Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 22.08.2021: Messi, Rice, Bernardo, Tolisso, Ndombele, Neves, Rodriguez
Manchester United ilikosa kutumia kasi waliopata katika mchuano wao wa ufunguzi dhidi ya Leeds United kwa kutoka sare ya bao moja na southampton uwanjani St Mary's.
Vijana wa Ole Gunnar Solskjaer walionyesha makucha yao katika mechi walioishinda Leeds mabao matano kwa moja lakini leo matokeo yao hayajaridhisha baada ya kulazimishwa kutoka na alama moja pekee .
Katika mechi nyingine ya ligi ya premia iliyosakatwa leo Tottenham imeishinda Wolves bao moja kwa nunge .
David Beckham amefanya mazungumzo na Lionel Messi juu ya kujiunga na Inter Miami wakati mkataba wa mshambuliaji huyo wa Argentina na PSG utakapomalizika mnamo 2023. (Mirror)
Kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 22, hafurahia gharama ya pauni milioni 100 ambayo kilabu imemwekea, ikimfanya asiweze kuondoka katika msimu huu wa joto. (Sunday Telegraph)
AC Milan wanataka kumsajili kiungo wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 27, kwa dau la pauni milioni 45. (Star on Sunday)
Mshambuliaji wa Fiorentina na Serbia Dusan Vlahovic nalengwa sana na Tottenham ikiwa Harry Kane ataondoka msimu huu wa joto. (La Repubblica - in Italian)
Tottenham ilikataa makubaliano ya kubadilishana kiungo wa kati wa Bayern Munich Mfaransa Corentin Tolisso, 27 na nyota wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 24, ambaye angejiunga na miamba hao wa Bundesliga. (Sky Sport Germany - in German)
Ndombele anataka kuhamia Real Madrid, Barcelona au Bayern Munich. (AS - in Spanish)
Mkuu wa uhamisho wa Tottenham, Fabio Paratici amefungua mazungumzo na Juventus juu ya uhamisho wa Ndombele, katika makubaliano ya kubadilishana ambayo yatafanya kiungo wa Marekain Weston McKennie, 22, ajiunge na kilabu hiyo ya London kaskazini(Tuttosport - in Italian)
Everton wamejiunga na Bologna na Eintracht Frankfurt katika harakati za kumsajili mlinzi wa Ufaransa Malang Sarr, 22, kutoka Chelsea. (Gianluca Di Marzo - in Italian)
Manchester United bado wanavutiwa na mchezaji wa Wolves na kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves. (Sunday Express)
Newcastle itafanya mazungumzo na Everton juu ya uhamisho wa kiungo wa Colombia James Rodriguez, 30, kwa ombi la meneja Steve Bruce. (Calcio In Pillole, via Star)
AC Milan wanakaribia kukamilisha mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea Mfaransa Tiemoue Bakayoko, 27. (Calciomercato - in Italian)
Manchester City ingependa kumsaini kiungo chipukizi wa Barcelona na Uhispania Ilaix Moriba, lakini ikiwa tu wangeweza kumsajili mchezaji huyo wa miaka 18 kwa uhamisho wa bure. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Anderlecht wanafanya mazungumzo ya kuafikia makubaliano ya kumsaini kwa mkopo Kiungo wa kati wa Manchester City Liam Delap, 18 (Football Insider)
Mlinzi wa zamani wa Arsenal na Chelsea David Luiz, 34, analengwa na Flamengo. Mbrazil huyo ni mchezaji huru baada ya kuondoka Arsenal mwishoni mwa mkataba wake msimu huu wa joto. (Globo, via Sun)
Southampton wanatumai kumaliza makubaliano ya kumsaini beki wa Torino na Brazil Lyanco, 24. (Mail on Sunday)
Burnley itapambna na Crystal Palace katika kumsaka kiungo wa Watford Muingereza Will Hughes, 26. (Mail on Sunday)
Southampton wanatarajia kumaliza makubaliano ya kumsajili kiungo wa Celtic na Scotland Ryan Christie, 26, kwa gharama ya chini wakati mkataba wake utakapomalizika Januari. (Sun)