Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ralf Rangnick: Jurgen Klopp asema nia ya Manchester United 'sio habari njema kwa timu nyingine'
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kwamba "kwa bahati mbaya mkufunzi mpya anakuja England" iwapo Manchester United inakubali kufanya mkataba na Ralf Rangnick.
Mahasimu hao wa Liverpool wamepanga kumteua Mjerumani mwenye umri wa miaka 63, set to appoint the German, 63, kama meneja wa muda kwa mkataba wa miezi sita.
Klopp ni mmoja wa wakufunzi wenye umri mdogo zaidi waliojifunza kutokana Rangnick na walikabiliana kama mameneja hasimu.
"United watapangwa vizuri katika uwanja," alisema Klopp, mwenye umri 54. "Hiyo sio habari njema kwa timu nyingine."
Rangnick aliweka rekodi katika kujudi za kuinadi ligi ya Ujerumani Bundesliga kwa mara ya kwanza kabla ya kuwa meneja wa Stuttgart, Hannover, Hoffenheim, Schalke na RB Leipzig.
Pia amehudumu kama mkurugenzi wa soka wa kikundi cha klabu za Red Bull na sasa ni meneja wa michezo na maendeleo katika klabu ya Urusi ya Lokomotiv Moscow.
Manchester United wanatafuta maelezo ya mwisho ya uhamisho wa Rangnick , ambayo yatawezesha kumpatia mkataba wa umeneja wa miaka miwili katika Old Trafford mwishoni mwa msimu.
"Tayari ni mwanaume mzuri na mkufunzi mwenye ujuzi wa hali ya juu," Klopp aliongeza. "Ni meneja mwenye uzoefu sana n ani maarufu kwa kuzijenga klabu mbili ambazo hazikuwa popote na kuziwezesha kufanikiwa nchini Ujeumani - Hoffenheim and RB Leipzig.
"Amekwisha fanya kazi nyingi tofauti katika soka, lakini hofu ya kwanza ilikuwa kila mara kuwa mkufunzi, kuwa meneja, na hapo ndipo ujuzi wake bora zaidi ulipo."
Rangnick 'bado ana denia' la Klopp baada ya kunadi Hannover
Ralf Rangnick na Jurgen Klopp walikuwa mameneja mahasimu wakati Schalke ilipokutana na klabu ya Klopp ,Mainz Disemba 2005
Michael Carrick atasalia kuwa kiongozi wa United katika safari yake yaPrimia Ligi dhidi ya Chelsea, na ingawa Rangnick hatakuwepo katika Stamford Bridge, inadhaniwa kuwa atakuwa akisimamia mechi ya Alhamisi ya Primia Ligi akiwa nyumbani dhidi ya Arsenal.
Klopp, ambaye ni meneja wa zamani wa Mainz na Borussia Dortmund boss, alisema: "Kati ya wakufunzi na katika ulimwengu wa soka nchini Ujerumani, anachukuliwa kuwa mkufunzi wa hali ya juu na yuko hivyo. Kokote alikokuwa, alifanya kazi nzuri sana.
"Alianza kama kijana mdogo katika Stuttgart, akifundisha timu ya akiba, na akaendelea kusonga mbele kuanzia pale.
"Tulikabiliana ana kwa ana kwa mara ya kwanza nilipokuwa mkufunzi kijana na alikuwa katika Hannover. Huenda amesahau, lakini walicheza kama mahasimu wetu wiki moja baadaye kwa hiyo aliniita, meneja kijana wa Mainz na akaniuliza maswali.
"Nilikuwa mwenye furaha sana Ralf Rangnick alikuwa kinipa simu, lakini alipata taarifa zote alizohitaji. Halafu waka wakapandishwa daraja (katika mwaka 2002) na hatukupandishwa, kwa hiyo bado ana deni langu!"
Meneja wa Chelsea Mjerumani Thomas Tuchel, 48, alicheza chini ya ukufunzi wa Rangnick katika Ulm na meneja wa Mainz na Borussia Dortmund baada ya Klopp.
"Alinisaidia sana," Tuchel alisema Rangnick. " alikuwa meneja wangu na mmoja watu muhimu kunishawishi kujaribu ni jaribu kwa hiyo alikuwa na ushawishi mkubwa kwetu sote wakati wote. Alituonyesha kuwa sio muhimu kuwafuata watu msalani katika mechi za sokakwasababu hiyo ndio ilikuwa imani.