Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 20.07.2020: Sancho, Costa, Jimenez, Ceballos, Harrison, Luiz

Chanzo cha picha, Getty Images
Winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 20, huenda akahitajika kuanzisha mwenyewe hatua ya kutaka kuhamia Manchester United kwa kusema wazi kwamba anataka kuondoka klabu ya Ujerumani. (Mirror)
Juventus inachochea ung'ang'aniaji wa kumsaka mshambuliaji wa Brazil Douglas Costa, 29, katika ya Manchester City na Paris St-Germain na wanataka nafasi yake ichukuliwe na mshambuliaji wa Wolves na Mexico Raul Jimenez, 29. (Tuttosport)
Kiungo wa kati wa Arsenal raia wa Uhispania Dani Ceballos, 23, yuko tayari kumuomba rais wa Real Madrid Florentino Perez aongeze makubaliano yake ya mkopo na Gunners kwa msimu mwingine. (El Confidencial, via Express)

Chanzo cha picha, EPA
Leeds United ambayo ndio ya hivi karibuni kupandishwa daraja imethibitisha kwamba winga mwingereza wa Manchester City, Jack Harrison, 23, atasalia kwenye klabu hiyo kwa makubaliano ya mkopo kwa msimu mwingine. (Manchester Evening News)
Kiungo wa kati wa West Ham,16, Benicio Baker-Boaitey amepangiwa kujiunga na Bayern Munich na atasafiri hadi Ujerumani kwa mazungumzo, baada ya kukataa ombi la kusaini mkataba wa makubaliano ya mchezaji wa kulipwa na Hammers atakapokuwa anatimiza miaka 17 Januari. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Brazil Willian, 31, anayehusishwa na Tottenham, Arsenal na Manchester United - amefichua kwamba ni miongoni mwa watakaocheza mechi inayubisiriwa ya Chelsea kwa mkataba mpya baada ya kuomba makubaliano ya miaka mitatu na akapewa miwili. (De Sola, via Mirror)
Kocha wa Newcastle Steve Bruce anahofia kwamba bajeti yake ya msimu ujao itapunguzwa kwasababu mapato ya klabu hiyo ya pauni milioni 170 mwaka jana yatapungua kutokana na kupungua kwa malipo ya matangazo na kurejeshewa mashabiki pesa zao walizokuwa wamelipia tiketi za mechi msimu huo. (Mirror)

Chanzo cha picha, EPA
Kuimarika kwa mchezo wa mlinzi wa Brazil David Luiz, 33, huenda kukabadilisha mawazo ya Mikel Arteta wakati kocha huyo wa Arsenal anajitayarisha katika dirisha la usajili msimu huu. (Star)
Manchester United ilimpa Jude Bellingham na wazazi wake fursa ya kutembelea eneo la kufanyia mazoezi, huku Sir Alex Ferguson akiwepo, katika jaribio la kumshawishi kiungo huyo wa kati wa Birmingham, kufikia nao makubaliano lakini badala yake akachagua kwenda Borussia Dortmund. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tetesi za Soka Ulaya Jumapili
Ushawishi wa Tottenham kwa kiungo wa Southampton Pierre-Emile Hojbjerg, 24, umesababisha hali ya wasiwasi kuhusu mustakabali wa kiungo wa kati Harry Winks,24, katika klabu hiyo. (Sunday Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood, 18, atapata dili mpya Old Trafford kiasi cha pauni 40,000 kwa wiki ikiwa ni miezi tisa tangu kusaini mkataba wake. (Sun on Sunday)
Kocha msaidizi wa Aston Villa John Terry anafikiriwa na Bristol City kuwa kocha wao ajaye baada ya chaguo lao la kwanza Steven Gerrard kukataa kuhamia katika klabu hiyo. (Sunday Express)

Chanzo cha picha, Getty Images
Borussia Dortmund inataka dau la pauni milioni 115 kumuachia Jadon Sancho, lakini mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi anayehusishwa na taarifa za kuhamia Manchester United, amekataa kuondoka kwenye klabu hiyo ya Ujerumani (Sunday Express)
Manchester City wako kwenye mazungumzo na Gremio kuhusu dili la pauni milioni 4.5 kwa ajili ya kiungo wa kati Diego Rosa,17. (Mail on Sunday)














