Tetesi za soka Ulaya 28.09.2019: Eriksen, Pogba, Neymar, Mourinho, Higuain, Sane

Paul POgba

Paul Pogba ameiomba Man United kumpatia kandarasi mpya yenye thamni ya £600,000 kwa wiki . Kiungo huyo wa kati wa Ufaransa ,26, anajua kwamba ananyatiwa na Juventus pamoja na Real Madrid. (Tuttosport - in Italian)

Wachezaji wa Spurs wamekasirishwa na mkufunzi Mauricio Pochettino baada ya kusema kwamba walikuwa na ajenda tofauti wakati waliposhindwa na Colchester katika kombe la Carabao siku ya Jumanne.. (sun)

Manchester United inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27, huku Spurs ikijiandaa kutokosa huduma za kiungo huyo wa Denmark katika uhamisho wa bure mwisho wa msimu huu. (Goal)

Manchester United inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar na klabu yake ya zamani Barcelona bado hawajatatua mzozo kuhusu malipo ya uaminifu baada ya makubaliano ya kuzuia kuipeleka kesi hiyo mbele ya jopo la mahakama kugonga mwamba.. (Sky Sports)

Mawakili wanaomwakilisha Neymar na Barcelona wameafikia siku nyengine ya pili mnamo tarehe 21 Oktoba.. (ESPN)

Mchezaji wa Brazil Neymar, 27, alikuwa tayari kufutilia mbali kesi hiyo iwapo Barcelona ingejitolea kwa maandishi kumsaini tena. (Cadena SER - in Spanish)

Neymar JR

Mkufunzi wa Jose Mourinho anataka kurudi Real Madrid, baada ya kukataa ofa kutoka Monaco, Lille, Wolfsburg, Schalke na AC Milantangu alipofutwa kazi na klabu ya Manchester United mwaka uliopita . (Goal)

Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer amemchagua skauti wake wa kibinafsi kutazama wachezaji anaowalenga katika dirisha la uhamisho. (Sun)

Jose Mourinho anataka kurudi Real Madrid

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kwamba hana wasiwasi kuhusu hali ya kiungo wa kati wa timu hiyo James Milner, 33, kuwa katika mwaka wa mwisho wa kandarasi yake . (Guardian)

Mkataba wa sare mpya ya Liverpool inayodhaminiwa na kampuni ya sare za michezo una thamani ya £15m kwa mwaka ikilinganishwa na mktaba wao sasa na kampuni ya New Balance, ambayo inatoa £45m kwa mwaka. (Times)

Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Gonzalo Higuain, 31, ametoa ishara ya kutaka kurudi katika klabu yake ya zamani ya River Plate kandarasi yake itakapokamilika 2021. (Fox Sports Radio Argentina - in Spanish)

Gonzalo Higuain

Rais wa Bayern Munich Uli Hoeness anasema kwamba huenda klabu yake ikaimarisha upya hamu yake ya kutaka kumsajili winga wa Ujerumani na Manchester City Leroy Sane, 23, mwezi Januari. (Planet Futbol via Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21, anasema kwamba alivutiwa na hamu kutoka Man United msimu huu lakini anasisitiza kuwa makubaliano yoyote yatategemea klabu zote mbili.. (Times - subscription required)

Southampton na Manchester City zinamnyatia beki wa klabu ya Hearts mwenye umri wa miaka 17 Aaron Hickey. (Daily Record)

Leroy Sane

Aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa Manchester United na Chelsea Peter Kenyon anajaribu kumshawishi mmiliki wa klabu ya Newcastle Mike Ashley kuhusu mpango wa malipo wa kuinunua klabu hiyo kwa niaba ya wawekezaji wa Marekani. (Sun)

Peter Kenyon pia alifanya mazungumzo na kampuni hiyo ya uwekezaji MSD Partners, ambao wanainunua klabu pinzani ya Newcastle iliopo kaskazini mashariki Sunderland. (Mail)

Mkufunzi Steve Bruce anasema kwamba hajali kuhusu mazungumzo ya ununuzi wa klabu hiyo akitaja kuwa swala ambalo limekuwa likiendelea.". (Mirror)

Aston Villa imepewa £7m kumuuza mchezaji wa Ivory Coast onathan Kodjia, 29, na klabu ya Qatari Al-Gharafa. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Nice Lamine Diaby-Fadiga amekiri kumuibia mchezaji mwenza Kasper Dolberg saa yenye thamani ya ' Yuro 70,000 . (ESPN)

