Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Christine Mboma wa Namibia ashinda tuzo ya mwanamichezo bora wa BBC Afrika 2021
Mwanariadha wa Namibia Christine Mboma amechaguliwa kuwa Mwanariadha Bora wa Mwaka wa BBC wa Afrika kwa mwaka wa 2021.
Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 18 alikuwa mwanamke wa kwanza wa Namibia kushinda medali ya Olimpiki alipotwaa medali ya fedha katika fainali ya mbio za mita 200 mjini Tokyo mwaka jana.
"Ninajisikia vizuri na ninajivunia kuwa raia wa Namibia," aliiambia BBC Sport Africa.
"Ninatoa tuzo hii ya BBC kwa Wanamibia wote. Hii ni [tuzo] kwa kazi ngumu niliyofanya."
Mboma iliwashinda wanariadha wa Kenya Eliud Kipchoge na Faith Kipyegon, mwanariadha mwenye ulemavu wa Afrika Kusini Ntando Mahlangu, kipa wa Senegal Edouard Mendy na muogeleaji wa Afrika Kusini Tatjana Schoenmaker kushinda tuzo hiyo.
Anakuwa mwanariadha wa pili wa Namibia kutambuliwa kwa mtindo huo, baada ya mwanariadha Frankie Fredericks kushinda tuzo ya BBC African Sports Star of the Year mwaka wa 1993.
Tuzo hii baadaye ikawa tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika wa Mwaka, ambayo ilianza 2001 hadi 2018 wakati BBC ilibadilisha tuzo hiyo kwa madhumuni yake ya awali kwa kuakisi utofauti wa michezo katika bara.
"Siku zote ni jambo zuri kuweka nchi yangu juu ya ramani . Siku zote ninaifanya nchi yangu kuwa na fahari na ninawashukuru Wanamibia wote walionipigia kura. Watapagawa watakaposikia hili," alisema alipopata tuzo yake.
Mbali na medali yake ya fedha ya Olimpiki, Mboma pia alikuwa bingwa wa Ligi ya Diamond na mshindi wa medali ya dhahabu ya kwa wanariadha wa Chini ya miaka 20 kwa zaidi ya mita 200, na alivunja rekodi ya U-20 mara kadhaa mwaka jana.
Nyakati hizo zote za kasi sana zilikuja muda mfupi baada ya Mboma kuzuiwa kushiriki mashindano aliyopendelea, ya mita 400, mwezi Julai, baada ya kugundulika kuwa na viwango vya juu vya testosterone.
Baraza linalosimamia mchezo huo, Shirikisho la Riadha duniani, huwazuia wanariadha wote walio na viwango vya juu vya testosterone kutoshiriki mbio zozote kati ya mita 400 na maili, likisema kwamba huwapa wanariadha kama hao faida isiyo ya haki.
"Nilivunjika moyo lakini sikukata tamaa," asema kuhusu wakati huo.
"Sikutarajia [mwaka uliosalia wa 2021 ungeenda vizuri sana] baada ya kile kilichotokea lakini ninajivunia kwa mafanikio yote ambayo nimefanya. Ilikuwa vigumu sana.
"Mafanikio yangu yatawapa motisha wanariadha chipukizi kutoka Afrika, na hapa Namibia, kujaribu kufanya wawezavyo na kufanya bidii katika ndoto zao."
Unaweza pia kusoma