Mkataba wa Liverpool na Luis Diaz: Kulinganishwa na Luis Figo na hofu za utapiamlo

Muda wa kusoma: Dakika 3

Kusaini mkataba na Liverpool ni hatua ya hivi karibuni ya kihistoria kwa Luiz Diaz, mshambuliaji Mcolombia ambaye wakati mmoja mkufunzi wake alihofia kuwa anaumwa utapiamlo.

Tangu wakati huo amezoea maisha ya Ulaya-baada ya kuwa katika klabu ya Prto kwa miaka mitatu-lakini akiwa na umri wa miaka 18 hajawahi kuondoka katika nchi yake, licha ya kulelewa katika eneo la mpaka na taifa la Venezuela lililopo Kaskazini -mashariki mwa Colombia.

Uzoefu wake wa kwanza wa kusafiri nje ya nchi aliupata katikati mwa mwaka 2015, wakati winga huyu mchanga alipoitwa kuwakilisha nchi yake katika michuano ya Copa America na wazawa.

Akiwa mzaliwa wa kabila la Wayuu -ambayo ni jamii kubwa zaidi ya wazawa nchini Colombia - alifurahi sana baada ya kumfurahisha mwana soka mashuhuri nchini humo Carlos Valderrama.

"Shindano lilifanyika Chile kwahiyo tulisafiri mwendo wa saa tano kwa ndege pale na ungeweza kuona macho yake yaking'ara kwa furaha ya uzoefu wa safari ,"mchezaji wa zamani wa kimataifa Colombia John 'Pocillo' Diaz, aliyefunza timu hiyo, aliiambia BBC Sport.

"Lucho alikuwa akituuliza iwapo tunaweza kula mlo saw ana ule aliokula zaidi ya mara moja. Alikuwa mtu wa mnyenyekevu kiasi hiki ."

Ingawa hilo halijabadilika, kitu kimoja bila shaka kimebadilika- Diaz alisafiri safari nyingi.

Na sasa atasafiri kwenda Liverpool, ambapo anasaini mkataba wa awali wa malipo ya pauni milioni 37.5, akiwa tayari anafurahia miezi sita bora zaidi ya kazi yake.

Diaz alikuwa mchezaji mahiri wakati wa michuano iliyopita ya msimu wa kiangazi ya kombe la Copa America, akiweza kutingisha wavu dhidi ya mataifa kama Brazil na Argentina na kumaliza shindano hilo kama wafungaji wengine wa kiwango cha juu sambamba na Lionel Messi.

Ushindi huo ulifuatiwa na magoli 14 katika mechi 18 akichezea Porto msimu huu, akiwa mchezaji aliyefunga vyema nyumbani na mbali dhidi ya AC Milan katika Championi Ligi:

Diaz mwenye umri wa miaka 25-aligeuka kuwa mchezaji mahiri ajaye katika sola ya Ureno na Liverpool iliamua kuingilia kati haraka kuhakikisha hawamkosi. Klabu nnyingine ikiwa ni pamoja na Tottenham, Newcastle na Everton - zote zimekuwa zikihusishwa na dau la kumchukua.

Changamoto ijayo aliyonayo ni kufuata nyayo za Wacolombia wenzake Radamel Falcao na James Rodriguez, nyota wa zamani wa Porto walioleta mabadiliko makubwa katika Ligi kubwa za Ulaya.

'Anaonekana kuwa na matatizo ya utapiamlo'

Mambo ambayo Diaz alikuwa akiyapenda alipokuwa mtoto ni kuitazama treni ikipita katika Kijiji chao kidogo cha Barrancas mara tatu kwa siku, ikibeba makaa ya mawe kutoka eneo la Cerrejon, moja ya maeneo makubwa zaidi duniani ya machimbo ya makaa ya mawe. Kiwango kikubwa cha mawe hayo kilipelekwa kwa njia ya meli na kusafirishwa hadi Ulaya.

Wakati treni zilipokuwa zikipita, mara nyingi Diaz alijipata akishangaa na kujiuliza iwapo atawahi siku moja kupata fursa ya kutembelea maeneo mengine ya dunia pia.