Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 12.06.2021: Neuhaus, Fonseca, White, Ramos, Lewandowski, Saul, Bissouma

Chanzo cha picha, EPA
Winga wa England Jadon Sancho, 21, atakuwa ndiye mchezaji wa pili atakayelipwa zaidi katika Manchester United, nyuma ya mlinda lango David de Gea, iwapo atakamilisha uhamisho wake kutoka Borussia Dortmund msimu huu. (Mail)
Meneja wa zamani Roma Paulo Fonseca amekubali kimsingi kanuni ya mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuifunza timu ya Tottenham. (Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool wako katika mazungumzo na Borussia Monchengladbach kwa ajili ya kusaini mktataba na kiungo wa kati Mjerumani Florian Neuhaus, 24. (Sport1 - in German)
Arsenal wanajiandaa kwa ajili ya hatua ya kumchukua kiungo wa safu ya kati-nyuma wa Brighton na England Ben White, mwenye umri wa miaka 23. (Athletic)

The Gunners pia wanamfuatilia kwa karibu kiungo wa kati wa Italia Manuel Locatelli , mwenye umri wa miaka 23, baada ya kucheza vyema katika mchezo na Sassuolo. (Sky Sport Italia, via Metro)
Chelsea wanamtaka kiungo wa kati wa Atletico Madrid Saul Niguez, 26, lakini Manchester United na Juventus zimesalia kuwa ndio timu ambazo mchezaji huyo anazipendelea zaidi. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Chanzo cha picha, EPA
Sevilla wamempatia ofa kiungo wao wa safu ya kati-nyuma Muhispania Sergio Ramos, 35, ya mkataba wa miaka mitano. Mkataba wa Ramos katika Real Madrid unaisha msimu huu. (esRadio - in Spanish)
Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 32, yuko huru kuondoka Bayern Munich. (AS - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Everton wanaangalia uwezekano wa kusaini upya mkataba na Mcroasia Nikola Vlasic, 23, anayecheza katika safu ya mashambulizi kutoka CSKA Moscow - miaka miwili baada ya kumuuza. (Star)
Beki wa wa England Danny Rose, 30, anakaribia kujiunga na Watford baada ya kuondoka Tottenham. (Watford Observer)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa safu ya kati-nyuma wa Tottenham na Ivory Coast Serge Aurier, 28, amekubaliana kuhusu masharti ya kibinafsi na klanu ya Paris St-Germain. (Football Insider)
Mlinda lango wa Italia Gianluigi Donnarumma, 22, anakaribia kukamilisha mkataba huru wa uhamisho kwa Paris St-Germain. Ataondoka AC Milan msimu huu wakati mkataba wake utakapokwisha. (Calciomercato - in Italian)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkataba wa kiungo wa kati wa England Jude Bellingham utaongezwa katika Dortmund utaongezwa mara moja kwa miaka miwili zaidi hadi 2025 atakapotimiza umri wa miaka 18 baadaye mwezi huu. (Bild - in German)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wameanzisha mazungumzo na mlinzi wa Uskochi Kieran Tierney, 24, juu ya kurefushwa kwa mkataba wale. (Football.London)
Burnley wameweka dau la pauni milioni 12 kwa ajili ya mlinzi wa timu ya Stoke na Jamuhuru ya Ireland Nathan Collins, mwenye umri wa miaka 20. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal watazidisha nia yao kumchukua kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma, 24,msimu huu. (90min)
Besiktas wanataka kusaini mkataba na mshambuliaji wa Sevilla na Uholanzi Luuk de Jong, 30. (AS - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Fulham wamekataa dau la pauni milioni 16 kutoka kwa klabu ya Urusi ya Dynamo Moscow kwa ajili ya mshambuliaji Mserbia Aleksandar Mitrovic, 26. (Sun)
Barcelona walifanya mkataba na meneja Mjerumani Joachim Low mapema mwaka huu kabla ya kuthibitisha kuwa Ronald Koeman ataendelea kuwa meneja wao. (Bild via Marca - in Spanish)












