Mapato ya mwaka ya Manchester United yaimarika, lakini je wataendelea kutambulika kama klabu tajiri duniani?

Marcus Rashford

Chanzo cha picha, Getty Images/AMA

Mapato ya Manchester United yameongezeka kwa rekodi mpya ya kiwango cha £627m kwa mwaka kufikia Julai.

Hii ni licha ya klabu hiyo kukabiliwa na msimu mgumu wa 2018-19 liochangia kuondoka kwa meneja Jose Mourinho na timu hiyo kumaliza msimu ikiw akatika nafasi ya sita.

Mapato yanayotokana na matangazo ya biashara yaliimarika kwa 18%, kutokana na mkataba mpya wa Uefa ya ligi ya mabingwa, huku mauzo ya kibiashara yakisalia kama yalivyokuwa.

Lakini timu hiyo inatarajia mapato na faida kushuka katika msimu wa 2019-20 baada ya kushindwa kufuzu katika ligi ya mabingwa msimu huu.

Klabu hiyo kwa sasa ni ya nane katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kuanza msimu kwa mchezo wa kiwango cha chini.

Inaiwacha nyuma ya Liverpool kwa pointi 10 na pointi tano nyuma ya mahasimu wa mjini na mabingwa watetezi Manchester City.

Kuna hatari kwa klabu hiyo kuishia nyuma ya wapinzani wake wa miaka mingi Ulaya kuipata haki ya kutambulika kuwa Klabu tajiri duniani.

Wiki iliyopita mabingwa wa Uhispania Barcelona walitangaza wanatarajia kupitisha kiwango cha mapato ya thamani ya £883m kwa mara ya kwanza msimu huu

'Kujijenga upya'

Licha ya kuongezeka kwa mapato hayo, naibu mwenyekiti wa Manchester United Ed Woodward amesema klabu hiyo inathamni ufanisi wa mchezo uwanjani kwa kiwango cha juu.

Amesema: "Tunaendelea kuuangazia mpango wetu wa kujijenga upya na uendelea kuimarisha mfumo wetu wa vijana, kwa mujibu wa falsafa ya klabu na meneja.

"Kila mtu anawajibika katika klabu ya Manchester United kuwasilisha lengo letu kuu la kushinda mataji."

Kwa mwaka huu wa kifesha, alitabiri mapato kukuwa kwa kati ya £560m hadi £580m, kiwango cha chini kutoka £627.1m, na faida kuu ya kati ya £155m hadi £165m, kutoka £185.8m.

Klabu hiyo imesema katika mwaka uliopita, imewasajili wachezaji watatu wa kikosi cha kwanza na imekamilisha mpango wa kuwaongezea mikataba wachezaji kadhaa wakuu.

Malipo kwa wachezaji

Imesema imetangaza pia mikataba 10 mipya au iliyosainiwa upya ya udhamini duniani na kwamba kwa kipimo cha Kantar - idadi jumla ya mashabiki wake na wafuasi wake duniani imeongezeka hadi bilioni 1.1 billion.

Katika mwaka huo klabu hiyo ya Old Traffordilipata faida kutokana na uhudumu ya £50m.

Malipo ya wachezaji kwa mwaka, yaliotumika pakubwa kwa wachezaji, yalikuwa ni £332.3m, ongezeko la £36.m, au 12.3%, katika mwaka uliopita, "kimsingi kutokana na uwekezaji katika kikosi cha kwanza cha wachezaji".

Klabu hiyo ilitumia zaidi ya nusu ya mapato yake kwa mishahara ya wachezaji, licha ya kampeni iliyoishia pasi kushinda mataji yoyote.