Floyd Mayweather Jr:Alishinda mataji lakini taaluma yake ilikumbwa na utata

J

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni wanamichezo ambao uwezo na rekodi zao zinakumbukwa .Wikii hii ya mashindano ya Olmpiki huko Tokyo Japan tunawaangazia wanamichezo hao leo tunamuangazia bondia Floyd Mayweather Jr ambaye licha ya kushinda mataji ulingoni maisha yake ya taaluma na binafsi yalijaa utata.

bbc

Floyd Joy Mayweather Jr. amestaafu kutoka masumbwi na lakini bado anajishughulisha na mchezo huo njia nyingine mbali mbali

Ni baba wa watoto watano, mkubwa ni Koraun, ana miaka 21, anayefuata ni binti yake Iyanna mwenye miaka 20, Zion kijana wa miaka 19 na binti yake wa mwisho ana miaka 16 anaitwa Jirah.

Ripoti nyingi kuhusu mapigano yake ya ndondi na hata sakata zinazomkumba yapo katika majarida mengi ya michezo ikiwemo BBC sport.Lakini mengi zaidi ukitaka kumjua basi yamo katika kauli zake kwenye mahojiano na vyombo vya habari na nukuu zake ambazo nyingine anapenda kuziweka katika mitandao yake ya kijamii.

Mwaka 2002, alifungiwa kwa miezi sita kutokana na vitendo vyake vya unyanyasaji. Mwaka 2004, alipewa adhabu ya kufanya kazi za jamii kwa masaa 100 na faini ya dola $1000 kwa makosa dhidi ya wanawake. Kuelekea pambano lake dhidi ya Manny Pacquiao, mpenzi wake mwingine wa zamani alimshitaki akitaka amlipe dola $20 million kwa kumdhihaki kwa kumwambia ni mtumiaji wa dawa za kulevya.

Mwaka 2020, mmoja wa wapenzi wake wa zamani alimshtaki kwa unyanyasaji na kumfanya akamatwe na kauchiwa kwa dhamaa ya dola $30,000.

Akiwa ulingoni alitambuliwa kwa makonde yake ya nguvu na akili ya kumkabili mpinzani bila kujali kimo na uwezo wake.

Familia na Maisha yake ya utotoni

Sr

Chanzo cha picha, RingTV

Maelezo ya picha, Mayweather Jr akiwa na baba yake na mwalimu wake wakati huo, Mayweather Sr

Floyd Joy Mayweather Jr. alizaliwa Februari 24, 1977 huko Michigan Marekani katika familia ya wanamasumbwi. Baba yake, Mayweather Sr. alishawahi hata kupambana na bondia mkali, Sugar Ray Leonard.

Baba zake wadogo Jeff na Roger Mayweather, walikuwa mabondia pia wakulipwa, huku mama yake akiwa anaishi katika maisha ya mihangaiko kutokana na athari za matumizi ya dawa za kulevya.

Aliishi na mama yake katika nyumba ndogo ambayo chumba kimoja walilazimika kulala mpaka watu 8 huklo New Jersey. Alikuwa anakuta mabomba ya sindano ya dawa za kulevya na hali ilizidi kuywa mbaya kwa wazazi wake.

Baba yake pia aliwahi kushtakiwa kwa ulanguzi wa dawa za kulevya na kuwekwa ndani. Kwa sababu hiyo akalazimika kulelewa zaidi na bibi yake. Alikuwa ni mtu wa hasira na chuki kwa sababu alihisi kama wazazi wake hawamtendei haki kumlea inavyopaswa. Anasema hasira zake ndizo zilizomuingiza kwenye masumbwi. Aliacha shule huko Ottawa Hills na kuanza kujiendeleza kwenye masumbwi. Mayweather alikuwa anatamani sana kuwa bondia.

Alivyojiingiza kwenye masumbwi

Ingawa haiko wazi hasa lini alijitupa rasmi kwenye masumbwi lakini alikuwa na rekodi nzuri wakati wa mwanzo mwanzo alipoanza kucheza ndondi za ridhaa. Kutokana na aina yake ya kucheza ngumi kwa kujilinda alipewa jina la'pretty boy'.

