Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumapili tarehe 29.08.2021:Mbappe, Ronaldo, Kounde, Dalot, Trippier, Edouard, Martine
Mshambuliaji Mreno Cristiano Ronaldo, 36, atakuwa ndiye mchezaji anayelipwa msahara wa juu katika historia ya Primia Ligi atakapo kamilisha uhamisho wake kutoka Juventus kuelekea Manchester United. (Telegraph - subscription required)
Matumaini ya Chelsea ya kusaini mkataba na Jules Kounde kutoka klabu ya Sevilla yamefifia baada ya klabu hiyo ya Uhispania kupandisha garama ya malipo wanayodai kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 hadi pauni milioni 68.5 (Telegraph - subscription required)
Real Madrid imeipatia Paris St-Germain hadi kufikia leo Jumapili iwe imekubali dau lao kwa ajili ya msambuliaji wao Kylian Mbappe, kwani klabu hiyo ya Uhispania haiko tayari kutoa ofa ya zaidi ya euro milioni 190 (£163m) kwa jili ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 22. (Le Parisien - in French)
Manchester United wanapanga kufanya uhamisho wa muda wa mwisho kwa ajili ya kiungo wa nyuma-kulia wa England mwenye umri wa miaka 30- Kieran Trippier, huku Atletico Madrid ikisemekana kudai malipo ya euro milioni (£34.3m) kwa ajili ya mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham. (AS via HITC)
Borussia Dortmund wanamatumaini ya kusaini mkataba na beki Mreno Diogo Dalot kutoka Manchester United iwapo klabu hiyo ya Primia itaweza kupata mchezajiatakayechukua nafasi ya Diego mwenye umri wa miaka 22 . (Sky Sports)Hatahivyo Dalot anasemekana kuwa ameazimia kuendelea kubakia Old Trafford na kupambania nafasi yake katika kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer. (Goal)
Tottenham wameanza juhudi za kumsaka kiungo wa safu ya nyuma-kulia wa Barcelona Emerson Royal, 22, na kumuachilia mlinzi Mivory Serge Aurier mwenye umri wa miaka 28 kutasaidia juhudi zao za kusaini mkataba na Mbrazili huyo . (Telegraph - subscription required)
Juventus wanakamilisha shughuli ya kusaini upya mkataba na mshambuliaji Muitalia Moise Kean ambaye anasaini mkataba wa miaka miwili wa mkopo kutoka klabu ya Everton, kwa sharti la kumnunua kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye alijiunga na Toffees kutoka Italia mwaka 2019. (Sky Sports)
Wolves wanakaribia kukamilisha utaratibu wa kusaini mkataba na mshambuliaji wa Korea Kusini Hwang Hee-chan kutoka klabu ya ujerumani ya RB Leipzig. Klabu kama vile Brighton, West Ham na Atalanta pia zilimtaka Chan mwenye umri wa miaka 25 msimu huu. (Telegraph - subscription required)
Crystal Palace imefanya dau la pauni milioni 15 kwa ajili ya mshambuliaji Mfaransa anayechezea klabu ya Celtic Odsonne Edouard, 23. Palace pia wamefanya mazungumzo na mshambuliaji wa Arsenal Muingereza Eddie Nketiah, 22, huku wakitafuta uwezekano wa uhamisho kwa ajili ya Waingereza Reiss Nelson, 21, na Ademola Lookman wa Arsenal mwenye umri wa miaka 23 anayechezea klabu ya RB Leipzig ,na wakati huo huo wakimsaka winga wa kimataifa wa Ivory Coast kutoka Sassuolo,Jeremie Boga. (Mail)
Kiungo wa kati wa Leicester Muingereza Hamza Choudhury, 23, yuko makini kujiunga na Newcastle kwa mkopo, huku Magpies wakikaribia kusaini mshambuliaji Mmexico Santiago Munoz, 19, kutoka klabu ya Santos Laguna. (Chronicle)
Everton wanataka kusiani mkataba na kiungo wa nyuma-kulia Muingereza Ainsley Maitland-Niles, 23, kwa mkopo kutoka Arsenal. (Sky Sports)
Reading wako katika mazungumzo na Chelsea kuhusu uhamisho kwa ajili ya kiungo wa kati muingereza Danny Drinkwater mwenye umri wa miaka 31. (Reading Chronicle)
Kiungo wa kati Mfaransa Tiemoue Bakayoko, 27, amewasili Italia kwajili ya matibabu kabla ya kujiunga na klabu ya AC Milan kutoka Chelsea kwa mkataba wa miaka miwili wa mkopo wenye kipengele cha kumnunua. (Football Italia)
Mshambuliaji wa Inter Milan Muargentina Lautaro Martinez, 24, amekubali ofay a klabu hiyo ya kuongeza mkataba wake. (Gianluca Di Marzio - in Italian)