Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Afcon 2021: Darubini ndani ya kundi C - Morocco, Ghana, Comoros na Gabon
Michuano ya 33 ya Kombe la Mataifa ya Afrika inaanza nchini Cameroon, Jumapili Januari 9, ikiwa imecheleweshwa kwa mwaka mmoja kutokana na janga la corona.
Hapa, tunaangazia kundi C, ambalo linajumuisha washindi mara nne Ghana , Morocco, Gabon na Comoros
Ratiba
Jumatatu, 10 Januari: Morocco v Ghana, Comoros v Gabon
Ijumaa, 14 Januari: Morocco v Comoros, Gabon v Ghana
Jumanne, 18 Januari: Gabon v Morocco, Ghana v Comoros
Morocco
Mohamed Amine El Amri (Mwandishi wa Habari za Michezo wa Le Matin, Morocco): Chini ya Vahid Halilhodzic, aliyeteuliwa mwaka wa 2019 mara tu baada ya kipigi kingine huko Afcon nchini Misri (kwa kutolewa katika awamu ya 16 bora dhidi ya Benin), Morocco imepitia mabadiliko mengi.
Meneja wa Bosnia amekuja na maamuzi yake, akiongeza vijana wengi kwenye timu na kuwaacha "kikosi cha zamani".
The Atlas Lions wanaweza kutegemea kizazi kipya chenye vipaji sana kinachoongozwa na supastaa wa Paris Saint-Germain Achraf Hakimi.
Wakiwa wamecheza mechi zao zote za kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Morocco - kwa sababu tofauti kutoka kwa uwanja uliobatilishwa hadi mapinduzi ya kijeshi - swali kuu ni jinsi timu hiyo inavyo weza kukabiliana na changamoto.
Ugomvi kati ya Hakim Ziyech na Halilhodzic umesababisha kukosekana kwa winga huyo wa Chelsea, na mashabiki watatumaini kuwa kipaji chake cha kufungua safu ya ulinzi hakitakosekana nchini Cameroon.
Ghana
Ibrahim Ridwan Asante (Ghana Soccernet): Ghana wanatafuta tena ubingwa wa Afrika ambao haujapatikana, wakiwa wamekaribia mara tatu tangu ushindi wao wa 1982 lakini wakaanguka kwenye kilele cha utukufu.
Black Stars walifanya vyema katika mchuano uliopita nchini Misri, na kuondolewa katika awamu ya 16 bora mikononi mwa Tunisia, na Milovan Rajevac, ambaye aliteuliwa tena Septemba, amepewa jukumu la kushinda nchini Cameroon.
Mwaka 2010 Mserbia huyo alikusanya kikosi cha vijana ambacho kilifika fainali lakini wakafungwa 1-0 na Misri. Nahodha wake Andre Ayew na beki Jonathan Mensah ndio walionusurika kikosini tangu miaka 11 iliyopita.
Imani ya Rajevac katika vijana itamfanya atumie huduma za vijana wenye vipaji kutoka Ulaya kama Kamaldeen Sulemana (Rennes), Kudus Mohammed (Ajax), Felix Afena-Gyan (Roma) na Edmund Addo (FC Sheriff).
Comoros
Kassim Oumouri (Mchangiaji wa ORTC): Comoros itacheza awamu ya mwisho ya shindano hilo la kifahari zaidi barani kwa mara ya kwanza katika historia yake fupi. Wanaume wa Amir Abdou wana mengi ya kupata na hakuna cha kupoteza.
Uhasama utaanza kwa mechi dhidi ya Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon. Kwenye karatasi, kila kitu kinawezekana, haswa kwa vile Wacomoro hawana majina makubwa ya kandanda ya Kiafrika. Kutoka Ghana hadi Cameroon, kupitia Misri na Morocco, zote zilizuiliwa na nahodha Nadjim Abdou na wachezaji wenzake.
Huku El Fardou Ben Mohamed akiwa kileleni mwa mchezo wake, Comoro inaweza kushangaza kundi la mauti linaloundwa na Ghana, Morocco na Gabon. Coelacanths wanaweza kucheza kama waharibifu na kumaliza nafasi ya tatu ikiwa wataifunga Gabon, na ushindi utawawezesha kuanza dimba wakijiamini.
Uzoefu wa wachezaji wa kigeni unaweza kuwa mali ambayo haipaswi kupuuzwa. Kuona Coelacanths katika awamu ya 16 itakuwa jambo la kushangaza.
Gabon
Gerauds Wilfried Obangome (Mwandishi wa Habari katika Plusinfos TV): Gabon wamepangwa kama mchezaji wa nje wa kuaminika, angalau kupita hatua ya makundi. Wanaanza dhidi ya Comoro, na kisha wanahitaji kushinda mawiji waili wa soka la Afrika, Ghana na Morocco.
Lengo la kocha Patrice Neveu na timu yake changa ni "kujitolea kwa vyovyote kwa heshima ya taifa" baada ya kukosa mechi za 2019.
Kazi inaweza kuwa mgumu kwa Mfaransa Patrice Neveu, ambaye tayari ametenga sehemu ya umma kwa kuchagua kumuacha Didier Ndong. Kutochaguliwa kwa kiungo wa Yeni Malatyaspor ni uamuzi wa kuhifadhi utulivu wa kikundi.
The Panthers wanaongozwa na mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye anatazamiwa kucheza fainali yake ya tano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ana uhakika wa kuthibitisha baada ya kuvuliwa unahodha wa Arsenal na kuachwa na klabu hiyo ya Ligi ya Premia mwezi Disemba.