Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 30.01.2020: Rakitic, Richarlison, Bale, Haaland, Jose, Piatek

Manchester United imefanya mwasiliano na Barcelona juu ya uwezekano wa kumsajili kiungo wa Croatia Ivan Rakitic, 31. (ESPN)

Beki wa kati wa klabu ya Napoli na timu ya taifa ya Senegal Kalidou Koulibaly, 28, hatahamia Ligi ya Primia mwezi huu licha ya kutakiwa na klabu ya Manchester United. (Sun)

Mshambuliaji Thomas Muller, 30, ambaye anawindwa na Manchester United anaweza kuondoka Bayern Munich baada ya kukosa uhakika wa kuanza katika kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya Ujerumani. (Bild - in German)

Tottenham wamefanya mazungumzo na Real Madrid juu ya uhamisho wa mshambuliaji Gareth Bale, 30. (Mail)

Mshambuliaji hatari na kinda wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Norway, Erling Braut Haaland, 19, ana kipengele cha mauzo cha pauni milioni 63 kwenye mkataba wake. (Bild - in German)

Haaland anaweza kuingizwa sokoni kwa ajili ya usajili baada ya msimu wa 2021. (Mail)

Everton wamekataa ofa ya usajili ya euro milioni 100 kutoka Barcelona kwa ajili ya mshambuliaji wao raia wa Brazil Richarlison. (Sky Sports)

Everton wanashikilia msimamo wao kuwa Richarlison, 22, hauzwi na wanapanga kuisuka timu yao upya huko mchezaji huyo akiwa nyota wa kikosi. (Liverpool Echo)

Mabingwa wa Uhispania Barcelona wanahangaika kutafuta streka mpya kabla ya dirisha la usajili kufungwa Ijumaa hususani baada ya Luis Suarez, 33, kupata majeraha. (Sport)

Atletico Madrid wamekataa kumnunua Cavani kwa zaidi ya Euro milioni 15 kutoka PSG. (Le Parisien - in French)

Timu ya David Beckham, Inter Miami, iliyopo kwenye Ligi ya Marekani imewasilisha ofa ya dakika za mwisho kutaka kumnunua Cavani. (AS - via NBC)