Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 18.04.2021: Mourinho, Pogba, Sterling, Traore, Varane, Abraham, Loftus-Cheek

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba anataka kulipwa euro 500,000-kwa-wiki kusaini mkataba mpya na Manchester United, huku Real Madrid, Paris St-Germain na Juventus wakipewa masharti hayo ikiwa wanataka kumsajili nyota huyo aliye na umri wa miaka 28. (Star on Sunday)

Chelsea itamenyana na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumsajili mchezaji wa safu ya kati na nyuma wa Real Madrid na Ufaransa Raphael Varane, 27. (Bild journalist Christian Falk on Twitter)

Tetesi "zimezidi kuongezeka" huko Tottenham kwamba meneja Jose Mourinho hatakuwepo kwenye klabu msimu ujao, Spurs ikijitahidi kupata nafasi ya Ligi ya Mabingwa 2021-22. (Football London)

Wolves wanataka kumuuza winga wa Uhispania Adama Traore ilikuchangisha fedha za kumsajili mchezaji mpya na £30m huenda ikatosha kufanikisha mpango wa usajili wa klabu hiyo . (Football Insider)

Mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling, 26,kwa mra nyingine tena ananyatiwa na Real Madrid, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa England akikakamua kuwa katika kikosi cha kwanza cha soka wiki za hivi karibuni. (Star on Sunday)

Tottenham wanaendelea kumfuatilia mchezaji Emerson,22, wa Brazil, ambaye yuko Real Betis kwa mkopo kutoka Barcelona. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Liverpool Georginio Wijnaldum, 30, anapanga kujiunga na Barcelona msimu huu wa joto kwasababu anataka kucheza pamoja na Lionel Messina mwenzake wa Uholanzi Memphis Depay. (Sunday Mirror)

Aston Villa na Crystal Palace wanataka kusaini kiungo wakati wa Chelsea na England Ruben Loftus-Cheek,25, ambaye yuko Fulham kwa mkopo . (Teamtalk)

AC Milan wameiambia wazi Chelsea kwamba wana mpango wa kubadili mkataba wa mkopo wa mlinzi wa England Fikayo Tomori.23, kuwa wa kudumu. (Football Insider)

Hatma ya mshambuliaji wa England Tammy Abraham,23, katika klabu ya Chelsea iko mashakani baada ya meneja Thomas Tuchel kumuacha nyota huyo katika kikosi chake nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester City. (Mail on Sunday)

Leeds United wanataka kumnunua mchezaji wa safu ya kushoto na nyuma wa Argentina Nicolas Tagliafico, ambaye kandarasi yake klabu ya Ajax inaendelea hadi mwaka 2023. (Sunday Mirror)

Leeds kwa pia wanajaribu kumsajili kwa mara ya tatu winga wa Rangers Muingereza Ryan Kent, 24, na wako tayari kulipa £15m. (Sun on Sunday)

West Ham wameongeza juhudi za kumsaka mshambuliaji wa Sparta Prague Adam Hlozek,18, huku klabu zingine pia zikimng'ang'ania mchezaji huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech. (90 Min)