Eliud Kipchoge na Dalilah Muhammad wamechaguliwa kuwa wanariadha bora wa mwaka huu duniani

Chanzo cha picha, Getty Images
Eliud Kipchoge na Dalilah Muhammad wametajwa kuwa wanariadha bora wa kike na wa kiume mwaka huu.
Mkenya Kipchoge ,mwenye umri wa miaka 35 alishinda mbio za London Marathon kwa mara ya nne mwezi Aprili kabla ya kuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia mbio za Marathon chini ya saa mbili.
Alikimbia mbio hizo za kilomita 42.2 kwa saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika shindano la Ineos Challnge 1:59 mwezi Oktoba.
Muhammad , mwenye umri wa miaka 29 alishinda dhahabu katika mbio za mita 400 kuruka viunzi mjini Doha Qatar baada ya kuivunja rekodi ya dunia mara mbili mwaka huu.
Raia huyo wa Marekani ambaye alishinda ubingwa wa Olimpiki mjini Rio 2016 alisema: Umekuwa mwaka mzuri, Umekuwa mwaka mgumu lakini nashkuru sana, Sikufikiria kumaliza mwaka hivi.
Kipchoge ambaye alishinda taji la mwanariadha bora wa kiume kwa mwaka wa pili mfululizo , alisema: Nadhania ninawapatia moyo wanadamu. Ninafurahia kuweka historia. Natumai ilikuwa motosha kwa vizazi vijavyo.
Mwanariadha wa Ethiopia ambaye ni bingwa wa mbio za mita 5000 Selemon Barega alichaguliwa kuwa mwanariadha bora anayechipuka huku nyota anayechipuka wa Ukraine Yaroslava Mahuchikh ambaye alishinda medali ya fedha katika kitengo cha kuruka juu alishinda akiwa na rekodi ya wanariadha wasiozidi umri wa miaka 20 mjini Doha akishinda taji upande wa wanawake.

Chanzo cha picha, Getty Images