Mayweather alipigana mapambano 92 ya ngumi za ridhaa, alipoteza manane, na kushinda 84. Alishinda tuzo ya bondia bora 'Golden Gloves' mara tatu, huku akipoteza kwenye nusu fainali ya mashindano ya Olympic ya mwaka 1996 dhidi ya mbulgaria, Serafim Todorov katika maamuzi yaliyokuwa na utata na kuzua gumzo.

Mayweather aliingia kwenye ndondi za kulipwa mwaka huo huo wa 1996 akapigana pambano lake la kwanza la kulipwa dhidi ya Roberto Apodaca na kushinda kilaini.

Aliendelea kuwachapa makonde mpaka mwanzoni mwa mwaka 1998 na pambanano yake mengi alishinda kwa knockout. Uwezo wake ukaanza kuangaliwa na dunia na alipofikisha pambano lake la 14 la kulipwa, baba yake Mayweather akaamua kuwa kocha wake baada ya kutoka gerezani.

Jr

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Toka akiwa kijana, Maywheather alionyesha ishara ya kuwa bondia mkubwa duniani

Ujuzi na uwezo wake ukaongezeka maradufu na ilimchukua miaka miwili ya kucheza ngumi za kulipwa kuweza kutwaa taji la kwanza la dunia la uzito wa WBC Super Featherweight (130 lb) akimtwanga bingwa wa dunia wa uzito huo Genaro Hernandez, mwaka 1998.

Baada ya hapo kila aliyekuja alimtwanga wakiwemo wakali kama Carlos Rico, Justin Juuko, Carlos Gerena, Emanuel Burton, Oscar De la Hoya, Shane Mosley, Manny Pacquiao, Conor McGregor na Victor Ortiz;

Katika wote Mayweather anasema hatasahau pambano lililomtoa jasho kabisa dhidi ya Diego Corrales. Katika miaka yote kwa mara ya kwanza Mayweather alidondoshwa chini akiwa ulingoni dhidi ya Carlos Hernandez ilikuwa Mei 26, 2001 katia raundi ya 6 ingawa pambano hilo lilimalizika kwa Mayweather kushinda.

Rekodi , ushindi na pato

Manny Pacquiao

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mayweather akitangwaza kushinda dhidi ya Manny Pacquiao kwenye pambano lililoweka rekodi ya pesa la mwaka 2015

Mayweather ana rekodi kadhaa katika miaka yake zaidi ya 20 aliyocheza ndondi, akicheza mapambano 50 ya kulipwa na kushinda yote. Hajapigwa pambano hata moja, akishinda mapambano 27 kwa KO.

Kwa sababu ya uwezo wake, Mapambanao mengi aliyoshiriki yalimuingizia pesa nyingi. Kwa mfano alivyomtwanga Manny Pacquiao Mei 4, 2015 alijipatia dola 180 million. Alishawahi kustaafu awali lakini Agosti 2017 akalazimika kurejea ulingoni kuzichapa na Conor McGregor. Alishinda mbele ya watazamaji 14,623 katika pambano lililomuingizia zaidi ya dola za kimarekani $300 million.

Floyd Mayweather anajulikana hasa wa jina la 'Money' kwa maana ya pesa, na si haba ni miongoni mwa wanamichezo matajiri ulimwenguni, Kwa mujibu wa mtandano wa wealthygorrilla.com, ulielezwa mwanamasumbwi huyo kuwa na utajiri unaofikia dola $450 million mwaka 2021,Ingawa Mayweather mwenyewe anakana hilo akisema utajiri wake unafikia dola $1.2 billion.

floyd

Kwa mujibu wa Forbes, Mayweather aliiingiza zawadi za ushindi kwenye mapambano yake zenye thamani ya dola $1 billion. Huku akitajwa na jarida hilo la Forbes kama mwanamichezo aliyekuwa analipwa Zaidi kuliko yoyote duniani katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo 2012, 2013 na 2014

Maisha tata ya Mayweather Jr nje ya Ulingo

Floyd Mayweather Jr

Chanzo cha picha, The Province

Maelezo ya picha, Floyd Mayweather Jr amekuwa akikutwa na makosa mengi hasa dhidi ya wanawake

Floyd Mayweather Jr amesajili ushindi katika ndondi lakini maisha yake binafsi yako tofauti kabisa,hayalingani na rekodi zake ulingoni . Mayweather amekuwa akitajwa kama mwanamichezo mtata, akisema maisha yake ya utotoni yamechangia alivyo leo.