Usain Bolt:Raia wa Jamaica ambaye kasi yake iliushangaza ulimwengu

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni wanamichezo ambao uwezo,talanta na rekodi zao zitasalia katika kumbukumbu za historia kwa muda mrefu .Wengine wameshastaafu lakini wenzao bado wapo katika tasnia ya michezo.Wikii hii tunakupakulia safari za wanamichezo wa kipekee ambao wameng'ara na kuacha mifano ya kuigwa katika aina mbali mbali ya michezo.Leo tunamuangazia Usain Bolt anayeshikilia rekodi ya dunia ya mbio za mita 100 na 200 na mtu mwenye kasi Zaidi duniani .

Watu wengi wanajua kuwa Usain Bolt ndiye mwanadamu mwenye kasi zaidi duniani.
Lakini sio watu wengi wanaojua jinsi mwanariadha huyo alivyoanza safari yake kufika kilele cha taaluma yake ,akiusisimua ulimwengu mzima kwa rekodi nyingi alizovunja na matumaini ya watoto wengi waliokuwa wakimtazama ,kumfuatlia na hata kutaka kuwa kama yeye .
Mnamo Mei 31 2008 mwanariadha asiyejulikana wa Jamaica alisajili rekodi yake ya kwanza duniani katika mbio za 100m
Usiku mmoja huko New York, Usain Bolt akiwa na miaka 21 alikuwa chipukizi lakini urefu wake wa kimo uliwazamisha washindani wake walipokuwa wakiinama kuanza mashindano ya mbio za mita 100 .
Pembeni mwake alikuwepo Tyson Gay, bingwa wa ulimwengu aliyetawala katika mbio za 100m na 200m, lakini kilichowashangaza wengi ni wakati Bolt mwenye urefu wa futi sita na nchi 5 alipoanza kuwacha pengo kati yake na wanariadha wenzake bada ya mita 20.

