Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mahrez, Mane, Salah wawania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2019
Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf) watatoa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2019, leo Jumanne katika sherehe zitakazofanyika nchini Misri katika eneo la ufukwe la Hurghada.
Nyota wa Algeria na Manchester City Riyad Mahrez atakuwa akichuana na nyota wengine wawili wa Liverpool Sadio Mane wa Senegal na Mohamed Salah kutoka Misri.
Mane na Salah waliisadia klabu yao ya Liverpool kutwaa ubingwa wa Ulaya na kombe la dunia la vilabu.
Mahrez aliiongoza Algeria akiwa nahodha katika michuano ya kombe la mataifa ya Africa yaliyofanyika mwaka jana nchini Misri.
Hatua ya mwisho ya upigaji kura kwa tuzo za wanaume na wanawake,watachaguliwa na makocha wakuu/ Wakurugenzi wa ufundi na manahodha wa timu za taifa.
Wachezaji wa kiume wanawania tuzo
Mohamed Salah (Egypt & Liverpool)
Riyad Mahrez (Algeria & Manchester City)
Sadio Mane (Senegal & Liverpool)
Wanaowania kwa upande wa wanawake
Ajara Nchout (Cameroon & Valerenga)
Asisat Oshoala (Nigeria & Barcelona)
Thembi Kgatlana (South Africa & Beijing Phoenix FC)
Unaweza kusoma
Mchezaji kijana
Achraf Hakimi (Morocco & Borussia Dortmund)
Samuel Chukwueze (Nigeria & Villarreal)
Victor Osimhen (Nigeria & Lille)
Kocha bora wa mwaka
Aliou Cisse (Senegal - Senegal)
Djamel Belmadi (Algeria - Algeria)
Moïne Chaâbani (Tunisia - Esperance)