Harry Kane, Patrick Schick, Grealish na Pogba: Ni mchezaji gani atakayevunja rekodi ya dirisha la uhamisho?

Nahodha wa timu ya England Harry kane

Macho yote huenda yameelekezwa katika kilele cha Euro 2020, lakini huku msimu mpya ukiwa umbali wa mwezi mmoja pekee, klabu zipo katika harakati za kuwasajili wachezaji wap

Manchester United ilianza kwa kumsajili Jadon Sancho kwa uhamisho wa dau la £73m, lakini je ni mchezaji gani mwengine ambaye anahamia klabu nyengine? Je nyota wa Euro atahamia katika ligi ya premia?

BBC Sport inatazama jinsi dirisha hili la uhamisho litakavyokuwa

Je ni wachezaji gani watakaovunja rekodi za uhamisho?

Sio kandarasi nyingi msimu huu zitakazovunja rekodi wa uhamisho wa Jadon Sancho kujiunga na na Man United

Wachezaji wawili ambao huenda wakavutia kiasi kikubwa cha fedha katika uhamisho wao ni mshambuliaji wa England Harry Kane na Jack Grealish wote wakinyatiwa na Manchester City.

Kane, 27, ameweka wazi kwamba anataka kuondoka katika klabu ya Tottenham ambayo haijakubali kumwachilia mchezaji ambaye ana kandarasi ya miaka mitatu iliosalia.

Ukweli ni kwamba klabu hiyo ilimwambia mkufunzi wake mpya Nuno Esporito Santos kwamba inataraji kwamba nahodha huyo wa klabu ya England atasalia.

Aston Villa nayo inatumia fursa yake ya kumzuia kiungo wake wa kati Grealish ,25, lakini ni watu wachache wanaotarajia kwamba watafaulu.

Imekataliwa na washikadau wote lakini kuna uvumi kwamba makubaliano ya Graelish kuichezea Man City msimu ujao yameafikiwa.

Beki wa kati wa England Ben White , 23, huenda akajiunga na Arsenal huku Brighton ikitarajiwa kupata malipo mazuri hususan baada ya kumuongezea mkataba msimu uliokwisha.

West Ham imeweka wazi kwamba haipo tayari kumuuza kiungo wa kati wa England 22, Declan Rice lakini hiyo haimaanishi kwamba haitamuuza.

Na iwapo West Ham huenda wakamkosa Rice , Je leeds haipo katika hali kama hiyo inapokaribia kumpoteza kiungo wao wa kati wa England Kalvin Phillips, 25, ambaye pia anaendelea vyema katika michuano ya Euro zaidi ya kazi anayofanya katika klabu yake.?

Baada ya kukosa Michuano ya Euro kutokana na ukosefu wa kushiriki katika mechi , kiungo wa kati Harry Winks , 25, huenda akaondoka klabu ya Tottenham.

Na iwapo Kane na Grealish watawasili katika klabu ya Manchester City , kutakuwa na wachezaji ambao wataondoka katika klabu ya City huku hatma ya mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus ,24, kiungo wa kati wa Portugal Bernardo Silva ,26, zikiwa hazijulikani.

Vilevile kumekuwa na uvumi kuhusu kiungo wa kati wa wa Man United na Ufaransa Paul Pogba tangu alipojiunga na klabu hiyo ya Old Trafford 2016. Kiungo huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28 amefanya mazungumzo na United kuhusu kuongeza kandarasi yake inayokamilika 2022.

Iwapo hatotia saini kandarasi mpya , United huenda ikampoteza kama mchezaji huru chini ya kipindi cha miezi kumi na mbili au kujaribu kumuuza katika soko lililo na shinikizo kuu kwa chini ya £89m walizolipa ili kumsajili.

Lakini iwapo atatia saini kandarasi mpya , huenda akaongezewa mshahara wakati ambapo wengi wanahoji iwapo anahitaji kuongezwa mshahara huo.

Wakati huohuo, United imewasiliana na Real Madrid kuhusu beki na mshindi wa kombe la dunia na Ufaransa Rphael Varane.

Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 inakamilika mwisho wa msimu ujao na kuna wasiwasi wa iwapo ataongezewa kandarasi ambayo itaafikia mahitaji yake , huku Real ikiaminika kutaka kumuuza kwa £50m.

Mbali na Ligi ya Premia , Lionel Messi, 34, anatarajiwa kusalia katika klabu yake Barcelona, licha ya kuwa mchezaji huru baada ya kandarasi yake kukamilika.

Mazungumzo kuhusu Christiano Ronaldo kutaka kurudi katika klabu ya Man United yanaendelea , lakini itagharimu kitita kikubwa cha fedha , ili kumleta mchezaji huyo wa Portugal katika uwanja wa Old Trafford , mchezaji ambaye anaondoka Juventus mwaka mmoja kabla ya kandarasi yake kukamilika.

Je ni klabu ipi yenye fedha?

Manchester City na Paris St-Germain zina uwezo wa kufanya usajili mkubwa kutiokana na hali yao ya kifedha ambayo imewalinda dhidi ya janga la corona.

Kwa wengine , ni swali la kutumia fedha vizivyo .

Hatua hiyo inaweza kufanyika kupitia ufadhili , kama Man United ilivyofanya , kuuza hisa, kama walivyofanya Juventus Jumatano iliopita , kuomba mkopo ama kuuza mali yake , hatua inayomaanisha kuuza wachezaji, ardhi ama nyumba.

Je ni nyota yupi wa michuano ya Euro2020 atahamia ligi ya Premia

Patrick Shick

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni msemo maarufu kwamba klabu kutokana na mchezo wao mzuri pekee katika michuano mikubwa.

Jambo hilo hufanyikaa hatahivyo na kuna wachezaji wenye talanta wanaotarajiwa kufuatiliwa.

Jinsi Tomas Soucek na Vladimir Coufal walivyoisaidia West Ham msimu uliopita na sifa iliowacha timu ya Czech katika michuano ya Euro 2020 kwa kufika robo fainali - usishangae iwapo baadhi ya wachezaji wake watasajiliwa katika ligi ya premia.

Mshambuliaji Patrik Schick, 25, amesalia na miezi 12 kabla ya kandarasi yake kukamilika katika klabu ya Bayern Leverkusen - lakini walishindwa kufuzu katika kombe la klabu bingwa Ulaya msimu ujao hivyobasi huenda klabu hiyo ikasubiri ofa.

Winga wa Ubelgiji Jeremy Doku ,19, alivutia macho ya wengi katika robo fainali ambapo timu hiyo ilipoteza kwa Itali.

Baada ya kusajiliwa na klabu ya Ufaransa Rennes kutoka Anderlecht mwaka uliopita ana kandarasi ya hadi 2025.

Kuendelea kwa Itali katika michuano hiyo kutasaidia katika wachezaji wake kusajiliwa na timu mbalimbali - ijapokuwa mchezaji mmoja ameburudisha , beki winga wa Roma Leonardo Spinazzola 28, anatarajiwa kukaa nje kutokana na jeraha alilopata la kifundo cha mguu dhidi ya Ubelgiji.

Mkataba wake katika klabu ya Roma unaendelea hadi 2024.

Kiungo wa kati wa Sassuolo Manuel Locatelli ,23, ambaye amefunga magoli mawili kufikia sasa katika michuano hiyo amehusishwa na uhamisho wa Juventus na Arsenal.

Manuel Locatelli

Chanzo cha picha, AFP

Footer - Blue