Chanzo cha picha, Getty Images
Miguu yake mirefu, humsaidia kupata kasi ya karibu mita 28 kwa saa na ulimwengu haukujua kabisa kwamba tangia wakati huo hakuna atakayeweza kumshika Bolt .
Wakati alipoongeza kasi na pengo kati yao , mpinzani wake Gay alibaki akiangalia nyayo zake kwa sekunde 9.71. Muda huo baadaye ulirekebishwa hadi 9.72 lakini matokeo hayakubadilika, Bolt alikuwa mtu mwenye kasi zaidi katika historia.
Wiki kadhaa baadaye, Bolt aliteka nyoyo na akili za ulimwengu wote kwenye Olimpiki ya Beijing ambapo alijizolea medali zote za dhahabu. Hakika, hapo ndipo sehemu kuu ya sinema ya Bolt ilianza.
Bolt ambaye alistaafu kutoka riadha ,wakati wake akiwa katika riadha ,alitajwa na wadadisi kama mwanariadha wa kipekee katika kizazi chake .Hakuna aliyewahi kuhudhuria mashindano ambayo Bolt alishiriki ambaye hatakueleza kuhusu kutajwa kwa jina lake au kuonekana kulivyokosa kuwasisimua mashabiki uwanjani.Bolt ambaye sasa ana umri wa miaka 34 ,alijitosa katika mchezo huo,kuandikisha historia na kuach rekodi kadhaa ambazo huenda itachukua muda mrefu kuzivunja .
Safari yake ilianzaje?
Ili kuelewa nakotoka na chimbuko la mtu mwenye kasi zaidi ulimwenguni, lazima uondoke Kingston na uelekee kijijini ambako yote yalianzia .
Kuna wachache tajika ambao wana uwezo wa kupita hata sifa za michezo yao. Babe Ruth wa Baseball, Pele wa soka , Michael Jordan wa mpira wa magongo na Muhammad Ali wa ndondi wote wanakuja akilini unapowafikiria wanamichezo maarufu zaidi duniani . Lakini kukua katika Pigtown, Bauru, Wilmington na Louisville kunahusiana vipi na kipaji Bolt?
Sherwood Content ni Sehemu ya mashambani na ni masaa matatu kutoka mji mkuu na hapa ndiko aliko shangazi yake Bolt ,Lilly . Anaapa kwamba ni chakula alichkua akimpikia Bolt ndico kinachomfanya kuwa na kasi aliokuwa nayo akiwa uwanjani .
Elimu ya michezo ya Bolt ilianzia katika Shule ya Msingi ya Waldensia, mwendo mfupi kutoka kwa nyumba ambayo wazazi wake bado wanaishi.
Mwalimu wake wa zamani, Sheron Seivwright, anasema kwamba kila wakati alikuwa akiwavutia watu wengi . "Sijui wazazi wake walimlisha nini lakini alikuwa na nguvu sana, angeweza kukimbia sana, haraka sana wakati akiwa bado na umri mdogo," anasema.
Wakati wa Alhamisi 'wakati wa michezo', anakumbuka akiangalia Bolt ikishinda mbio dhidi ya watoto wanaomshinda umri . Katika hafla nadra mtu alimshinda , alikuwa hapendi kushindwa.
Anakumbuka: "Alikuwa akilia. Kila wakati analia. Nami ningekuja kumliwaza na kusema" hapana, huwezi kulia. Siku moja utakuwa mwanariadha mkubwa "."
Bolt ambaye ni mshindi wa medali ya Olimpiki mara nane ,baadaye aliamua kubadilisha taalum ili kujiunga na soka lakini mwaka wa 2019 alisalimu amri na kusema misheni yake hiyo imefeli . Aliwahi kufanya mazoezi kwa miezi miwili na klabu ya Australia Central Coast Mariners lakini akaondoka .Baadaye alikataa ofay a klabu ya Malta Valleta b aada ya kushindwa kugharamia malipo yake na aliwahi pia kufanya mazoezi na Stromsgodset ya Norway na miamba wa Ujerumani Borussia Dortmund.
Bolt hakupenda kurauka
Bolt anatambua kuwa jeni zake zina wajibu katika safari yake lakini pia, mazingira na usimamizi wa uwezo wake. Mafanikio yake yalileta ujio mzuri lakini pia ratiba iliyohitaji niadhamu ya hali ya juu .
Aliyekuwa naye wakati wote ni meneja wake mtendaji NJ Walker, rafiki yake mkubwa tangu alipokuwa na umri wa miaka sita.

"Tunaangalia kazi yangu kama bafa kati yake na ulimwengu wote," anasema Walker.
"Nasimamia mambo ya maisha yake. Ninaratibu shughuli zake , kupitia mikataba, kujadili mikataba - kitu pekee ambacho simfanyii ni kusaini mikataba hiyo."
"Kujua kuwa rafiki yako uliyekua naye, ulicheza naye mkiwa wadogo amekuwa na athari kubwa ulimwenguni, amekuwa na mafanikio kama hayo - hatkuwahi kuota vitu kama hivi."
Bolt na maisha ya familia
Mnamo Juni mwaka huu Bolt litangaza kwamba mpenzi wake Kasi Bennett alikuwa amejifungua watoto pacha wa kiume waliopewa majina Thunder Bolt na Saint Leo Bolt.
Bolt, 34, alitangaza Habari hizo kwa wafuasi wake kupitia instagram katika siku iliyokuwa ya kuwasherekea akina baba .

Chanzo cha picha, USAIN BOLT/INSTAGRAM
Kando na pacha hao Bolt aa mtoto mwingine wa kike binti yake Olympia Lightning aliyezaliwa Mei mwaka wa 2020. Mwanariadha mwenye kasi duniani ,ambaye rekodi zake hazijavunjwa ,aliamua kustaafu ili kujishughulisha na biashara zake pamoja na kuwa mzazi wa wanawe,Usain Bolt bila shaka ni jina litakalosalia katika kumbukumbu za historia kwa miaka miwingi ijayo .














