Tetesi za soka Ulaya Jumapili 19.07.2020: Hojbjerg, Winks, Bielsa, Greenwood, Terry, Gerrard, Ancelotti

Chanzo cha picha, Getty Images
Ushawishi wa Tottenham kwa kiungo wa Southampton Pierre-Emile Hojbjerg, 24, umesababisha hali ya wasiwasi kuhusu mustakabali wa kiungo wa kati Harry Winks,24, katika klabu hiyo. (Sunday Mirror)
Mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood, 18, atapata dili mpya Old Trafford kiasi cha pauni 40,000 kwa wiki ikiwa ni miezi tisa tangu kusaini mkataba wake. (Sun on Sunday)
Kocha msaidizi wa Aston Villa John Terry anafikiriwa na Bristol City kuwa kocha wao ajaye baada ya chaguo lao la kwanza Steven Gerrard kukataa kuhamia katika klabu hiyo. (Sunday Express)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wako tayari kufikia dau la oauni milioni 40 kwa ajili ya mshambuliaji wa U17 Joelson Fernandes,17, anayekipiga Sporting Lisbon ambaye pia anazivutia Barcelona na Juventus (A Bola-in Portuguese)
Kocha wa Sheffield United Chriss Wilder amesema kuwa usajili wa mlinda mlango Wes Foderingham,29, hauna maana kuwa Dean Henderson ataondoka katika klabu hiyo na kuonesha matumaini kuwa mchezaji huyo,23, atasalia akichezea kwa mkopo kutoka Manchester United katika msimu mwingine. (Maii Sunday)
Chelsea bado haijaamua kuhusu kumsajili Henderson. (Sunday Express)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkurugenzi Mtendaji wa Leeds Angus Kinnear amesema kuwa wamiliki wa klabu watakutana na kocha Marcelo Bielsa juma lijalo kujadili kuhusu mkataba mpya na kufanyia kazi malengo ya usajili wakati wanaporejea ligi ya primia msimu ujao. (Sunday Express)
Zenit St Petersberg wako tayari kutoa ofay a pauni milioni 9 kwa ajili ya mchezaji wa nafasi ya ulinzi Dejan Lovren,31, lakini mabingwa hao huenda wakahitaji kitita cha takribani pauni milioni 15 kwa ajili ya mchezaji huyo, raia wa Croetia. (Mail on Sunday)
Villarreal imethibitisha kuwa Santi Cazorla amechagua kutoongeza mkataba na klabu hiyo, wakati kukiwa na tetesi kuwa kiungo huyo wa kati ,35, anaweza kurejea Arsenal. (Sunday Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Borussia Dortmund inataka dau la pauni milioni 115 kumuachia Jadon Sancho, lakini mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi anayehusishwa na taarifa za kuhamia Manchester United, amekataa kuondoka kwenye klabu hiyo ya Ujerumani (Sunday Express)
Manchester City wako kwenye mazungumzo na Gremio kuhusu dili la pauni milioni 4.5 kwa ajili ya kiungo wa kati Diego Rosa,17. (Mail on Sunday)
Kiungo wa kati wa QPR Bright Osayi-Samuel,22, anajiandaa kufanya vipimo katika klabu Bruges baada ya vilabu kukubaliana ada ya pauni milioni4.75. (Mail on Sunday)
Kocha wa Everton Carlo Ancelotti anaamini kuwa ataungwa mkono na bodi ya klabu katika kipindi cha dirisha la usajili baada ya kusema kuwa kikosi chake kinahitaji maboresho. (Sky Sports)












