Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 22.07.2020: Henderson, Aubameyang, Cavani, Soucek, Bruce, Hojbjerg

Samatta

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Aston Villa Mtanzania, Mbwana Samatta

Mshambuliaji wa Aston Villa raia wa Tanzania Mbwana Samatta, 27, huenda akaelekea Fenerbahce baada ya kushindwa kuiridhisha Villa Park tangu alipojiuga nao Januari. (Takvim via Sport Witness)

Chelsea imejitayarisha kutoa ofa kwa mlinda lango mwingereza Dean Henderson, 23, ya pauni 170,000 kwa wiki ambaye sasa hivi yuko Sheffield United kwa mkopo , kujaribu kumshawishi kujiunga nao kutoka Manchester United. (Manchester Evening News)

Henderson atatafuta kwa kila namna kuondoka tena kwa mkopo labda tu apate hakikisho kutoka Manchester United kwamba atapata fursa ya kushindana na mlinda lango wa Uhispania David de Gea, 29, awe chaguo la kwanza. (Times - subscription required)

David de Gea

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mlinda lango wa Manchester United David de Gea

Chelsea pia itajitahidi kusaini mkataba na mlinda lango wa Barcelona na Ujerumani Marc-Andre ter Stegen, 28, na iko tayari kutoa ofa kwa mlinda lango wa kimataifa Kepa Arrizabalaga, 25, kama sehemu ya makubaliano yoyote yale. (Mundo Deportivo, via Mail)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ana uhakika kwamba mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31, atasaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Independent)

Pierre-Emerick Aubameyang

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ana uhakika kwamba Pierre-Emerick Aubameyang atasaisini mkataba mpya

Everton ina nia ya kumsajili kiungo wa kati raia wa Denmark mchezaji wa Southampton Pierre-Emile Hojbjerg, 24, lakini ameiarifu timu ya Toffees kwamba angependelea zaidi kujiunga na Tottenham. (Liverpool Echo)

Mlinda lango wa Paris St-Germain Alphonse Areola, 27, ambaye yuko kwa mkopo Real Madrid, huenda akawa njiani kuelekea klabu ya Uingereza baada ya mchezaji huyo raia wa Ufaransa kununua nyumba ya familia yake mjini London. (Marca)

Mlinda lango wa Paris St-Germain Alphonse Areola

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mlinda lango wa Paris St-Germain Alphonse Areola yuko kwa mkopo Real Madrid

Kocha wa Newcastle United Steve Bruce ataendelea na kazi yake ikiwa Henry Mauriss, mpinzani wa Saudi Arabia ambayo pia inataka kuinunua klabu hiyo, atanunua klabu ya Magpies. (Telegraph - subscription required)

Mmiliki wa Leeds United Andrea Radrizzani amesema "ataangalia suala la kumleta mshambuliaji wa Uruguay, 33, Edinson Cavani katika klabu hiyo baada ya kupandishwa daraja na kuingia katika Ligi ya Premier. Cavani aliondoka Paris St-Germain msimu huu baada ya mkataba wake kumalizika. (Sky Sports Italia, via Football Italia)

Edinson Cavani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Leeds United inamsaka mshambuliaji wa Uruguay, 33, Edinson Cavani

Winga raia wa Austria wa Magpies ambaye yuko kwa mkopo Valentino Lazaro, 24, anafikiria mara mbili kuhusu kuondoka Inter Milan kabisa kwasababu ya kutopangwa kushiriki kweye mechi na St James' Park. (Chronicle)

West Ham itahitajika kubadilisha mkataba wa mkopo wa kiungo wa kati raia wa Czech Republic Tomas Soucek, 25, kutoka Slavia Prague hadi kuwa wa kudumu kwa pauni milioni 18.9 baada ya kuthibitishwa kwamba itaendelea kushiriki kwenye Ligi ya Premier. (Telegraph - subscription required)

Tetesi za Soka Jumanne

Juventus wanatafakari uwezekano wa kumnunua mkufunzi wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino kuchukua nafasi ya Maurizio Sarri kama kocha wao mpya. (La Stampa, via Mail)

Mauricio Pochettino

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, mkufunzi wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino

Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 25. (Guardian)

Manchester United wanatarajiwa kuwasilisha ofa ya £80m kwa Borussia Dortmund kumnunua winga wa England Jadon Sancho, 20. (Star)

Kiungo wa kati wa Arsenal Mjerumani Mesut Ozil, 31, amekataa ofa ya kujiunga na Fenerbahce inayoshiriki ligi kuu ya Uturuki . (Bild)

Mesut Ozil

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mesut Ozil, akiombe timu yake ushindi katika moja ya mechi zao

Chelsea watalazimika kumlipia kiungo wa kimataifa wa Slovenia Jan Oblak euro milioni 120 (£110m) ya kumruhusu kuhama ili kushinikiza mazungumzo ya ya uhamisho wa kipa huyo wa miaka 27- wa Atletico. (Goal)

Arsenal huenda wakaondoa masharti ya kulipa £40m katika mkataba wa mshambuliaji wa Sporting Joelson Fernandes ,17 katika kipindi cha saa 24 zijazo. (A Bola)

Licha ya dau lao kukataliwa, Tottenham wanamatumaini kuwa watakmilisha mchakato wa kumsajili beki wa Beijing Guoan na Korea Kusini Kim Min-jae, ambaye amepewa jina la 'Virgil van Dijk wa Korea Kusini'. (90min)