Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 01.01.2020: Ronaldo, Aubameyang, Chilwell, Calvert-Lewin, Dembele, Xhaka

Cristiano Ronaldo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Juventus kurefusha mkataba wa Cristiano Ronaldo hadi mwaka 2023

Juventus ina mpango wa kurefusha mkataba wa mshambuliaji nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo hadi mwaka 2023 - atakapokuwa na umri wa miaka 38. (Corriere dello Sport, via Mail)

Inter Milan imeingia katika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30. (Mirror)

Inter pia anataka kuilipa Chelsea £25m kumpata kiungo wa Italia anayecheza safu ya kushoto na nyuma Emerson Palmieri, 25. (Independent)

Mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Aubameyang alifunga mabao katika mechi zote za ligi ya Primia alizoichezea Arsenal mwezi Septemba

Chelsea na Manchester City wanatarajiwa kung'ang'ania saini ya beki wa Leicester na England Ben Chilwell, 23. (The i)

Mshambuliaji wa England wa chini ya miaka 21 Dominic Calvert-Lewin, 22, atasaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu ya Everton licha ya Manchester United kuonesha nia ya kutaka kumnunua. (Telegraph)

Paul Pogba

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kiungo wa Manchester United Paul Pogba

Ajenti wa Paul Pogba, Mino Raiola anasema uendeshaji wa kazi katika klabu ya Manchester United ni mbaya na kwamba hali hiyo "atawangamiza" baadhi ya wachezaji wazuri wa kandanda walio na talanta kama za kina Pele na Diego Maradona. (La Repubblica, via Times - subscription required)

Hertha Berlin imefikia mkataba wa kumsajili kwa mkopo kiungo wa kati wa Arsenal Uswizi Granit Xhaka, 27, wakitarajia kumchukua kabisa msimu ujao. (Independent)

Xhaka alijiunga na Gunners kutoka Borussia Monchengladbach mwezi Mei 2016

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Xhaka alijiunga na Gunners kutoka Borussia Monchengladbach mwezi Mei 2016

Kiungo wa kati wa Manchester United na Serbia Nemanja Matic, 31, amesema "hana uhakika" ikiwa atarefusha mkataba Old Trafford. (Telegraf - in Serbian)

Chelsea wanatafakari uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Moussa Dembele, 23. (Sky Sports)

Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anasisitiza kuwa mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha hatauzwa lakini amekiri kuwa klabu hiyo itatilia maanani dau la"kisawa sawa" la kumnunua kiungo huyo wa miaka 27 (Guardian)

Wilfried Zaha

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Zaha aliifungia Palace mabao 10 msimu wa 2018-19

Tetesi Bora Jumanne

Mazungumzo ya Chelsea kuhusu mkataba mpya wa mshambuliaji wa England Tammy Abraham yamekwama kwa sababu kiungo huyo wa miaka 22-anataka kulilipwa - £180,000 kwa wiki - sawa na winga Callum Hudson-Odoi, 19. (Goal)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amekubali kumpoteza kiungo wa kati wa England Adam Lallana, 31, mwisho wa msimu huu. (Telegraph)

Tammy Abraham

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Chelsea, Tammy Abraham anataka kulilipwa - £180,000 kwa wiki - sawa na winga Callum Hudson-Odoi

Mkufunzi mpya wa Arsenal Mikel Arteta anakabiliwa na kibarua kigumu kumshawishi mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, kusalia katika klabu hiyo badaa ya msimu huu utakapokamilia. (Telegraph)

Thierry Henry atakuwa mmoja wa watakaowania nafasi ya ukufunzi wa Barcelona ikiwa mkufunzi wa sasa Ernesto Valverde ataondoka klabu hiyo mwaka 2020. (Sport - in Spanish)

Everton wanaongoza kinyang'anyiro cha usajili wa winga wa Colombia James Rodriguez, 28, kutoka Real Madrid. (El Desmarque - in Spanish)

James Rodriguez

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Real Madrid haipo tayari kumpoteza nyota wa Colombia James Rodriguez

Aston Villa inataka kumsajili kiungo wakati wa Chelsea Danny Drinkwater, 29, kwa mkopo mwezi Januari January. Mchezaji huyo wa England kwa sasa yuko Burnley kwa mkopo. (Sky Sports)

Real Madrid inapania kumrudisha nyumbani beki wa Uhispania Jesus Vallejo, 22, kutoka Wolves mwezi Januari kwa sababu ya kukosa muda wa kucheza. (AS - in Spanish)