Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 01.02.2020: Emery, Ighalo, Ings, Bale, Pukki, Richarlison, Salah

Unai Emery

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Unai Emery alitimuliwa kaziArsenal mwezi Novemba

Aliyekuwa meneja wa Arsenal Unai Emery anasema mashabiki wa Gunners "walimuondoa"katika klabu hiyo. (Marca - Spanish)

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy alisafiri hadi Uhispain kufanya mazungumzo na rais wa Real Madrid, Florentino Perez kufukuzia usajili wa winga wa Wales Gareth Bale, 30. (Times)

Leicester City wameonesha nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Southampton raia Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 24, ambaye kandarasi yake itakamilika katika kipindi cha miezi 18. (Ekstra Bladet - via Leicester Mercury)

Danny Ings celebrates scoring for Southampton

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Danny Ings amefunga mabao 14 msimu huu

Mshambuliaji wa Southampton Danny Ings, 27, alikuwa mada kuu kama mchezaji anayelengwa na Manchester United mwezi Januari. (Telegraph)

United badala yake imefikia makubaliano ya mkopo ambapo italipa theluthi moja ya mshahara wa wiki moja wa £300,000 wa mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo, kutoka kwa klabu yake Shanghai Shenhua. (Mail).

Manchester United pia inafikiria kuumsaka mchezaji wa Norwich na Finland Teemu Pukki, 29. (Independent)

Nemanja Matic

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nemanja Matic amekataa maombi ya kuondoka United

Kiungo wa kati wa Manchester United raia wa Serbia Nemanja Matic, 31, amekataa maombi ya kuondoka United na uko tayari kuongeza kandarasi yake iwapo klabu hiyo itaamua kufanya mazungumzo naye. (Telegraph)

Mlinzi wa England Ashley Young, 34, aliyejiunga na Inter Milan kjwa mkopo kutoka Manchester United mwezi January, amesema Antonio Conte alijaribu kumsajili alipokuwa meneja wa Chelsea. (Sky Sports)

Crystal Palace imeshindwa kufanya usajili wa washambuliaji wawili siku ya mwisho. Jarrod Bowen, 23, alijiunga na West Ham kutoka Hull huku Nathan Ferguson, 19, akisalia West Brom. (Mail)

Richarlison

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Richarlison alikuwa anahusishwa na uhamiaji wakati wa dirisha la usajili

Carlo Ancelotti amesema Everton itakuwa na wakati rahisi kukataa maombi ya Richarlison iwapo kutatumwa maombi ya kuhamia klabu nyengine wakati ujao. Raia huyo wa Brazil, 22, alikuwa anahusishwa na kuhamia Barcelona wakati wa dirisha la usajili. ( Liverpool Echo)

Christian Eriksen

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Christian Eriksen amejiunga na Inter Milan kwa kima cha £17m

Jose Mourinho anasema mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy alifikia makubaliano mazuri wakati wa kumuuza kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 27, kwa Inter Milan kwa kima cha £17m. (Evening Standard)

Kocha wa Man City Pep Guardiola anadai winga raia wa Ujerumani Leroy Sane, 24, anaichelewesha klabu kumpa mkataba wa muda mrefu. (Gurdian)

Manchester United ilishindwa kumsajili mshambuliaji wa Birmingham City Jude Bellingham, 16. (Mail)

Mashetani wekundu wamefanya mazungumzo na klabu ya Argentina San Lorenzo juu ya nia ya kumsajili mshambuliaji Adolfo Gaich, 20, kabla ya siku ya ukomo ya usajili. (Fox Sports Argentina - via Express)

Manchester City inataka kumsajili Coritiba, 17, mshambuliaji Yan Couto huku Barcelona ikijiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kuonesha nia ya kumsajili raia huyo wa Brazil. (Goal)

Mohamed Salah

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Salah alifunga mabao karibia 9 nine goals katika mechi 17 alizoshiriki za Liverpool msimu uliopita

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ametupilia mbali uvumi kuwa mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 27, huenda akaondoka Anfield mwishoni mwa msimu. (Liverpool Echo)

Real Madrid iko mbioni kumsajili mshambuliaji wa Ajax raia wa Denmark, Brian Brobbey, 17. (Mundo Deportivo - in Spanish)