Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 31.01.2022: , Halaand, Alli, Henderson, Caleta-Car, Dembele, Carvalho, Nketiah, Ndombele

Kipa wa Manchester United na England Dean Henderson, 24, anatarajiwa kutia saini ya mkopo katika klabu ya Newcastle siku ya misho katika dirisha la uhamisho. (Talksport)

AC Milan huenda ikawasilisha ombi la kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Delle Ali 25, kwa mkopo. (Gazzetta dello Sport)

Mshambuliaji wa Norway Erling Braut Halaanda ,21 anataka kuondoka klabu ya Borussia Dortmund katika msimu wa joto ili kujiunga na Barcelona .

Beki wa Liverpool na Wakes Neco Williams , 20, huenda akauzwa kwa mkopo huku klabu ya Bournemouth ikiwa na hamu naye. (Liverpool Echo)

West Ham imewasiisha ombi la dau la £18m kumsajili beki wa Marseille na Croatia Duje Caleta-Car, 25. (Goal)

Mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele, 24, huenda akaondoka katika klabu hiyo ya Uhispania na licha ya kuweka makubaliano na PSG , Manchester United imeingia katika kinyan5'ganyiro cha kumsaini mshambuliaji huyo wa Ufaransa kwa dau la €20m (£16.6m). (Journalist Pedro Almeida)

Tottenham pia ina hamu ya kumsaini Dembele , lakini haiko tayari kulipa mshahara anaotaka. (Marca)

Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 32, amekubali kuendelea kucheza katika klabu hiyo ili kumaliza kipindi cha msimu uliosalia na klabu ya Barcelona , lakini anahitaji klabu hiyo ya Uhispania kumuuza Dembele mwanzo . (Sport)

Ombi la pili la Crystal Palace la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah limekataliwa , licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa England kusalia na kandarasi ya miezi sita pekee . (Sky Sports)

Hatua ya Lyon ya kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele kwa mkopo imepiga hatua , lakini mkwamo mkubwa katika majadiliano hayo ni hatua ya kutaka kumnunua mchezaji huyomwenye umri wa miaka 25.

Chelsea imewasilisha ombi la kutaka kumsaini winga wa Leeds na Brazil Raphinha , lakini huenda mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 atapatikana katika dirisha la uhamisho la msimu wa joto. (Daily Mail).

Kiungo wa kati wa Switzerland Denis Zakaria, 25, anelekea kujiunga na Juventus baada ya klabu hiyo ya Itali kukubali mkataba na klabu Borussia Monchengladbach. (Goal)

Kiungo wakati wa Mali Brighton Yves Bissouma, 25, huenda akaondoka huku Aston Villa , Tottenham na Manchester United wakiwa nah amu ya kumsajili (Journalist