Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 14.06.2021: Coutinho, Cornet, Kane, Bellingham, Silva, Lingard, Fekir, Buffon
Klabu ya Leicester City imepanga kumsajili kiungo wa Barcelona Philippe Coutinho (29), ingawa bado haijapeleka ofa rasmi, klabu hiyo iko kwenye mazugumzo ya kumnasa Mbrazili huyo ikiwezekana kwa ada ya £17m au kwa mkopo. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Klabu ya Leeds United inamtaka beki wa kushoto wa Lyon, Maxwel Cornet, (24) lakini dau walilotajiwa la £20m kwa ajili ya kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, linawafanya kusita. (Sun)
Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti amewaarifu mabosi wa klabu hiyo kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, mjerumani Timo Werner (25). (Fichajes, via Express)
Kiungo wa kihispania, Juan Mata, 33, atalazimika kuchukua mshahara kiduchu wa £70,000 kwa wiki kama anataka kuendelea kusalia Manchester United baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa mwezi huu. (Star)
Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta yuko tayari kumuuza mlinda mlango, raia wa Ujerumani Bernd Leno (29), msimu huu kama atapatikana mbadala wake. (Mirror)
Chelsea imeongeza dau kwa ajili ya kumnasa mlinzi wa Inter Milan, raia wa Morocco Achraf Hakimi, ikiwemo kitita taslimu cha £43m pamoja na kumtoa nyota wa kimataifa wa Italia Emerson Palmieri (26). (Corriere dello Sport, via Express)
Mwenyekiti wa Klabu ya Tottenham Daniel Levy amesema atafanya 'kile kilicho sahihi kwa klabu' kuhusu masuala ya usajili, ikiwemo mustakabali wa mshambuliaji Harry Kane, aliyeonyesha nia ya kutimka msimu huu. (Goal)
Liverpool inaongoza mbio za kuwania saini ya beki wa Juventus, Cristian Romero raia wa Argentina, ambaye awali alihusishwa na mipango ya kumtimkia Manchester United, baada ya kuonyesha kiwango kizuri akichezea Atalanta kwa mkopo. (Calciomercato - via Team Talk)
Mlinda mlango wa Hispania David de Gea, 30, inaelezwa kwamba hajui hatma yake ndani ya Manchester United wakati huu akijiandaa kufanya mazungumzo na kocha wa mashetani hao wekundu Ole Gunnar Solskjaer kuhusu mustakabali wake ndani ya Old Trafford. (Mirror)
Southampton na West Ham ni vilabu vya hivi karibuni kutoka ligi kuu ya England kuhusishwa na mipango ya kumsajili mshambuliaji wa Boavista Alberth Elis (25), huku vilabu vya Brighton na Watford awali vilionyesha pia nia yao ya kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa Honduras. (A Bola - in Portuguese)
Klabu ya Borussia Dortmund itatumia kipengele maalumu kuhuisha mkataba wa Jude Bellingham atakapotimiza miaka 18 baadae mwezi huu, ili kiungo huyo wa England asalie katika klabu hiyo ya Bundesliga mpaka mwaka 2025. (Bild, via Sun)
Arsenal wanamuwania kiungo mfaransa, Nabil Fekir kutoka Real Betis, lakini ofa ya washika bunduki hao haifikii kiwango wanachohitaji klabu hiyo ya La Liga kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 27. (AS - in Spanish)
Crystal Palace inajiandaa kupeleka ofa ya £15 kwa ajili ya kiungo wa kiingereza Conor Gallagher (21) kutoka Chelsea, ambaye anataka kusalia Stamford Bridge baada ya msimu uliopita kuonyesha kiwango kizuri akiwa West Brom kwa mkopo. (Sun)
West Ham, Southampton na AC Milan zinapambana kumsajili mlinzi wa Barcelona Junior Firpo, (24) raia wa Dominica, huku klabu hiyo ya Catalan ikigoma kumuuza kwenye klabu za ligi kuu England, badala yake ikitaka kumpeleka Milan kwa mkopo pakiwa na fursa ya kumsajili baadae moja kwa moja. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Kiungo wa England, Jesse Lingard, 28, ameimwmabia meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kwamba anataka kusalia kwa mashetani hao wekundu, baada ya kuwa na wakati mzuri msimu uliopita aikiwa na West Ham kwa mkopo. (Sun)
Mlinda mlango wa Juventus, aliyenyakuwa pia kombe la dunia akiwa na Italia, Gianluigi Buffon, 43, anajiandaa kurejea Parma, ya Serea B, ikiwa ni miaka 20 tangu aondoke kwenye klabu hiyo. (Sky Italia - in Italian)
Kiungo wa Tottenham, mfaransa Moussa Sissoko (31) anawaniwa na klabu ya Napoli inayoshiriki ligi kuu ya Italia, Serie A. (Sky Italia - via Team Talk)
Meneja wa Norwich City Daniel Farke anataka kumsajili kiungo wa Bournemouth raia wa Denmark, Philip Billing (25), ambaye anataka kuondoka baada ya kabu hiyo kushindwa kupanda daraja kucheza ligi kuu ya England. (Mirror)
Kiungo wa Bernardo Silva (26) anataka kutimka Manchester City, huku vilabu vya Barcelona na Atletico Madrid vikionyesha nia ya kumtaka nyota huyo wa kimataifa wa Ureno. (Duncan Castles on Twitter)
Leeds United inahusishwa na mpango wa kumsajili mlinzi wa kushoto wa Rangers, raia wa Croatia Borna Barisic (28). (Football Insider)
Mlinzi wa Juventus, raia wa Romania, Radu Dragusin anawaniwa na klabu ya Crystal Palace, ambayo tayari imeshapeleka ofa kwa ajili ya kinda huyo mwenye umri wa miaka 19. (Calciomercato - in Italian)