Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 08.06.2021: Grealish, Sancho, Ronaldo, Jesus, Haaland, Edouard
Manchester United wanakaribia kufikia mkataba wa kumsajili Jadon Sancho, 21, kutoka Borussia Dortmund baada ya bei ya winga huyo wa Uingereza kushuka hadi £80m. (Times)
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anataka kumsaini kiungo wa kati wa Villa na England Jack Grealish, 25, msimu huu. (ESPN)
Mshambuliaji wa Ureno Ronaldo, 36, anaelekeza darubini yake kwengine licha ya kufanya mazungumzo na Juventus kuhusu hatma yake katika klabu hiyo. (ESPN)
Endapo Ronaldo atahama Juve, Mbrazil Gabriel Jesus ,24, wa Manchester City anapigiwa upatu kuongoza katika orodha ya wachezaji watakaochukua nafasi yake. Wengine ni mshambuliaji wa Fiorentina na Serbia, Dusan Vlahovic, 21, na Muargentina Mauro Icardi, 28, wa Paris St-Germainy. (Gazzetta dello Sport - kwa Kitaliano)
Everton wamemhoji kocha wa zamani wa Wolves Nuno Espirito Santo, 47, kuhusu uwezekano wa kumrithi Carlo Ancelotti kama meneja wa klabu hiyo baada ya Mtaliano huyo kujiunga tena na Real Madrid. (Football Insider)
Chelsea wameongeza juhudi za kumsaka mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland kutoka Borussia Dortmund,"wanaamini" watafanikiwa kumpata nyota huyo , kwa mujibu wa mshambuliaji wa zamani wa Ligi ya Primia Mjerumani mwenzake Jan Aage Fjortoft. (Mail)
Atalanta wameweka bei ya £52m kumuuza mlinzi wa Argentina Cristian Romero. Kiungo huyo aliye na umri wa miaka 23- amehusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United. (Tuttosport - kwa Kitaliano)
Leicester wamekubali uhamisho wa pauni milioni 15 na Celtic kwa mshambuliaji wa Ufaransa Odsonne Edouard, 23. (Sun)
Newcastle wanataka kumenyana na Southampton katika usajili wa kiungo wa kati wa Leicester Muingereza Hamza Choudhury, 23. (Football Insider)
Kocha wa Fulham Scott Parker huenda akaondoka klabu hiyo ili kuwa meneja wa Bournemouth. (Talksport)
West Ham na Aston Villa wanataka kumsajili mshambuliaji wa Burnley Chris Wood, huku Everton wakimnyatia kiungo wa kimataifa wa New Zealand wakati wanasupobiri uteuzi wa meneja mpya. (Mirror)
West Ham wamefikia mkataba wa kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Mfaransa Pierre Ekwah,19. (Sky Sports)
Aston Villa wanapigiwa upatu kumsaini mlinzi wa kati Josh Feeney,16, kutoka Fleetwood msimu huu wa joto, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Manchester United. (Mail)