Afcon 2021: Sadio Mane aisaidia Senegal kuilaza Zimbabwe 1-0

Penalti ya mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane dakika saba kabla ya mechi kukamilika iliisaidia Senegal kuilaza Zimbabwe 1-0 katika mechi ya ufunguzi ya kundi B katika michuano ya kombe la bara Afrika.

Ushindi huo wa Senegal ulikuwa mtamu upande wa timu hiyo ya Simba wa Teranga lakini ukawa uchungu mkali kwa miamba ya Zimbabwe, ambao waliwazuia Senegal katika kipindi kirefu cha mechi hiyo.

Katika dakika nne ya muda wa lala salama , Kelvin Madzongwe alidaiwa kuunawa mpira baada ya kugeuka ili kuzuia shambulio la mchezaji wa ziada Pape Gueye.

Mane alifunga penalti hiyo na kuisaidia timu ya nyumbani kuanza vizuri katika kundi hilo.

Ikiwashirikisha wachezaji wenye umaarifu mkubwa akiwemo nahodha Kalidou Coulibaly na Edward Mendy ambao hawakushiriki kutokona na maambukizi ya corona, Simba hao wa Teranga walikosa nafasi chungu nzima.

Nafasi bora zaidi ilimuangukia kiungo wa kati Gana Gueye muda mfupi kabla ya muda wa mapumziko , lakini nyota huyo wa Paris saint Germain hakuweza kudhibiti pasi safi kutoka kwa Sadio Mane huku akiwa amesalia na goli.

Awali Shambulio la Mane lilizuiliwa na kipa wa Zimbabwe Petros Mhari , ambaye alionesha mchezo mzuri .

Senegal yapata ushindi wa dakika za lala salama

Senegal iliwasili katika michuano hiyo ikiwa na lengo la kushinda kombe lao la kwanza baada ya kupoteza kwa Algeria katika fainali za 2019 , lakini walilazimika kuwatangaza wachezaji 17 pekee kati ya wachezaji 28 kutokana na mchanganyiko wa visa vya corona na majeraha.

Timu hiyo ya Afrika magharibi ilianza vizuri katika mechi hiyo , huku mchezaji wa Bayern Munich Bouna Sarr akipiga shambulio kali la kimo cha nyoka na kutoka nje .

Upande wa pili nahodha Musona alipiga shambulio kutoka miguu 20 na nusra afunge.

Muda mfupi baada ya muda wa mapumziko , Pape Cisse alikosa nafasi nzuri kufunga bao la pekee baada ya kupiga kichwa kilichotoka nje huku kipa Mhari akiwa amewachwa asijue cha kufanya.

Hatahivyo , Senegal - Timu ambayo inaorodheshwa katika nafsi ya juu barani Afrika ilishindwa kuonesha mchezo mzuri dhidi ya Zimbabwe ilioonekana kujitayarisha vyema.

Kabla ya michuano hiyo , kulikuwa na tishio la kupigwa marufuku na FIFA, baada ya bodi moja ya serikali kuchukua udhibiti wa shirikisho la soka nchini humo , hatua ambayo ni kinyume na sheria ya Fifa.

Mabingwa hao wa Afrika Kusini walikuwa wanakaribia kupata sare yao ya kwanza katika michuano hiyo , baada ya kushiriki kwa mara ya 13 , kabla ya kushangazwa wakati refa raia wa Guatamala Mario Escobar alipoonesha katika eneo la penalti huku VAR ikimuunga mkono.