Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Sasa ni hatia kuonyesha makalio hadharani Australia
Kuonyesha makalio hadharani sasa ni uhalifu katika jimbo la Victoria nchini Australia.
Hatia hiyo inayojulikana kama ''mooning'' kwa lugha ya kiingereza sasa ina hukumu ya hadi miezi sita jela .
Marekebisho ya sheria hiyo yanalenga kutengenisha utani unaohusisha uchi na ule wa kujionyesha kingono.
Sheria hiyo mpya pia inapiga marufuku uimbaji wa nyimbo chafu pamoja na tabia nyengine zinaozoonekana kuwa za uasherati, uchafu, kukera au kutusi.