa uelewa unaofaa wa sheria kwani hakuwa na wakili wa kumteteawakati wa kesi yake ya kwanza.
Baada ya mwaka 2017 Mahakama kuu ilitoa uamuzi uliosema hukumu ya kifo "haiendani " na katiba ya kenya, Bwana Okumu, ambaye alifungwa kwa kosa la wizi wa kutumia ghasia na kumiliki mali iliyoibiwa , alikuwa na fursa ya kujitetea mwenyewe mahakamani kwamba hukumu yake ya awali ilikuwa kali sana.
Jaji aliafiki na kupunguza hukumu yake kuwa ya miaka 10, ambayo tayari alikuwa ameitumikia.
Unaweza pia kutazama:
Aliweza kufanya haya kwa msaada wa Mradi wa Magereza ya Afrika (APP), ambayo inafanyia kazi katika nchi zaidi ya 15 kote barani Afrika, ukiwasaidia wafungwa kupata usaidizi wa kisheria.
Kuna zaidi ya wafungwa 50,000 katika magereza nchini Kenyan, wengi wao wakiwa ni wale waliofanya makosa madogo wanaoishi katika mahabusu zilizojaa kupita kiasi kwamujibu wa taasisi ya mtandao ya data za magereza ya World Prison Brief.
Umaskini na viwango vya chini vya elimu miongoni mwa wafungwa mara nyingi huwafanya wasiwe na uwezo wa kupata mawakili wa kuwasaidia kuwatetea katika kesi zinazowakabili.
Licha ya uamuzi wa Mahakama Kuu wa mwaka 2017 , kipengele cha adhabu ya kifo bado kipo katika shertia ya kenya ya uhalifu - ingawa hakuna hukumu ya aina hiyo ambayo imewahi kutolewa katika taifa hilo la Afrika Mashariki tangu mwaka 1987.