TETESI ZA SOKA ZA IJUMAA

Paul Pogba

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Paul Pogba

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, atachukua hatua mpya ya kuondoka mwezi Januari. (Sun)

Mkuu wa zamani wa Chelsea na Manchester United Peter Kenyon ameanza mchakato mpya wa kuinunua Newcastle kwa ushirikiano na mkewe kwa kumlipa mmiliki wake Mike Ashley pauni milioni 125 kwanza . (Mail)

Mkataba wa ununuzi huo unadai kuwa meneja wa Newcastle manager Steve Bruce amepata mafanikio "yasiyoweza kulinganishwa Ulaya ". (Sun)

Unaweza pia kusoma:

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, mwenye umri wa miaka 27,amewasili nchini Uhispania kwa ajili ya kesi dhidi ya klabu yake ya zamani Barcelona juu ya kusaini mkataba usio na malipo kuhusu faida. (Mundo Deportivo)

Neymar kuwasili Uhispania kwa ajili ya kesi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Neymar kuwasili Uhispania kwa ajili ya kesi

Barcelona na Atletico Madrid watakata rufaa juu ya uamuzi wa kuitoza faini Barca euro 300 (£265) kutokana na namna walivyowasiliana na mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann alipokuwa Atletico. (Marca)

Nahodha wa zamani wa England David Beckham amepanga kuwa wakala wa soka - huku mshambuliaji wa United Mason Greenwood, mwenye umri wa miaka 17, akiwa na uwezekano wa kuwa mteja . (mirror)

David Beckam
Maelezo ya picha, David Beckam

Manchester United wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Dembele, mwenye umri wa miaka 23, ambapo wametuma ujumbe wake kumfuatilia mchezaji huyo katika mechi tatu (Mail)

Fulham wanataka fidia ya pauni milioni 7 kutoka Liverpool baada ya kiungo wa kati Harvey Elliott mwenye umri wa miaka 16 kujiunga na Reds msimu huu. (Times - subscription required)

Unaweza pia kusoma:

Manchester United awako tayari kulipa pauni milioni 32 ili kutimiza kigezo kinachotakiwa kwa ajili ya meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino. (Sun)

Manchester United wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Dembele,

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Manchester United wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Dembele,

Crystal Palace wanaangalia uwezekani wa kumnunua mlinzi wa safu ya kati wa Shakhtar Donetsk Taras Stepanenko, mwenye umri wa miaka 30, baada ya kukosa fursa ya usaini mkataba na mchezaji huyo wa kimataifa wa ukraine kwa pauni milioni 8 msimu huu. (Sun)

Wachezaji wa Arsenal walipiga kura kuamua ni nani atakayekuwa nahodha wa kikosi hicho huku meneja Unai Emery akiangalia mkakati wa kujenga upya uongozi wake unaowahusisha watu watano katika timu . (Telegraph)

Harvey Elliott

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Harvey Elliott

Mshambuliaji wa England Tammy Abraham, mwenye umri wa miaka 21, "hakufurahia " kiwango ambacho FIFA ilimpa cha mchezaji nambari 20 baada ya kupokea "zawadi ya kipekee " katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea(Star)

Mshambuliaji wa Denmark Kasper Dolberg, mwenye umri wa miaka 21, aliibiwa saa ya pauni 62,000 katika kiwanja cha mazoezi cha Nice mwezi huu na mchezaji mwenza Lamine Diaby-Fadiga mwenye umri wa miaka 18-anashukiwa kuichukua . (L'Equipe - in French)

Unaweza pia kusoma:

Waandalizi wa Kombe la dunia 2022 nchini Qatar wamekamilisha mkataba ambao utawezesha kupunguzwa kwa bei ya pombe wakati wa mashindano ya kombe hilo. (Guardian)

Mwizi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lamine Diaby-Fadiga ameshutumiwa kuchukua saa ya thamani ya Mshambuliaji wa Denmark Kasper Dolberg

Newcastle wamekuwa wakimchunguza kwa karibu mlinzi wa Rochdale Luke Matheson mwenye umri wa miaka 16, aliyefunga bao dhidi ya Manchester United Jumatano , tangu alipojiunga na timu hiyo kwa mara ya kwanza mwaka jana. (Chronicle)

Huddersfield wanatumai kusaini mkataba na mlinzi Danny Simpson mwenye umri wa miaka 32-ambaye amekuwa huru tangu alipoondoka Leicester msimu huu . (Yorkshire Post)