Tetesi za soka Ulaya Jumapili 13.06.2021: Marcelo, Gonzalez, Sancho, Van de Beek, Trippier, Lukaku, Dembele

Klabu za Everton na Leeds United zinamuwania beki wa kushoto wa Real Madrid, Marcelo, Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 33, ambaye hayuko kwenye mipango ya kocha wa Madrid, Carlo Ancelotti. (Sunday Mirror)

Bournemouth imejaribu kwa mara nyingine kumsajili gwiji la zamani la Arsenal kama Kocha wao mpya, walijaribu pia kumnasa mfaransa huyo (44), mwezi Februari. (Sunday Mirror)

Leicester City inungana na vilabu vya Liverpool, Chelsea na Tottenham katika mbio za kumsajili mshambuliaji raia wa Zambia, anayecheze RB Salzburg, Patson Daka (22). (Sunday Express)

Tottenham inapigana vikumbo na klabu ya Fiorentina kumuwania mshambuliaji wa Muargentina wa klabu ya Stuttgart, Nico Gonzalez, (23), tayari klabu hiyo ya Fiorentina ya Seria A, imeshatenga dau la £21.5m. (Sky Italia - in Italian)

Kocha mpya wa Celtic, Ange Postecoglou anamuwania kipa wa Brighton, Mat Ryan, ambaye aliwahi kumfundisha akiwa na timu ya taifa ya Australia. Klabu ya Arsenal, ambayo Ryan ameichezea kwa mkpo msimu uliomalizka, inamtaka pia mlinda mlango huyo. (Sky Sports)

Manchester United inashughulikia uhamisho wa kiungo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 21, Jadon Sancho ikiwemo marupurupu, baada ya klabu yake ya Borussia Dortmund kukataa ofa ya kwanza kutoka Man Utd. Klabu hiyo ya Ligi ya Bundasliga inataka kitita cha £86m kumuachia nyota huyo. (Sunday Times, subscription required)

Arsenal imewasiliana na Manchester United kuhusu uhamisho wa kiungo wa Kidachi mwenye umri wa miaka 24, Donny van de Beek. (90min)

Atletico Madrid imeiambia Manchester United kwamba Kieran Trippier ana thamani ya £30mil. Bosi wa Manchester Utd, Ole Gunnar Solskjaer anamtaka beki huyo (30), mlinzi huyo wa kulia wa England ili kumpa changamoto ya ushindani, Aaron Wan Bissaka. (Sunday Mirror)

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amemuweka sokoni mshambuliaji mfaransa, Anthony Martial, 25, kwa sababu ya utukutu, huku Klabu ya Real Madrid ikihusishwa kumsaka. (Transfer Window Podcast, via Sunday Express)

Wakati Trippier akitaka kurejea ligi kuu ya England, kocha wa Atletico Diego Simeone hana mpango wa kumuuza mlinzi huyo kwa sasa labda mwakani. (Daily Star Sunday)

Mshambuliaji wa Ubelgiji Romeu Lukaku amepuuza taarifa zozote za kumuhusisha kurejea Chelsea msimu huu, akisisitiza ana furaha Inter Milan. (HLN, via Mail on Sunday)

Burnley inajaribu kutaka kumrejesha England, mlinzi Ashley Young, kwa mkataba wa mwaka mmoja. Young, ambaye awali alihusishwa kurejea Watford, ameshapewa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja na klabu yake, mabingwa wa Italia, Inter Milan. (Sunday Mirror)

Manchester City imesitisha kwa muda mipango yake ya kumsajili beki wa kushoto mwenye umri wa miaka 18, Nuno Mendes kutoka Sporting Lisbon mpaka baada ya michuano ya Euro, ikiiacha Real Madrid ikijaribu bahati yake kwa mreno huyo. (Sunday Mirror)

Barcelona itamfahamisha winga wa Ufaransa, Ousmane Dembele (24), kuchagua mawili kusajili mkataba mpya ama kuondoka klabuni hapo. (ESPN)

Kocha mpya wa Wolves' Bruno Lage amefahamishwa kwamba kiungo wa kireno, Ruben Neves, 24, na mshambuliaji wa Kihispania, Adama Traore (25) wako sokoni ili kupata fedha za kuboresha kikosi hicho. (90min)

Barcelona inajiandaa kupeleka ofa kwa kiungo wa kihispania, Ilaix Moriba (18), baada ya kuhusishwa na usajili wake hapo awali, lakini pia anafuatiliwa na vilabu vya Manchester City, Chelsea na Manchester United. (Marca)

Everton inamtaka mlinda mlango wa Kibrazili, Neto (31) kutoka Barcelona. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Leeds United imefanya mazungumzo ya awali na Club Bruges kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji wa kidachi, Noa Lang (21). (Football Insider)

Mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe, 22, ameleta sintofahamu mpya kuhusu hatma yake katika klabu ya Paris St-Germain, baada ya kukiri kuwa hajui kama klabu hiyo ni mahala sahihi kwake. (France Football, via Mail on Sunday)

Winga wa Ufaransa, Kingsley Coman, 24, alitaka apewe mshahara unaolingana na nyota mwenzake wa Bayern Munich, Robert Lewandowski wakati huo anafikiria kusaini mkataba mpya na wakali hao wa Bundesliga. (Marca)

Coman hakuwa anapendezwa na mshahara kiduchu aliokuwa analipwa na Bayern akaamua kutimka. (Sky Germany - in German)

Leeds United inajaribu kuipiku Norwich City katika mpango wake wa kumsajili mlinda mlango wa Southampton, Angus Gunn, baaada ya ada ya uhamisho wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 kufikiwa muafaka. (Football Insider)

Mahasimu Bristol City, Cardiff City na Swansea City wameonyesha nia ya kumsajili kiungo aliye huru, Matty James, 29, ambaye anaondoka Leicester City msimu huu, baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka tisa. (Mail)

Barcelona wana uhakika wa kukamilisha mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kidachi, Memphis Depay (27), ambaye mkataba wake na Lyon, unamalizika wiki ijayo. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Barca pia inajiandaa kumsajili mshambuliaji wa Argentina, Lautaro Martinez (23), baada ya kusitisha mazungumzo yake ya mkataba mpya na klabu yake ya Inter Milan. (Sport - in Spanish)

Mlinzi wa Romania aliyeitumikia muda mrefu klabu ya Lazio Stefan Radu (34) anaweza kumfuata kocha Simone Inzaghi aliyetimkia Inter Milan, na ambaye amegoma kumuongezea mkataba mpya kusalia San Siro mlinzi wa kiserbia, Aleksandar Kolarov'. (Calciomercato - in Italian)